Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, ilani yako na CHADEMA itahitaji msaada zaidi ya asilimia 90, tutarudi utumwani

Tatizo lako kubwa hujui hata kodi inalipwa lini,baada ya kujenga na kuanza biashara au wakati wa kujenga kiwanda.

Ukweli ni kuwa baada ya kumaliza ujenzi mwekezaji huruhusiwa kutoa gharama za ujenzi kama gharama kabla ya kodi (tax allowable expenses-investment cost) na ndio maana wengi wenye viwanda vipya hulipa corporate tax ndogo au hawalipi kabisa kwa miaka ya mwanzo ili kurudisha gharama za uwekezaji.
 
Umeisoma vizuri ilani ya CHADEMA? sehemu gani inazungumzia ujenzi wa viwanda? sikumsikia jana akizungumzia ujenzi wa viwanda tofauti na kuingiza bidhaa nchini kutoka nje ili watu wasiende kununua tena Uganda, sisi tunajenga uchumi shindani tukauze bidhaa nje tukuze pato la nje yeye anaahidi kufuta ushuru wa bidhaa za nje ili tutumie fedha za kigeni kuziingiza kwa wingi, afisa masoko wa mabeberu huyo.
 
Masisiem yanahangaika kweli kweli,pesa iko nyingi sana ,hizo pesa za kununulia ndege zitafanya hiyo kazi cdm hatuna ujinga wa kununua mandege yasiyomsaidia mwananchi,pesa za ruzuku kuendeshea shirika la ndege zitatekeleza sera ,pesa zinazopelekwa kwenye ma sgr na stiglaz zitatumika haku cdm hakuna mjinga wa kutenga 2/3 ya bajeti ya wizara au 1/3 ya bajeti kuu kutekelea miradi 2 huu ujinga wanaweza ufanya ccm tu..
Kwa hiyo mtoa post chagua cdm ,haki,maendeleo na ustawi achana na sera za kijima za ccm jana eti tutanunua ndege 5 sijui viwanja vya mpira mara uchumi 8% wakati kaushusha kutoka 7% to 5%
 
Yaani Lissu anaongea vituko tu,amekariri sheria tu mambo ya uchumi hakuna kitu.
Humu ndio anashabikiwa mno pengine hakuna kitu.
Wananchi sio wajinga.
Magufuli ameweza my friend,so acha aendelee na drama.
 
Hao wenyewe ni washangiliaji,hawasikilizi kuelewa.
 
Chanzo kikuu cha pesa za serikali ni kodi;Tundu Lissu kasema anafuta ili wafanyabiashara wawe na hela kuliko serikali
 

..uko kisiasa-siasa zaidi.

..wawekezaji huzingatia masuala yote ya kikodi kabla ya kuchukua maamuzi ya kuwekeza ktk eneo husika.
 
Hatokusanya Kodi kandamizi bali atakusanya kodi rafiki kutoka kwa wafanyabiashara .Acheni kupotosha.
 
Niliwahi sema tungeenda mwendo wa Jk usingekuta kuna kilio kikubwa ha ugumu wa maisha na kukosa ajira maana JK alijikita kwenye demand side policy kwa kuimarisha kipato cha mtu mja mja ili iwe chachu ya aggregate demand ambayo automatically itapelekea production via investments maana tayari kuna soko/consumer demand ni kubwa.
Sasa huyu jamaa kaua kipato cha watu matokeo yake hakuna kinachofaulu wazalishaji wachache kwa vile walaji hakuna na ameishia kuendesha nchi kwa mikopo kuliko kiongozi yoyote aliyewahi kuongoza nchi,tuachane na huyu anatutia umaskini
 

..suala la kodi litawahusu wanaozalisha bidhaa nchini, na wanaoagiza bidhaa kuleta hapa nchini.
 
..mfumo wa sasa hivi umejikita ktk kukamua watu wachache kwa kodi na hauchochei wananchi wengi zaidi kuanzisha biashara.
Akiwa Mbeya nadhani...alisema atafuta kitambulisho cha machinga. Sasa hapo anaongeza wigo wa kodi ama anapunguza wigo huo!?
 
Chanzo kikuu cha pesa za serikali ni kodi;Tundu Lissu kasema anafuta ili wafanyabiashara wawe na hela kuliko serikali
Anafuta mlolongo au utitiri wa kodi na kuacha 1tu pengine VAT na mapato mengineyo kama huko kwenye utalii lakini pia ataiondoa serikali kufanya biashara kama ilivyo saizi eti serikali inaanzisha sijui parking sijui hotel na upuuzi mwingine wa dizaini hii
Lengo la hii sera ni kuimalisha kipato kwa mtu mja mja awe mkulia au mfanyabiashara nk ,hii itachochea automatically investments ambayo itaoa ajira na kodi zaidi kwa serikali..Kwanz ahakuna mfanyabiashara anaweza kuizidi pesa serikali kwa bongo hii,hii haipo
 
Hatokusanya Kodi kandamizi bali atakusanya kodi rafiki kutoka kwa wafanyabiashara .Acheni kupotosha.
Hayo ni maneno yake mkuu weka video ya jana hapa tuone, kasema TIN TRA ni bure hivyo hata hiyo 20,000/= wanayotozwa wafanyabiashara wadogowadogo kwa mwaka no wizi yeye ataifuta hivyo watafanya biashara bure, wafanyabiashara wengine wako na kodi 15 ambazo wala hakuzitaja akasema yeye akiingia atazifuta, na bidhaa kutoka nje zitaingia bure zitamwagika nchini (ataifanya nchi dampo), watu hawatahangaika kwenda Uganda kununua bidhaa, sasa wenye akili tukijiuliza haya na kwa wafanyakazi akasema payee haitazidi 8% which means yaweza kuwa 2%, hayo makubwa anayoahidi atayafanya vipi bila kodi? hakuna jibu tofauti na KUTUUZA.
 
Development should be people centered!!!

Maendeleo lazima yaendane na Uhuru. Upuuzi wakujenga uwanja chattle hauvumiliki hata kidogo, kejeli za kuwatukana wahitimu kuwa wajitolee ndio waajiliwe ni upuuzi.
 

..mbona Jpm anatoa matrilioni ya kodi za waTz kwenda kununua midege toka kwa mabeberu?

..na midege yenyewe inatutia hasara kila mwaka kwanza kwa kuinunua, na pili kutoa ruzuku kwa shirika la ndege?

..Je, Jpm ni wakala wa mabeberu? Kuna nini kati yake na makampuni ya kutengeneza ndege? Kwanini analazimisha manunuzi ya ndege wakati zinatutia hasara na kutubebesha mzigo wa kuendesha shirika la ndege?
 
Kwani hizi kodi wakati wa JK zilikuwepo?Na mapato ya hizi fedha yanaeleweka yanapokwenda?
 
Kodi ipi? Kwa sababu kodi ambayo wao hulipa direct ni corporate tax labda kama unajua nchi inayotoza asilimia pungufu zaidi ya Tanzania.

Pili,nimekuuliza atafanyaje kufidia mapato yatakayoondoka baada ya kufuta kodi? atafanya mbinu gani kufidia nakisi ya bajeti,sikusikia akiainisha vyanzo vya mapato kuendesha serikali.Hapa ndipo hasa kwenye msingi wa mjadala kamanda
..uko kisiasa-siasa zaidi.

..wawekezaji huzingatia masuala yote ya kikodi kabla ya kuchukua maamuzi ya kuwekeza ktk eneo husika.
 
Akiwa Mbeya nadhani...alisema atafuta kitambulisho cha machinga. Sasa hapo anaongeza wigo wa kodi ama anapunguza wigo huo!?

..wamachinga wana kipato kidogo sana hawatakiwi kutozwa kodi ya vitambulisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…