Umeandika pumba tupu kwa sababu ya ushabiki maandazi. Tundu Lissu sio kibaraka, and honestly, Vibaraka halisi wanajulikana na wapo CCM. Ni wale wanaosaini mikataba ya hovyo kama wa DP World uliotoa hatamu za bandari zetu kwa miaka 30, au mikataba ya madini ambapo nchi inaambulia mrahaba (royalty) wa 6% tu huku asilimia 94 ikiondoka nje!
Tangu miaka ya nyuma, Lissu amepigania rasilimali zetu hadi kupigwa risasi, wakati nyie mkiuza nchi huku deni la taifa likishika kasi kuelekea trilioni 100 kwa mikopo ya World Bank na IMF, nchi mmeiacha ikiendeshwa kwa rimoti ya IMF na World Bank, That is the ultimate definition of a puppet!.
Kuhusu nywele, huko ni kukariri mifumo ya kikoloni na ki-pharao (Wanyoa vipara kama zungu). Carefree hairstyle ni alama ya uhuru wa Mwafrika na kukataa kufungwa vizimba vya kifikra. Hata billionaire Jay-Z kwenye ngoma yake na Meek Mill (What's Free) alishatupa somo: 'No dreadlocks, check the fed docks.... you're all boxed in. 'Don't control someone's identity!
Kendrick Lamar kwenye 'Alright' anakuambia "We hate po po, wanna kill us dead in the street for sure... but baby, we gonna be alright. Lissu alipigwa risasi 16 akasimama, huku hao unaowashabikia wakiziona tu hizo dreadlocks wanatetemeka!
Mwisho, stress haiwezi kufichika, inaonekana kwenye mwili. Lissu anazidi kung'aa kila siku kwa sababu he has clarity of mind, a clean conscience, and the truth on his side. Ukweli unamweka huru! Wanaopata tabu hadi 'mavi kujaa kwenye chupi' kwa hofu ya kupoteza madaraka na uoga wa wananchi ni hao viongozi wako wa mfumo dhalimu. Get your facts straight and read big books before opening your mouth! 🤫🔥