Pre GE2025 Tundu Lissu: Ili tuweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa Kura!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Maandamano ya Amani atakupa nani ruhusa hiyo ikiwa wenye bunduki ndio watoa ruhusa. Dhamira ya maandamano ikiwa kinyume na kumsifia malikia huwezi pewa kibali kamwe.

Utalazimisha watasema unataka kuleta tahatuki mwisho uvunjwe miguu na mabunduki na mabomu ya machozi.
Jamani tuwe wakweli, tulifanya maandamano ya AMANI Dar Mbeya Arusha nk tena tukapewa na ulinzi wa polisi.
 
Naona anakaribia kujaa sehemu ambayo watu wengi walikuwa wanamsubiri ajae, hakika atajuta, na hatapata wa kumsaidia. Akaulize Kibiti ndio atajua nchi hii inafanyaje special operations. Hiyo afya kidogo aliyobakiza anaweza kuikosa. Na anaweza kupigwa kesi ugaidi halafu hakuna mtu atafanya kitu, na chadema ikafutwa.

Nadhani waliosababisha Mzee Kibao akafa wameanza kuongea
Duh!,operation ya kibiti ndiyo ya kujisifia,mwaka huu lazima tugawane mbao tu,subir hiyo octoba ifike
 
Usajili wa vijana wa kwenda front line unaanza lini??? Atangaze ajira watu hatuelewi mtaani uku
 
Nchi yetu ni ya Amani na itazidi kuwa ya Amani milele MUNGU alie hai atatulinda na hizi roho za machafuko zisizotaka amani. Duniani viumbe vyote tu wapitaji tu kwa hiyo hata wao pamoja na kiburi chao chote pia mwisho wao upo tu hatuhitaji huo ujinga wa bunduki katika nchi yetu iliyobarikiwa amani.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumzia harakati za 'No Reform No Election' amedai kuwa "Ilituweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa kura"

"Watu wetu wa leo ni welevu kuliko miaka 10 iliyopita, mwaka jana mliweka wagombea wa nafasi zote zinazogombaniwa hapa Kibamba na sehemu kubwa walienguliwa, mkatumia nguvu kubwa kuwarudisha, wakarudishwa baadhi alafu siku ya tarehe 27 mkashughulikiwa vizuri zaidi, matokeo yakatangazwa kwa mitutu ya bunduki ndio maana hamna Mwenyekiti wa mtaa hata mmoja, sio kwasababu mmekuwa wajinga kuliko mlivyokuwa miaka 10 iliyopita ni kwasababu sasa hivi ilitushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao"

Lissu ameendelea kwa kusema: "Katika mazingira ya uchaguzi wa sasa ili tushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao, ili wasiweze kutumia bunduki zao kuingia vituoni kwa nguvu na kuchukua masanduku ya kura kwa nguvu,"

Lissu amehoji: "kama na sisi tukiwa na bunduki hiyo nchi itakuwaje?, patakua na pakukaa hapo?, ndivyo wanavyotaka?

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

ATAPOKUJA KUSHIKWA NA VYOMBO VYA DOLA KWA UCHOCHEZI MSIJE MKAANZA VIJINENO.
Sababu hayo maneno ni hatarishi ya usalama wa nchi
 
Tanzania hakuna amani. Nchi ambayo watu wanatekwa mchana kweupe, hiyo haina amani
Watu kutekwa ipo nchi nyingi.
Hutekwa sababu za kisasi au kubiashara au kutaka viungo vya mwili au wivu na mengineyo.

Hata vyama vya siasa vinaweza kutekana wenyewe.
 
Hata hivyo,
movement hiyo haramu ya kuhubiri na kuchochea chuki na migawanyiko miongoni mwa waTanzania, itasaidia sana na kuvipa fursa na nafasi muhimu, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na mamlaka ya mawasiliano nchini kujipanga vizuri zaidi, ili kukabiliana ipasavyo kwa mujibu wa sheria na vibaka hao na matapeli wa kisiasa wanaopanga uovu huo kwa mwamvuli wa kufanya siasa, lakini wanalenga kuvuruga umoja, amani na utulivu wa waTanzania, wanaofanya kazi na shughuli zao mbalimbali za kijamii, kisiasa na kiuchumi nchini, hususani kuelekea uchaguzi mkuu wa kihistoria mapema october mwaka huu2025.

Ni muhimu sana,
waTanzania wote na dunia nzima kufahamu wazi kwamba, umoja, amani na utulivu wa waTanzania utalindwa kwa nguvu zote na kwa gharama yoyote ile.

Fyoko fyoko za kuvuruga amani ya waTanzania, hazitavumiliwa hata sekunde moja, iwe ni mitandaoni au mitaani.
Epuka kujiambatanisha na magenge ya kihalifu, matapeli na vibaka wa kisiasa nchini. :NoGodNo:

Mungu Ibariki Tanzania
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumzia harakati za 'No Reform No Election' amedai kuwa "Ilituweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa kura"

"Watu wetu wa leo ni welevu kuliko miaka 10 iliyopita, mwaka jana mliweka wagombea wa nafasi zote zinazogombaniwa hapa Kibamba na sehemu kubwa walienguliwa, mkatumia nguvu kubwa kuwarudisha, wakarudishwa baadhi alafu siku ya tarehe 27 mkashughulikiwa vizuri zaidi, matokeo yakatangazwa kwa mitutu ya bunduki ndio maana hamna Mwenyekiti wa mtaa hata mmoja, sio kwasababu mmekuwa wajinga kuliko mlivyokuwa miaka 10 iliyopita ni kwasababu sasa hivi ilitushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao"

Lissu ameendelea kwa kusema: "Katika mazingira ya uchaguzi wa sasa ili tushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao, ili wasiweze kutumia bunduki zao kuingia vituoni kwa nguvu na kuchukua masanduku ya kura kwa nguvu,"

Lissu amehoji: "kama na sisi tukiwa na bunduki hiyo nchi itakuwaje?, patakua na pakukaa hapo?, ndivyo wanavyotaka?

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kwani CCM inazo bunduki? Usikurupuke siasa hauwezi kuitafsiri hivyo ukaielewa.
 
Hata hivyo,
movement hiyo haramu ya kuhubiri na kuchochea chuki na migawanyiko miongoni mwa waTanzania, itasaidia sana na kuvipa fursa na nafasi muhimu, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na mamlaka ya mawasiliano nchini kujipanga vizuri zaidi, ili kukabiliana ipasavyo kwa mujibu wa sheria na vibaka hao na matapeli wa kisiasa wanaopanga uovu huo kwa mwamvuli wa kufanya siasa, lakini wanalenga kuvuruga umoja, amani na utulivu wa waTanzania, wanaofanya kazi na shughuli zao mbalimbali za kijamii, kisiasa na kiuchumi nchini, hususani kuelekea uchaguzi mkuu wa kihistoria mapema october mwaka huu2025.

Ni muhimu sana,
waTanzania wote na dunia nzima kufahamu wazi kwamba, umoja, amani na utulivu wa waTanzania utalindwa kwa nguvu zote na kwa gharama yoyote ile.

Fyoko fyoko za kuvuruga amani ya waTanzania, hazitavumiliwa hata sekunde moja, iwe ni mitandaoni au mitaani.
Epuka kujiambatanisha na magenge ya kihalifu, matapeli na vibaka wa kisiasa nchini. :NoGodNo:

Mungu Ibariki Tanzania
Mnavyobubujikwa na machozi!
 
Back
Top Bottom