Pre GE2025 Tundu Lissu: Hatutashiriki Uchaguzi Mkuu bila Katiba Mpya na Tume Huru

Pre GE2025 Tundu Lissu: Hatutashiriki Uchaguzi Mkuu bila Katiba Mpya na Tume Huru

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Usiandike vitu kiholela tu.Hela ya wafadhili utatoa wewe?
Hakuna hela wafadhili waliwahi simamisha kisa Chadema kupigwa ban,pesa pekee nayoijua ni Ile ya USA ambayo hata Sasa haijatoka lakini zingine zote zipo.

Usiwe mjinga , Mabeberu hawana shida na Chadema bali interest zao.
 
Kuanzia sasa hatutashiriki tena kwenye chaguzi zijazo ukiwemo uchaguzi mkuu 2025 bila kuwa na Katiba mpya na mfumo mpya wa kidemokrasia wenye Tume huru ya uchaguzi na sheria mpya za uchaguzi tutashiriki huku tukijua kwamba Wapiga kura feki wataandikishwa, Wagombea wetu wataenguliwa, tutafanyiwa vurugu kwenye kampeni na siku ya uchaguzi, kura feki zitaingizwa na kura halali zitaibiwa, na Wagombea walioshindwa watatangazwa Washindi wa chaguzi hizo”

“Ukweli huu mchungu unatutaka tubadilishe mbinu za mapambano ya kidemokrasia, tumesubiri CCM na Serikali zake wabadilishe msimamo wao kuhusu Katiba mpya na Tume huru kwa miaka mingi, tumewabembeleza kwa muda mrefu wakubali Nchi yetu iondokane na Katiba ya sasa bila mafanikio”

“Kuhusu uchaguzi wa Chama chetu, Mwenyekiti wetu wa Chama na Mgombea mwenzangu wa Uenyekiti wa CHADEMA (Freeman Mbowe) amesema uchaguzi wetu wa Chama unatakiwa kuwa huru na haki nami naunga mkono maneno yake, bila uchaguzi huru Wanachama wetu hawatopata fursa ya kuonesha kuwa wao ndio wenye madaraka ya mwanzo na mwisho katika kuamua hatima ya Chama chetu, ili haya yatekelezwe tunahitaji kutafakari masuala yafuatayo”

“Napendekeza kuwa pamoja na Wazee Wastaafu wa Chama watakaopatikana kusimamia uchaguzi, Kamati Kuu iwaombe Viongozi wa Dini kuhudhuria mkutano mkuu kama Watazamaji ili kusaidia kuzuia mipango ya Waovu kuvuruga uchaguzi wetu, Kamati Kuu pia iwaite Wawakilishi wa Balozi mbalimbali nchini kushuhudia uchaguzi wetu” —— Mgombea wa Uenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu akiongea na Watanzania leo January 01,2025
Nani kamtuma sio maadhimio ya chama na labda kama atabakishwa baada ya uchaguzi!
 
Sawa ushauri mzuri asa kuhusu uchaguzi wa NDANI ya chama kaharika mabalozi na kiongozi wa dini
 
Hakuna hela wafadhili waliwahi simamisha kisa Chadema kupigwa ban,pesa pekee nayoijua ni Ile ya USA ambayo hata Sasa haijatoka lakini zingine zote zipo.

Usiwe mjinga , Mabeberu hawana shida na Chadema bali interest zao.
Usipende kutumia neno "mjinga"!Utakuja kutukana baba yako.
 
Mimi nawashangaa CHADEMA, huwa wanasema hayahaya kila baada ya kuchezewa rafu kwenye uchaguzi. Ila uchaguzi mwingine ukifika wao ndo wa kwanza kuwaambia watu kuwa ni busara kushiriki uchaguzi huo!
Hii hapa kutoka Mei 27, 2021.

Katiba mpya na mfumo mpya wa kidemokrasia wenye Tume huru ya uchaguzi na sheria mpya za uchaguzi tutashiriki huku tukijua kwamba Wapiga kura feki wataandikishwa,

Mchakato wa kuandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la Kudumu la Mpiga Kura.

Je vyama vya siasa vinahusishwa katika zoezi hili au vyama vipo katika vyombo vya habari kutoa matamko dhidi ya kambi pinzani ndani ya vyama vyao.

Huku mchakato wa uchaguzi kuelekea Oktoba 2025 Tume Huru ya Uchaguzi inatayarisha daftari bila vyama kutoa ushirikiano pengine ni chama dola kongwe CCM pekee ndiyo kinafuatilia mazoezi yote katika mchakato ambao umeanza wa uchaguzi Mkuu 2025:

31 December 2024
Songea, Ruvuma
Tanzania

TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI - INEC yataka wadau wa uchaguzi kuhamasisha watu kujitokeza kujiandikisha

View: https://m.youtube.com/watch?v=suMwZQHZ5V4
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekutana na wadau wake wa uchaguzi mkoani Ruvuma na kuwataka kuhamasisha wananchi wenye sifga kujitokeza na kuboresha taarifa zao katika daftari la Kudumu la Mpiga Kura......
1735739500226.jpeg

Uboreshaji wa Daftari​

Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya siku ya uteuzi. Wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao: -
  1. Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali;
  2. Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025;
  3. Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine;
  4. Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari;
  5. Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji; na
  6. Waliopoteza au kadi zao kuharibika.
Watendaji wa Uandikishaji/ Uboreshaji
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi hutumia watendaji mbalimbali wakati wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na:-
  1. Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa;
  2. Maafisa Waandikishaji;
  3. Maafisa Waandikishaji Wasaidizi;
  4. Waandishi Wasaidizi; na
  5. Mwenyesha Kifaa cha Bayometriki
Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura
Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.
Wajibu/Majukumu ya Mawakala wa Uandikishaji
  1. Kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
  2. Kushirikiana na Waandishi Wasaidizi kutambua wakazi wa eneo hilo na kutoa taarifa juu ya watu wasio na sifa.
Pamoja na majukumu tajwa, Mawakala wa Uboreshaji hawaruhusiwi kufanya yafuatayo:-
  1. Kuingilia shughuli za uendeshaji wa zoezi la Uboreshaji. Msimamizi wa kituo ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya nani anastahili kuandikishwa au kuboresha taarifa zake kwa mujibu wa Sheria.
  2. Kufanya kampeni za kisiasa katika kituo cha uandikishaji
  3. Kuorodhesha majina ya watu wanaojiandikisha.
Kiapo cha Kutunza Siri cha Mawakala wa Uandikishaji
Kila Wakala wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, ni lazima kula kiapo cha kutunza siri za taarifa za mwombaji au Mpiga Kura aliyeandikishwa. Wakala atakula kiapo mbele ya Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi. Hata hivyo, kutokuwepo kwa Wakala wa uandikishaji katika kituo cha kuandikisha Wapiga Kura hakuzuii utekelezaji wa majukumu ya Uandikishaji Wapiga Kura.
Watazamaji wa Uandikishaji
Kwa mujibu wa Kanuni za 46, 47, 48, 49, 50 na 51 (1) za Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Watazamaji wa ndani na kimataifa, wanaruhusiwa kutazama mchakato wa Uboreshaji utakavyofanyika katika vituo vya Uandikishaji.
Watazamaji wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutembelea vituo vya Uandikishaji, ni lazima waombe na kupatiwa idhini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Watazamaji. Aidha, Watazamaji 24 watakaoruhusiwa na Tume watapewa barua za kuwatambulisha kwa Maafisa Waandikishaji na Mwongozo wa watazamaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume. Maafisa Waandikishaji watatakiwa kuwapa barua za kuwatambulisha kwa Watendaji wa vituo ambavyo watavitembelea. Aidha, Watazamaji wa Uandikishaji wa Wapiga Kura hawapaswi kutoa maelekezo kwa Mwandishi Msaidizi katika kituo husika.
Kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura
Kwa mujibu wa Kifungu vya 11 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume inatakiwa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:
  1. Kulikagua Daftari;
  2. Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
  3. Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
  4. Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali
Kifungu cha 27 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024,kinaruhusu Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa Mwandikishaji au mtu yeyote aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura, kuweka pingamizi dhidi ya jina lililopo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura. Kifungu cha 28 Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, kinaweka utaratibu wa kuweka pingamizi. Mtu aliyewekewa pingamizi hutakiwa kupelekewa taarifa ili aweze kutoa ufafanuzi ndani ya siku saba (7).
Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Mahakama itapaswa kutoa uamuzi wa rufaa hiyo ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kupokea rufaa hiyo, uamuzi wa Mahakama ya Wilaya na iwapo aliyewekewa pingamizi hakubaliani na 25 maamuzi ya Afisa Mwandikishaji ya kuendelea kukataliwa kuwemo katika Daftari, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi Wilaya ndiyo utakuwa uamuzi wa mwisho na mtu hatoweza kukata rufaa katika Mahakama nyingine yoyote.
Source : Tume Huru INEC
 
Kuanzia sasa hatutashiriki tena kwenye chaguzi zijazo ukiwemo uchaguzi mkuu 2025 bila kuwa na Katiba mpya na mfumo mpya wa kidemokrasia wenye Tume huru ya uchaguzi na sheria mpya za uchaguzi tutashiriki huku tukijua kwamba Wapiga kura feki wataandikishwa, Wagombea wetu wataenguliwa, tutafanyiwa vurugu kwenye kampeni na siku ya uchaguzi, kura feki zitaingizwa na kura halali zitaibiwa, na Wagombea walioshindwa watatangazwa Washindi wa chaguzi hizo”

“Ukweli huu mchungu unatutaka tubadilishe mbinu za mapambano ya kidemokrasia, tumesubiri CCM na Serikali zake wabadilishe msimamo wao kuhusu Katiba mpya na Tume huru kwa miaka mingi, tumewabembeleza kwa muda mrefu wakubali Nchi yetu iondokane na Katiba ya sasa bila mafanikio”

“Kuhusu uchaguzi wa Chama chetu, Mwenyekiti wetu wa Chama na Mgombea mwenzangu wa Uenyekiti wa CHADEMA (Freeman Mbowe) amesema uchaguzi wetu wa Chama unatakiwa kuwa huru na haki nami naunga mkono maneno yake, bila uchaguzi huru Wanachama wetu hawatopata fursa ya kuonesha kuwa wao ndio wenye madaraka ya mwanzo na mwisho katika kuamua hatima ya Chama chetu, ili haya yatekelezwe tunahitaji kutafakari masuala yafuatayo”

“Napendekeza kuwa pamoja na Wazee Wastaafu wa Chama watakaopatikana kusimamia uchaguzi, Kamati Kuu iwaombe Viongozi wa Dini kuhudhuria mkutano mkuu kama Watazamaji ili kusaidia kuzuia mipango ya Waovu kuvuruga uchaguzi wetu, Kamati Kuu pia iwaite Wawakilishi wa Balozi mbalimbali nchini kushuhudia uchaguzi wetu” —— Mgombea wa Uenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu akiongea na Watanzania leo January 01,2025
Hatashiriki yeye Lisu na ACT Wazalendo.
 
Nchi hii hakuna kiongozi wa upinzani anaweza kushinikiza katiba mpya akafanikiwa kwa sababu hana watu bali ana mashabiki wa key board only.

Mbowe anaonekana mjinga lakini sio mjinga analilia maridhiano kwa sababu walau hata uchaguzi tu wa wabunge ukiwa huru CHADEMA inaweza kupata wabunge wengi wakaenda bungeni kupaza sauti.

Watanganyika bado wanelala usingizi wa pono na hawaamki leo wala kesho, wale wanaoonekana wamesoma wengi wao ni wajinga kupindukia ( rejea watu kama kina Slaa, Lwaitama hoja zao katika sakata la Lissu na Mbowe) wanaohitaji kuelimishwa upya kama alivyowahi sema Mtikila; hiki ukichanganya na tabia ya watanganyika ya kupenda kupata pesa kirahisi inaondoa uwezekano wowote wa upatikanaji wa katiba mpya walau kwa kizazi kimoja.

Niliwahi sema humu jf labda wanaozaliwa kuanzia miaka ya 2020 na kuendelea waje wawe watu wazima ndio waongoze kudai katiba moya lakini sio kizazi hiki tulichonacho.

Katika mazingira haya hakuna mwanasiasa wa upinzani atakayeleta maajabu ataishia kutoa maneno makali ya jukwaani basi.

Heri nusu shari kuliko shari kamili; hata hoja ya kudai tu mgombea binafsi ambayo ingekuwa rahisi kuipata tumeshindwa kuisimamia .

Katiba mpya maana yake CCM itaondoka madarakani na wana uhakika nalo asilimia 100, sasa utegemee wakubali kujinyonga ( suicide constitution and suicide electoral commission!).

Wapi Africa katiba mpya na electoral commission reforms zilipatikana bila shinikizo la wananchi walio hai ( sizungumzii wananchi maiti). Anzia kule Benin waliokuwa wa mwanzo kufanikiwa kuzipata,, Ghana, Malawi kwa rais wa maisha, Zambia ya Kaunda, Kenya, mk
 
Bila timu Tundu Lissu kuanza kujipanga kuanzia ngazi ya mashinani kwenye watu, ili kushiriki kila hatua za uandikishaji basi ni moja kwa moja imeshindwa kuhakikisha mchakato mzima wa uchaguzi ni (full proof) wa uwazi, huru na hautoi upendeleo:

Mbinu za chama cha Frelimo Mozambique zimetumika na zitatumika siku ya uchaguzi TAMISEMI 2024 kupitia chama dola kongwe CCM . Je ni mbinu gani ? kuhitimishwa tarehe 27 November 2024:

Kigogo wa Tume ya Uchaguzi Mozambique ktk mahojiano exclusive - Mchakato na Uchaguzi uligubikwa na uchafuzi

View: https://m.youtube.com/watch?v=2B_xQtuZLW8

Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Fernando Mazanga asema uchafuzi wa uchaguzi na uchafuzi wa mchakato wa uchaguzi, Tume haiwezi kusema nani alishinda..

Kwanza kiukweli kulikuwa na Tume mbili zinazosimamia mchakato, moja ni Tume ya Uchaguzi halisi isiyo na meno, na nyingine ni Tume Kificho ya Watu Wachache wa Frelimo waliokuwa na meno, rasilimali fedha na maamuzi ya kupika matokeo asema Fernando Mazanga

Alipoulizwa kuhusu Tume Kificho ya Watu wachache wa Frelimo ikifanyaje kufanya uchachuzi wa mchakato wa mzima wa matayarisho ya uchaguzi, uandikishaji na upigaji kura siku ya uchaguzi tarehe 9 Oktoba 2024 kigogo Fernado Mazanga alifunguka ...

Tume ya Ukweli ya uchaguzi ilinyimwa fedha na wizara ya fedha ya Mozambique na hata pesa zikipotolewa kidogo zote zikitumika makao makuu ya tume huku mikoani, wilayani na mitaani wasimamizi na wasimamizi uchaguzi walikuwa hoi si kifedha bali hata kimafunzo ya kuwapa uwezo wa kuandikisha wapiga kura, uteuzi na rufaa za mapingamizi.

Wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi walikuwa hawaelewi kanuni, sheria na miongozo ya kufanikisha uchaguzi ulio wa kiwango cha kukubalika ni huru, usiopendelea upande wowote na wakuweza kutoa matokeo sahihi ya kura zilizopigwa na mgombea yupi kazoa kura halali.

Fernando Mazanga anaongeza kuwa kutokana na Tume halisi kunyimwa uwezo wa kila aina, Tume kificho ya FRELIMO iliingia kazi kutangaza idadi ya watu waliojiandikisha ambayo haiwiani na takwimu za sensa ya taifa ya Mozambique ikiyofanyika 2023.

Wasimamizi wakuu na wasimamizi wasaidizi katika majimbo na wilaya walikosa kuwa na idadi za kulinganisha idadi ya watu katika maeneo yao ya majimbo, wilaya, kata na mitaa hivyo kura za ziada ya kuongezwa na FRELIMO ziliweza kutangazwa.

Huku wananchi hawafahamu idadi ya watu rasmo ktk maeneo yao kama sensa ya taifa ilivyokuwa ikionesha eneo kwa eneo, kijiji kwa kijiji, mtaa na kata.

Ingawa vyama makini vya upinzani zilipiga kelele kuwa idadi ya kuandikishwa watu katika sensa hailingani idadi ya wapiga kura watarajiwa na kura za matokeo yaliyotangazwa zimezidi kwa mbali idadi ya watu katika ripoti za sensa za taifa .

Wananchi baada ya kustuliwa kuhusu wafanye rejea za idadi ya watu na idadi ya wapiga kura wakabaini uchafuzi uliofanyika na kupelekea maandamano nchini Msumbiji kupinga matokeo yaliyotangazwa.

Mahakama ya Kikatiba iliyopewa mamlaka kusikiliza mapingamizi ya matokeo, imeomba tume ya uchaguzi ya taifa iwasilishe nyaraka ili ukaguzi ufanyike. Tume ilipewa siku 8 iwe imewasilisha nyaraka zote za uchaguzi uliofanyika 9 Oktoba 2024 zipitiwe na kufanyiwa ukaguzi wa kina.

Bw. Fernando Mazanga Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Mozambique anasema siku 8 zimepita na zinaonesha kuwasilishwa nyaraka zote zilizohifadhiwa katika Ofisi za Majimbo na Wilaya.

Lakini pamoja na nyaraka hizo kukusanywa sehemu, Mahakama ya Kikatiba hawajapewa makaratasi hayo ya kura na rejister za wapiga kura leo.

Inasemekana serikali inalaumu kutofika makaratasi hayo kutokana na vurugu za maandamano, lakini kigogo huyo Fernando Maganza anatillia shaka sababu hiyo kuwa vurugu zimezuia katatasi hizo kufika mji mkuu wa Mozambique Maputo.

Pengine Tume fiche ya Uchaguzi ya FRELIMO imeshikilia makaratasi hayo katika kituo salama (safe house) ikiyapitia matokeo hayo ya uchafuzi wa uchaguzi na kujiuliza wayawasilishe au la. Pia wanatafuta njia nyingine ya kuingilia mchakato wa Mahakama ya Kikatiba n.k n.k kujiokoa kutoka skandali hilo zito.

Fernando Mazanga alipoulizwa kama matokeo yanaweza kufutwa kutokana na uchafuzi wa wazi wa mchakato na uchaguzi sawia, kigogo huyo mzalendo wa Tume Halisi ya Uchaguzi anasema hawezi kutoa mawazo yake sasa kwa kuwa yeye ni mtu wa ndani kabisa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mozambique.

Hivyo anaiachie Mahakama ya Kikatiba ibebe majukumu yake kuhakiki na kutoa hukumu sahihi baada ya kujiridhisha na ushahidi wote anahitimisha naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchi Mozambique Bw. Fernado Mazanga.

Muito Abrigado kwa kutusikiliza
Source : DW Português para África : DW Kireno Africa

More info :
Maputo, Mozambique
Mahakama ya Katiba Mozambique yataka wasimamizi wa uchafuzi wa uchaguzi kujitetea madudu ya wazi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa 9 Oktoba 2024 nchini Mozambique
1735740046928.jpeg

Picha : Waheshimiwa majaji wa Mahakama ya Kikatiba Mozambique
 
CHADEMA Kibamba wajaribu kubana mchakato wa kuelekea uchaguzi wa TAMISEMI 2024 hadi siku ya mwisho, lakini matokeo ya uchaguzi yakapinduliwa.

Je timu Tundu Lissu kukiwepo Reform na Election badala ya No Reforms No Election halafu matokeo kama ya Kibamba yenye takwimu zote kakini serikali ya CCM ikaamua kutangaza matokeo, CHADEMA ya Tundu Lissu itachukua hatua gani? Je watanzania pia watajitokeza kuandamana kupinga matokeo ?

TOKA MAKTABA:

JUHUDI, JITIHADA NA SAYANSI YA KUSHINDA UCHAGUZI WA TAMISEMI 2024, ZILIVYOSHINDWA KWA TAMKO LA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WA SERIKALI

Mhe.Mchengerwa amesema kuwa taarifa ya jumla itatolewa ifikapo saa sita usiku leo muda hautaongezwa.

CHADEMA JIMBO LA KIBAMBA DSM WATOA TAKWIMU. ZIMETOLEWA MAJIRA YA SAA NNE USIKU TAREHE 20 OCTOBER 2024

Pongezi CHADEMA Kibamba jijini Dar es Salaam Tanzania kuwabana chama kongwe dola kwa kutoa takwimu za wapiga kura waliojiandikisha kwa ajili ya uchaguzi serikali za mitaa 20q4 :
JIMBO LA KIBAMBA DAR ES SALAAM IDADI WAPUGA KURA WALIOJIANDIKISHA KATIKA VITUO :

Kinganzi A 1886
Kiganzi B 3,400
Kwembe 2964
Lunguruni 2773
Mlonganzila 1772
Mpakani 2236
Msakuzi 1,834
Ngeteni
Kibamba
Gogoni 2,310
Hondigo 2637
Kinamba 3238
Kibwegere
Kiluvia 2105
Salanga Vituo 32 :
Kimara B 2,645
Kingongo 2,658
Matangini 4,221
Michungwani 2261
Mji Mpya 3843
Salanga 3960
Stop Over 2464
Ukombozi 1,337
Upendo 2437

Msigani 3947
Yusufu 2411
Malamba mawili 4379
Msingwa 3068
Temboni 1,751
Mbezi
Luis 3558
Makabe 3365
Mbezi Luis Centre 3788
Mpigi Magohe 3077
Msakuzi 3493
Msakuzi Kusini 2087
Mshikamano 3795
Msumi 4312

Tegeta 4430
Kunguru 2705
Muungano 2489
Matosa 3023
Kulangwa 2124

Takwimu za mitaa 40 kati ya 44, CHADEMA tumeamua kutangaza takwimu hizi ili zisiwe tofauti na takwimu za TAMISEMI.

Idadi hii tumepata kutoka kwa wasimamizi wasaidizi tulizopewa kupitia mawakala wetu. Na kesho tunategemea takwimu zitakazobandikwa katika kuta za vituo zitafanana na takwimu tulizoziona katika madaftari ya wapiga kura jimbo la Kibamba Dar es Salaam

View: https://m.youtube.com/watch?v=PYvgsf30q-Y
 
Back
Top Bottom