Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Badala ya kujikita kushambulia maridhiano ni vyema Tundu Lissu aeleze sasa atafanya nini akichaguliwa kuwa mwenyekiti ikiwa aina ya chaguzi zilizofanyika 2019, 2020 na 2024 zinaendelea. Ikiwa wanachama wa chama chake wataendelea kupotea, kukamatwa na kufunguliwa kesi za kisiasa.
Tundu Lissu anajisifia kwamba alikataa mialiko yote ya CCM na serikali wakati Freeman Mbowe akiwa gerezani lakini hasemi alifanya nini zaidi ya hilo na kupiga kelele tu.
Tundu Lissu ana uwezo wa kuwashawishi Wanachadema wenzake au Watanzania kwa ujumla washinikize mabadiliko kwa njia yoyote? Mimi siamini kama huo uwezo anao. Angalau Mbowe alijaribu maridhiano.