Uchaguzi 2020 Tundu Lissu is not Presidential Material

  1. Lissu atafaa kwa 2025 na sio 2020
Anaweza akawa lakini inavyo onekana yeye na Magufuli hawana tofauti kubwa sana kitabia. Wote ni arrogant na ni watu wabishi sana. Tofauti zao ziko katika uzalendo. Magufuli ni mzalendo wa damu. Yuko tayari ku sucrfyce maisha yake kwa uzalendo wake lakini Lissu sio mzalendo kabisa na yeye yuko tayari kupoteza maisha yake maadam ashinde. Kushinda binafsi ni kitu kikubwa sana. Kitendo cha kushindwa hakimpendezi Lissu. Ni mtu ambaye anataka madaraka kwa nguvu. Yuko tayari wananchi wake wapate shida maadam anapata anacho kitaka ambacho ni ushindi wake binafsi wa madaraka.

Lissu ni mtu dhaifu sana. Ni mtu ambaye hajiamini mwenyewe ukilinganisha na Magufuli mbele ya wazungu. Wazungu watakacho sema yuko tayari kukubaliana nacho maadam yeye binafsi anafaidika.

Kingine ambacho Magufuli anacho ni kupenda maendeleo. Magufuli anapenda sana Maendeleo ya nchi yake. Yuko tayari asiwe na hela mfukoni, lakini hela zake zinatumika ipasavyo katika kuleta maendeleo ya nchi yake.

Katika starehe wote wako karibu sawa. Sio watu ambao wanapenda sana party kama baadhi ya viongozi wengine kama Kikwete alivyo kuwa. Kwa hali hiyo sio watumiaji ovyo wa hela kwa faida zao.

Wote ni wachapa kazi wazuri japo kuwa hapa Magufuli amemzidi Lissu kidogo hasa tukizingatia point moja, Magufuli anapenda sana kila kitu kifanyike acuratly.

Katika ukabila Lissu ni liberal. Hana ukabila at all. Kila mtu kwake yuko sawa. Naweza sema Lisu ni mzaramo kuliko hata mzaramo mwenyewe. Ni mbongo wa Dar haswa. Magufuli kwa upande mwingine ana ukabila kidogo. Bado watu wa Kanda ya ziwa wana advantage kidogo kwake kuliko watu wa kusini mwa Tanzania. Sielewi kwa nini plan ya reli ya standard gauge na treni ya umeme isijengwe pia kusini mwa Tanzania?

Kwa hali hiyo kushinda urais itakuwa vigumu kwa Lissu. Inabidi awe mzalendo wa kweli kama Magufuli itamsaidia sana. Vinginevyo itakuwa vigumu. Magufuli katika uzalendo ameweka stage kubwa sana kwa watanzania kiasi kwamba wagombea urais wa baadaye watakuwa na shida sana.

Ni mtazamo wangu tu.
 
Magufuli is still the great, the champion, we need him for more 60years..
 
Iq ya nyani kweli, subiri 2020
 
Wow....your English is hard! Teh teh teh

The question remain, is the current president of URT a "presidential material"? What does a "presidential material" look like? And who is a "presidential material"?
 
Akiwa ubelgiji hats omba omba hatakutana naye. Anaumwa no mgonjwa.
 
Chako uliandikaje ili tujue? Sisi tutafuata chako chao tutawaachia wenyewe. Kwahiyo huyu mnyapala wa Barabara ndio malighafi ya urais?
 
kuhusu 2020 LISSU kugombea uraisi au huenda apite au asipite bado JPM atakuwa rais.
Kama kuna free and fair elections, Magufuli has no chance. Ila kwa kuwa tupo under police ‘skunk’ state, tukitawaliwa na chama dola, basi upo sahihi!
 
Labda kama sielewi maana ya "presidential material" kwa maneno ya kiswahili maneno haya ya kiingereza yanaimanisha mtu "afaae kuwa rais" kama tafsiri hii ambayo sio rasmi inaakisi ukweli basi sio sahihi kusema Mhe. Tundu Lissu hafai kuwa rais wa nchi (kwa maana hata sasa yeye ni "Rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika"). Kuwa rais hakuna maana ya kuwa rais bora na ubora wa rais unatokana na matendo yake kukidhi matarajio ya wananchi. Hata baba wa Taifa ubora wake bado unazua mabishano makali na majadala mrefu. Ubora unatokana na ulinganisho kati ya rais wa awamu moja na nyingine.
Kwa maoni yangu, kama Dr. John Joseph Pombe Magufuli ameweza kuwa rais na inaonekana yapo maeneo ambayo anayafanya vizuri;anaye sema Mhe. Tundu Lissu hafai kuwa rais naamini hawezi kuwa sahihi. Endapo akijitokeza kugombea urais, akadhaminiwa na chama cha siasa, akapigiwa kura na wapinga kura, akatangazwa na Tume ya Uchaguzi, akaapishwa kwa mujibu wa sheria ni nini kitamzuia kuwa rais?
 

[emoji1532][emoji1532][emoji1532][emoji1532][emoji1532][emoji1532]
 
There is no genuine reason behind your argument, if I were you, I would have kept quiet because silence is golden, una kipimometer gani ulichokitumia kujua hana sifa.
 

ha ha ha, kazi ipo!!
 

...nakubaliana na wewe. Maana tunaona Magufuli alivyo ki-barabara na mechanical, na hasara yake kwa taifa. Na siyo kisayansi kama baadhi ya fanatics wake wanavyomtetea!!

Na wazo la Lissu kupewa wizara ya kilimo ni zuri sana! Kwa kweli sekta ya kilimo, serikali (post-Nyerere) zote hazijawahi kukipa kipaumbele kinachostahili. Lissu akipata exposure na uelewa wa matatizo ya kilimo na masuluhisho yake, basi atakuwa candidate mzuri sana.
 
Nakubaliana na Nyani Ngabu, JokaKuu na Pascal Mayalla.

Tusijadili ‘presidential material’ kwa kuwaangalia akina Magufuli, Kikwete, na Mwinyi. Hawa si benchmark, maana hawafai hata kidogo.

Ila naamini Lissu hayupo mbali sana na kuwa presidential material. Nchi nyingi duniani (mf. Marekani) marais uwa wanasheria. Naamini kwamba Rais kama CEO wa taifa ni muhimu sana awe acquainted na sheria kwanza. Kisa masuala ya kodi na fedha, na sekta nyingine ambayo ni muhimu zaidi kwenye taifa. Kwa Tanzania, sekta hiyo ni kilimo. Ndiyo maana nimekubaliana na wazo la JokaKuu juu ya Lissu kupewa wizara kivuli ya kilimo.
 

Marekani marais wote si wana sheria. Actually breakdown ya wanasheria na walio sio wanasheria ni almost half and half.
 
Marekani marais wote si wana sheria. Actually breakdown ya wanasheria na walio sio wanasheria ni almost half and half.
Marais 25 kati ya 45 walikuwa na taaluma ya sheria. Hii ni kama 56% ya marais wote buda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…