Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
CCM wakae vizuri sasaMwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumzia harakati za 'No Reforms No Election amedai kuwa "Ilituweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa kura"
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
View attachment 3244560
Hakika!Na hiyo ndo hoja ya Lissu kuwa hatupaswi kwenda huko. Tufanye Reforms ili kuepusha watu kuwaza kushika bunduki ili washinde uchaguzi
Umesikiliza clip au umesoma tu na ku comment?Eeeh , juzi alisema yuko tayari kufa leo zinahitajika Bunduki, karudia mbali mbili kuonesha hajateleza. Sawa Mzee
Ata usipoipenda kauli ya lisu haisaidii kitu ndio imeshaenda viral na ujumbe umefika ulipohitajika kufika, hamna muda wa kulambana miguuUkweli mchungu ni kwamba waliopo madarakani wanaona kuwa wao Wana haki ya kufanya Kila ukandamizaji na ukiukwaji wa haki so kauli ya Lisu cjaipenda ila watawala wajiangalie
Hujamwelewa Lissu!Ukweli mchungu ni kwamba waliopo madarakani wanaona kuwa wao Wana haki ya kufanya Kila ukandamizaji na ukiukwaji wa haki so kauli ya Lisu cjaipenda ila watawala wajiangalie
Si kirahisi, hoja zake si za kitotoAlichokisema ni sahihi kabisa,sasa Lissu unaelekea pazuri,tatzo watakuweka ndani,tunakuhurumia jela sio kuzuri
Tapeli la kisiasaMwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu akizungumzia harakati za 'No Reform No Election' amedai kuwa "Ilituweze kushinda uchaguzi lazima tuwe na bunduki kama wao. Ikulu ndio inaamua wizi wa kura"
"Watu wetu wa leo ni welevu kuliko miaka 10 iliyopita, mwaka jana muliweka wagombea wa nafasi zote zinazogombaniwa hapa Kibamba na sehemu kubwa walienguliwa, mkatumia nguvu kubwa kuwarudisha, wakarudishwa baadhi alafu siku ya tarehe 27 mkashughulikiwa vizuri zaidi, matokeo yakatangazwa kwa mitutu ya bunduki ndio maana hamna Mwenyekiti wa mtaa hata mmoja, sio kwasababu mmekuwa wajinga kuliko mlivyokuwa miaka 10 iliyopita ni kwasababu sasa hivi ilitushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao"
Lissu ameendelea kwa kusema: "Katika mazingira ya uchaguzi wa sasa ili tushinde uchaguzi inabidi tuwe na bunduki kama wao, ili wasiweze kutumia bunduki zao kuingia vituoni kwa nguvu na kuchukua masanduku ya kura kwa nguvu,"
"kama na sisi tukiwa na bunduki hiyo nchi itakuwaje?, patakua na pakukaa hapo, ndivyo wanavyotaka?
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Lakini amezungumza ukweli mtupu, kuna upuuzi mwingi kwenye chaguzi zetu.Hii kauli itakuwa ni mwanzo na chanzo kikuu Cha machafuko hapa nchini
Vipi lakini kuhusu hoja zake mwanana?Mwache aongee lakini mshindi come 2025 election ni CCM