Pre GE2025 Tundu Lissu: Ili CHADEMA iaminike, ipendwe na kuthaminiwa tena na Wananchi ni lazima ipate Nahodha Mpya, kwa sasa haiaminiki na Jamii!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CDM itapotea kabisa kuwa na mtu kama huyo - wajumbe malizeni kazi mapema mkinusuru chama chenu kutekwa na watu wa ajabu ajabu.
Jamaa anatuaminisha watanzania kwamba CDM haipendwi na haiaminiwi tena na wamanchi na Tanzania.

Huyu jamaa hana nia njema na chama chenu.
Kwa hiyo wewe unaona CDM inaaminiwa na Wananchi kama ulivyokuwa kabla ya 2015?. Jifunze kuupokea ukweli mchungu!
 
Uzuri wa lissu ni ukweli na uwazi, ukweli mbowe kwa sasa ushawishi umepungua Sana hasa kwa vijana na umma kiujumla, Mbowe kwa miaka 20+ imetosha abaki kuwa mshauri.Nje ya hapo chadema wasitafute mchawi
 
Kwa hiyo wewe unaona CDM inaaminiwa na Wananchi kama ulivyokuwa kabla ya 2015?. Jifunze kuupokea ukweli mchungu!
Watanzania wamedanganywa kwamba siasa ni uwongo na kupindisha maneno, matokeo yake watu wanaamini siasa ni ujanjaujanja...
 
Angejiuzulu nafasi ya makamu mapema ningeelewa hii hoja yake. Pia asingekuwa amechukua form ya kugombea nafasi ya makamu ningeelewa zaidi hii hoja yake.
Kilichobaki sasa ni kuwaaminisha wafuasi wake kuwa yeye anauwezo mkubwa kuliko wengine. Na akifanikiwa kuwa kiongozi kwenye hicho chama chao atapoa kama ilivyokuwa kwa kiongozi wa TLS.
Mara nyingi ukiwa nje ya ulingo unaona vizuri sana ila ukishaingia kwenye mfumo utaona tofauti na unavyoona ukiwa nje.
Na hakuna mfuasi wa Lissu yupo tayari kusema Lissu alifanya kitu gani TLS kama Rais wake. Zaidi alikuwa white elephant ofisini!
 
Sawa, akishindwa akaungane na vyama vingine au aanzishe cha kwake na wafuasi wake tuone atafika wapi.
Uongozi sio one man show, lazima ukubali mchango wa kila mmoja. Anayekosea aadhibiwe kulingana na kanuni na taratibu za chama na sio kubwatuka kwenye vyombo vya habari.
Sasa unaongea upuuz gani. Huyo ayatollah si ndio one man show. Lissu hana u one man show
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lissu amesema kwa sasa chama chao kimepoteza Imani kwa Wananchi

Lissu amesema ili Chadema iaminike ppendwe na kuthaminiwa tena na Wananchi ni Lazima ipate Nahodha mpya

Mlale Unono 😄
Huo ndio ukweli, cdm imepoteza imani hadi kwa wanachama wake.
Mbowe amekuwa kigeugeu na mtu asiyeaminika,wengi wanamuona kama chawa wa ccm
 
Sawa, akishindwa akaungane na vyama vingine au aanzishe cha kwake na wafuasi wake tuone atafika wapi.
Uongozi sio one man show, lazima ukubali mchango wa kila mmoja. Anayekosea aadhibiwe kulingana na kanuni na taratibu za chama na sio kubwatuka kwenye vyombo vya habari.
Mbona unepaniki? Relax dogo. Usultani utakomeshwa soon na dunia itajifunza demokrasia kwa vitendo kupitia cdm
 
CDM itapotea kabisa kuwa na mtu kama huyo - wajumbe malizeni kazi mapema mkinusuru chama chenu kutekwa na watu wa ajabu ajabu.
Jamaa anatuaminisha watanzania kwamba CDM haipendwi na haiaminiwi tena na wamanchi na Tanzania.

Huyu jamaa hana nia njema na chama chenu.
Ukweli mchungu CDM hakipendwi tena na vijana
 
Back
Top Bottom