Pre GE2025 Tundu Lissu: Ili tuweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa Kura!

Pre GE2025 Tundu Lissu: Ili tuweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa Kura!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumzia harakati za 'No Reforms No Election amedai kuwa "Ilituweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa kura"

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
View attachment 3244560
CCM wakae vizuri sasa
 
Hoja nzur,

Tatizo unazuia vipi uchaguzi?

Watu wana ndoto zao..., suo kujiunga na chama tu ili kupiga makofi..

Lakini zaidi , Huo ukata wa fedha anaouona hapo chama kisipo shiriki uchaguzi kitageuka chama fukara na watahongwa mwanzo mwisho na ndio end of the good days ya CDM .
 
Ukweli mchungu ni kwamba waliopo madarakani wanaona kuwa wao Wana haki ya kufanya Kila ukandamizaji na ukiukwaji wa haki so kauli ya Lisu cjaipenda ila watawala wajiangalie
Ata usipoipenda kauli ya lisu haisaidii kitu ndio imeshaenda viral na ujumbe umefika ulipohitajika kufika, hamna muda wa kulambana miguu
 
Ukweli mchungu ni kwamba waliopo madarakani wanaona kuwa wao Wana haki ya kufanya Kila ukandamizaji na ukiukwaji wa haki so kauli ya Lisu cjaipenda ila watawala wajiangalie
Hujamwelewa Lissu!

Lissu anasema kwa hali iliyopo ambayo Polisi wanaingiza masanduku ya kura kwa mtutu wa Bunduki ili kuharibu Uchaguzi, Wapinzani wakitaka kushinda uchaguzi inawabidi nao kushika bunduki kupambana ns polisi wanaotumika.

Amesisitiza hatupaswi kufika huko akimaanisha tufanye Reforms za Katiba na Sheria za Uchaguzi kuepusha kuwafanya watu kufikiri kushika Bunduki ili washinde uchaguzi.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumzia harakati za 'No Reform No Election' amedai kuwa "Ilituweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa kura"

"Watu wetu wa leo ni welevu kuliko miaka 10 iliyopita, mwaka jana muliweka wagombea wa nafasi zote zinazogombaniwa hapa Kibamba na sehemu kubwa walienguliwa, mkatumia nguvu kubwa kuwarudisha, wakarudishwa baadhi alafu siku ya tarehe 27 mkashughulikiwa vizuri zaidi, matokeo yakatangazwa kwa mitutu ya bunduki ndio maana hamna Mwenyekiti wa mtaa hata mmoja, sio kwasababu mmekuwa wajinga kuliko mlivyokuwa miaka 10 iliyopita ni kwasababu sasa hivi ilitushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao"

Lissu ameendelea kwa kusema: "Katika mazingira ya uchaguzi wa sasa ili tushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao, ili wasiweze kutumia bunduki zao kuingia vituoni kwa nguvu na kuchukua masanduku ya kura kwa nguvu,"

"kama na sisi tukiwa na bunduki hiyo nchi itakuwaje?, patakua na pakukaa hapo, ndivyo wanavyotaka?

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa:
Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tapeli la kisiasa
 
Back
Top Bottom