Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,467
- 1,697
Anaweza akawa lakini inavyo onekana yeye na Magufuli hawana tofauti kubwa sana kitabia. Wote ni arrogant na ni watu wabishi sana. Tofauti zao ziko katika uzalendo. Magufuli ni mzalendo wa damu. Yuko tayari ku sucrfyce maisha yake kwa uzalendo wake lakini Lissu sio mzalendo kabisa na yeye yuko tayari kupoteza maisha yake maadam ashinde. Kushinda binafsi ni kitu kikubwa sana. Kitendo cha kushindwa hakimpendezi Lissu. Ni mtu ambaye anataka madaraka kwa nguvu. Yuko tayari wananchi wake wapate shida maadam anapata anacho kitaka ambacho ni ushindi wake binafsi wa madaraka.
- Lissu atafaa kwa 2025 na sio 2020
Lissu ni mtu dhaifu sana. Ni mtu ambaye hajiamini mwenyewe ukilinganisha na Magufuli mbele ya wazungu. Wazungu watakacho sema yuko tayari kukubaliana nacho maadam yeye binafsi anafaidika.
Kingine ambacho Magufuli anacho ni kupenda maendeleo. Magufuli anapenda sana Maendeleo ya nchi yake. Yuko tayari asiwe na hela mfukoni, lakini hela zake zinatumika ipasavyo katika kuleta maendeleo ya nchi yake.
Katika starehe wote wako karibu sawa. Sio watu ambao wanapenda sana party kama baadhi ya viongozi wengine kama Kikwete alivyo kuwa. Kwa hali hiyo sio watumiaji ovyo wa hela kwa faida zao.
Wote ni wachapa kazi wazuri japo kuwa hapa Magufuli amemzidi Lissu kidogo hasa tukizingatia point moja, Magufuli anapenda sana kila kitu kifanyike acuratly.
Katika ukabila Lissu ni liberal. Hana ukabila at all. Kila mtu kwake yuko sawa. Naweza sema Lisu ni mzaramo kuliko hata mzaramo mwenyewe. Ni mbongo wa Dar haswa. Magufuli kwa upande mwingine ana ukabila kidogo. Bado watu wa Kanda ya ziwa wana advantage kidogo kwake kuliko watu wa kusini mwa Tanzania. Sielewi kwa nini plan ya reli ya standard gauge na treni ya umeme isijengwe pia kusini mwa Tanzania?
Kwa hali hiyo kushinda urais itakuwa vigumu kwa Lissu. Inabidi awe mzalendo wa kweli kama Magufuli itamsaidia sana. Vinginevyo itakuwa vigumu. Magufuli katika uzalendo ameweka stage kubwa sana kwa watanzania kiasi kwamba wagombea urais wa baadaye watakuwa na shida sana.
Ni mtazamo wangu tu.