Pre GE2025 Tundu Lissu: Ili tuweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa Kura!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jamani tuwe wakweli, tulifanya maandamano ya AMANI Dar Mbeya Arusha nk tena tukapewa na ulinzi wa polisi.
 
Duh!,operation ya kibiti ndiyo ya kujisifia,mwaka huu lazima tugawane mbao tu,subir hiyo octoba ifike
 
Usajili wa vijana wa kwenda front line unaanza lini??? Atangaze ajira watu hatuelewi mtaani uku
 
Nchi yetu ni ya Amani na itazidi kuwa ya Amani milele MUNGU alie hai atatulinda na hizi roho za machafuko zisizotaka amani. Duniani viumbe vyote tu wapitaji tu kwa hiyo hata wao pamoja na kiburi chao chote pia mwisho wao upo tu hatuhitaji huo ujinga wa bunduki katika nchi yetu iliyobarikiwa amani.
 
ATAPOKUJA KUSHIKWA NA VYOMBO VYA DOLA KWA UCHOCHEZI MSIJE MKAANZA VIJINENO.
Sababu hayo maneno ni hatarishi ya usalama wa nchi
 
Tanzania hakuna amani. Nchi ambayo watu wanatekwa mchana kweupe, hiyo haina amani
Watu kutekwa ipo nchi nyingi.
Hutekwa sababu za kisasi au kubiashara au kutaka viungo vya mwili au wivu na mengineyo.

Hata vyama vya siasa vinaweza kutekana wenyewe.
 
Hata hivyo,
movement hiyo haramu ya kuhubiri na kuchochea chuki na migawanyiko miongoni mwa waTanzania, itasaidia sana na kuvipa fursa na nafasi muhimu, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na mamlaka ya mawasiliano nchini kujipanga vizuri zaidi, ili kukabiliana ipasavyo kwa mujibu wa sheria na vibaka hao na matapeli wa kisiasa wanaopanga uovu huo kwa mwamvuli wa kufanya siasa, lakini wanalenga kuvuruga umoja, amani na utulivu wa waTanzania, wanaofanya kazi na shughuli zao mbalimbali za kijamii, kisiasa na kiuchumi nchini, hususani kuelekea uchaguzi mkuu wa kihistoria mapema october mwaka huu2025.

Ni muhimu sana,
waTanzania wote na dunia nzima kufahamu wazi kwamba, umoja, amani na utulivu wa waTanzania utalindwa kwa nguvu zote na kwa gharama yoyote ile.

Fyoko fyoko za kuvuruga amani ya waTanzania, hazitavumiliwa hata sekunde moja, iwe ni mitandaoni au mitaani.
Epuka kujiambatanisha na magenge ya kihalifu, matapeli na vibaka wa kisiasa nchini.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Kwani CCM inazo bunduki? Usikurupuke siasa hauwezi kuitafsiri hivyo ukaielewa.
 
Mnavyobubujikwa na machozi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…