Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
Kuna chaka ambalo linataka kutumika katika maridhiano la kumuahidi Umakamu wa Rais au Uwaziri Mkuu Tundu Lissu kama sehemu ya kumpoza na kurudisha imani ya Jumuiya ya Kimataifa ambayo kwa kika siku inayokwenda wanazidi kukaza kamba.
Hili chaka ka kuzawadia watu Umakamu wa Rais au Uwaziri Mkuu limetumika nchi nyingi za Africa lakini mwisho wa siku tumeona limedumaza juhudi za kweli za kuleta haki na demokrasia katika nchi hizo.
Lissu ni Mwalimu na Mwanafunzi mzuri wa Historia. Ameshuhudia na kujifunza kilichowapata wengine waliozawadiwa vyeo hivyo kuanzia Zimbabwe, Kenya hadi Zanzibar na nini kilifuata katika harakati zao. Lissu hatakubali kuwa muathirika mwingine wa njama hizo za kisiasa.
Kwanza wanaopanga njama hizo wakumbuke Katiba hairuhusu hilo na kama wako tayari kubadili kipengele hicho ni afadhali wafumue Katiba nzima ili isukwe upya kama ambavyo wengi wamekuwa wanapendekeza kwa muda mrefu.
Hata mkimuahidi Uwaziri Mkuu bado sitegemei Lissu atakubali maana nia itakuwa kumuweka karibu na kummaliza taratibu. Tukumbuke pia, wengi waliopewa vyeo hivyo kwa mtindo huo huwa wanafariki ndani ya miaka michache mbele.
Ndiyo maana mnaona mpaka leo kesi yake imekwama na haijulikani hatma yake.