Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

Kwa hiyo Jpm alikuwa anajenga SGR kwa fedha za ndani kama alivyokuwa ananena majukwaani? Alivyomnunua mgembea ubunge wa upinzani kule chato ili apite bila kupigwa ndo huo ukweli unaoongelea? Matokeo yale akaishia kudhurumiwa pesa zake akawa anashinda Kebi's Hotel huku akiwa hajui hatima yake
 
Wanabodi
Msingi Mkuu wa kazi ya uandishi wa habari ni ukweli, kuwa mkweli kuusema ukweli na kuandika ukweli...
Katiba huwa kwenye vitabu ambavyo hutawanywa watu wavisome, sasa ni wazi ukinyofoa ukurasa kitabu kitalegea na unawezaje kunyofoa kurasa kwenye kitabu kilichopelekwa Magu au Mafia?

Labda utumie nguvu za giza kuzifuta(kuyeyusha) kama ulivyosema, nieleweshe mimi mzito kuelewa.
 
Wakati mnamsifia mZiLaNkeNdE kuwa alikuwa mkweli semini pia alikuwa mtu muovu kupindukia Katika utawala wake tulishuhudia umwagaji damu usio wa kawaida, dhuluma, upotevu haki, kusiginwa kwa katiba na mengineyo.

Na nyinyi acheni unafiki semeni ukweli Kwani ukweli utawaweka huru.
 
Kilichonyofolewa ni kipengele kimoja tuu sio ukurasa mzima, kilinyofolewa kifungu kimoja tuu!. Nimesema kimenyofolewa kwasababu hakikujadiliwa rasmi, na kikayeyuka bila kuwemo kwenye randama kiliondokaje, yaani just vanished into thin air!.
P
 
Acha zarau mzee lissu siyo bwana mdgo wako mtu Ana miaka56 halfu unamuita kwa kejeli eti bwna mdgo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
NotaBene

1.Pasco alistaafu ya uandishi wa Habari.

2.Pasco ni kada wa chama Cha mapinduzi aka mambuzi.

Kwa namba yeyote Ile andiko la Pasco Kaa Sasa litakuwa na chembechembe za propaganda sababu ule uandishi habari halisi alisema kastaafu.

Kuwa makini sana na soma between lines utagundua kapenyeza propaganda.

Andika hili sidhani kama Lina lengo kusifia ukweli wa TAL ila nahisi Lina lengo la kumfarakanisha Lissu na wanachama wenzake.

Kuweni makini nae.
 
Nafasi mbalimbali za uongozi NDANI ya chama

Urais sio uongozi wa ndani ya chama
Ubunge sio uongozi wa ndani ya chama
Udiwani alkazalika
 
Tundu Lisu yupo na kaja/kaletwa ili kuilinda na kutetea Serikali iliyopo, kinachotokea sasa hivi siyo bahati mbaya kimepangwa, ona hakuna anayejadili mambo yanayowasumbua wananchi kwa sasa kama mfumuko wa bei, kushuka kwa elimu wanafunzi wamefeli na haijulikani wataenda wapi, Deni la nchi linazidi kuongezeka wamekopa walichofanyia fedha haijulikani wala hakuonekani kitu lkn Tundu Lisu yuko kuongelea maisha ya Walemavu Ubelgiji.

Mtu yoyote ambaye haongelei mfumuko wa bei na madeni makubwa ya nchi huyo yuko upande wa Serikali makes no mistake about that, Tundu Lisu, Mwigulu, Adolf, Bashe wote wana bosi na paymaster mmoja, yuko hapa kuwazugeni na kuwatoa relini msijadili mambo muhimu.

Angalia Kenya kinachoendelea Raila na Ruto huo ndiyo Upinzani unaotaka kuondoa Serikali iliyopo siyo hawa, Tundu Lisu yupo kwenye payroll to protect those in power, Tundu Lisu kaletwa kuwatoa relini msijadili mambo ya maana, Amkeni!
 
Dah! Pasco katunza hii na kusubiri right time apige! Sasa JF ya zamani tungepata mjadala wa kina uliokuwa unaimarisha hata upinzani wenyewe. Siku hizi tuna machawa kaka akina Mwijaku! Watakuja na comments za kejeli badala ya kuhoji kwa hoja.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Acha zarau mzee lissu siyo bwana mdgo wako mtu Ana miaka56 halfu unamuita kwa kejeli eti bwna mdgo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Unaujua umri wangu?. Mimi niko A-level dogo yuko O-level!.
Yeye alizaliwa kijijini na kusomea kijijini hivyo wanaanza shule na miaka 7!. Mimi nimeanza nursery St. Peter's Kindergarten Tanga, at 4 years!, nimeanza la kwanza at 5 years Nyakahoja Mwanza, Mzee Mayalla akapata matatizo nikahamia Dar

Binti yangu mmoja is 10 years yuko Form 1 Mazinde!. Mwingine 22 years anafanya masters US!. Kwenye udogo na ukubwa mtu ukimtangulia vidato regardless ana umri gani anakuwa ni dogo tuu!.

Mimi mwenyewe naenda 60!, nimepata admission ya kuwa advocate last year, according to my Roll number, kuna madogo ya 30 years walikuwa admitted kabla yangu, wananiita junior counsel wakati mimi ni babu!.
P
 

Halafu walikuwa wanamuita JPM mshamba kumbe hakuna mtu mshamba kama.

Tundu Lissu kazaliwa kijijini kakulia huko katoka sababu ya Shule vinginevyo angekuwa huko, kaishi na anaishi Ulaya lkn ni mshamba kupita washamba jamaa ni villager sana, ukisikia akiongea kuhusu Belgium ndio utajua kwamba ni villager nilikuwa najiuliza how come yuko soo petty?
 
How comes 10 years kuwa form 1!? huyu alipaswa awe darasa la 4 hata kama ingekuwa kuwaishwa sana basi angekuwa Drs la 6

Je alisoma nje ya nchi.

Ufahamu wake uko?. Unaendana na masomo anayosoma.!?
 
Kuwa mshamba sio lazima uzaliwe kijijini.

Jk yule pale kazaliwa msoga kasoma huko bagamoyo ya enzi hizo. Bado bush sana.

Msoga tu hadi Leo Kuna nyumba za udongo isingekuwa Ile barabara ya lami iliyokatiza pale kijijini pangekuwa sitimbi kweli kweli.

Lakini JK anaitwa born town, mtoto Wa mjini wakati kazaliwa bush msoga huko.

Mambo yake Yako kimjini mjini. Ame adapti maisha ya mjini anawaza kimjini mjini na anatenda, kimjini mjini.

Hii ni tofauti na yule jamaa yenu mshamba yule anaeongea kilugha hadi kwenye majukwaa ya kitaifa kama sio kutuletea ukabila ni Nini!?

Ushawahi msikia JK akizungumza kikwere mahali popote!?. Sidhani sababu yule mtoto Wa mjini hana pigo za kiporipori.
 
Kuwa mshamba sio lazima uzaliwe kijijini.

Jk yule pale kazaliwa msoga kasoma huko bagamoyo ya enzi hizo. Bado bush sana.

Msoga tu hadi Leo Kuna nyumba za udongo isingekuwa Ile barabara ya lami iliyokatiza pale kijijini pangekuwa sitimbi kweli kweli.

Lakini JK anaitwa born town, mtoto Wa mjini wakati kazaliwa bush msoga huko.

Mambo yake Yako kimjini mjini. Ame adapti maisha ya mjini anawaza kimjini mjini na anatenda, kimjini mjini.

Hii ni tofauti na yule jamaa yenu mshamba yule anaeongea kilugha hadi kwenye majukwaa ya kitaifa kama sio kutuletea ukabila ni Nini!?

Ushawahi msikia JK akizungumza kikwere mahali popote!?. Sidhani sababu yule mtoto Wa mjini hapa pigo za kiporipori.
 
How comes 10 years kuwa form 1!? huyu alipaswa awe darasa la 4 hata kama ingekuwa kuwaishwa sana basi angekuwa Drs la 6

Je alisoma nje ya nchi.

Ufahamu wake uko?. Unaendana na masomo anayosoma.!?
Wife ni US Subject, watoto wangu wakubwa wawili wamezaliwa Bongo tukahamia US wakasoma kule mpaka vyuo, hawataki kuisikia Tanzania!. Tukaamua basic na elementary watasoma kule, Sekondari wanakuja huku tuwa Tanzanianate Shule za seminary, halafu university wanarudi kule.
P
 
Ungekuwa muandishi wa habari makini ungeandika juu ya foreign reserve kujenga madarasa kimya kimya ilihali tuliambiwa pesa za Uviko zinatosha.
 
Lissu hafanani na Magu kwa lolote. Na ukweli huu unathibitishwa na kiu ya Magu kuona kuwa Lissu anauawa.
Yaani hapa ni mmoja kuwa msiri na usiri huu ni wa upande wa kuficha uovu unaopelekea chuki ya kuuzika ukweli kwa kifo cha mauti.
Hili linadhihirisha watu hawa wawili wakiwa spark, yaani mmoja mwongo sana na mwingine mkweli sana.
Mmoja muovu sana na wa pili mnyoofu sana katika haki na adili.
Ujasiri wa mmoja unajengwa juu ya unyoofu wa moyo na uadilifu katika kutimiza wajibu wa haki na kwa wa pili ujasiri wake unajengwa juu ya kiburi cha uzima na kujitakia utukufu asiostahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…