Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Katika miaka hii mitano kila Mtanzania awe ni tajiri au maskini ana hadithi yake ya maumivu

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Katika miaka hii mitano kila Mtanzania awe ni tajiri au maskini ana hadithi yake ya maumivu

Wengine wazee wetu miaka 5 sasa hawajapata pension zao.. ni hadithi tu kila siku. Matibabu yao kasheshe nyingine tena. Kwa walio na Bima ya afya, kuna limitations kibao za matibabu na vipimo.. dawa kibao nazo zimetolewa huko kwenye Bima. Nyumba zetu zimebomolewa.. Watanzania tunanuka shida tu kwa miaka hii yote ya Jiwe. Kwa kweli hatuwezi kumsahau. Mtu tulimshabikia 2015, tukijua tumepata kumbe tumepatikana.

Kura zetu zote sisi wanyonge safari hii ni kwa Lissu. Huyu ndiye atatusikiliza na kutufaa.
 
Wanaccm tu ndo wameinjoi hii miaka ya dikteta magufuli
 
CHADEMA ACHENI UNAFIKI. MNAZUNGUMZIA KUTEKWA BEN SAA NANE WAKATI MNAJUA WALIOMTEKA. KAMA MNATETEA HAKI MBONA HAMSEMI CHOCHOTE JUU YA WAFUASI WA CCM, VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA NA POLISI WALIOUAWA MKURANGA??? MNAZUNGUMZIA KILA SIKU BEN SAA NANE TU KWA KUPOTEA, JE, HAO WALIOUAWA SIO BINADAMU?? MNAJIFANYA HAMHUSIKI NA MATUKIO HAYO WAKATU TUNAJUA WALIOTEKA BEN SAA NA KUMPOTEZA NI NYIE.
RISASI ALIZOPIGWA LISSU MLIZIPANGA NYIE NDO MAANA MMEMPOTEZA KABISA DEREVA WA LISSU,
KOROSHO WAKULIMA WALIKWISHA LIPWA KWA BEI NZURI KULIKO BEI WALIOTAKA KUPEWA NA WAFANYA BIASHARA.
VYOMBO VYA HABARI VISIVYOFUATA WEREDI LAZIMA SHERIA ITUMIKE KUVIFUNGIA. SHERIA ZINATUNGWA ILI ZITUMIKE.
Kuna sehemu nimetaja CHADEMA hapo juu ?

Kama waliomteka Ben Saanane wanafahamika kwanini hawakamatwi ?

Hayo mauaji ya MKIRU mbona hakuna aliyekamatwa hata mmoja na utawala uko kimya ?
 
Unatishia kuondoa tone moja la maji baharini,ukidhani kwamba bahati itakauka?😂,mkuu sio wewe tu, yaani hata ukoo wenu wote ukipiga Kura kwa Lissu, bado Magufuli atabaki kuwa Rais wenu.
Labda Kwa bao la mkono, ila kwenye sanduku babu yenu hawezi mshinda Lissu!
 
Sisi Watanzania wazalendo tunafurahi uongozi wa Rais Magufuli

Wanaotumika na Mabeberu wamezibiwa mirija ndio hao wanalia
Wewe na nani
Acha kutuchanganya na sisi hatusapport upuuzi wala wizi🚮🚮🚮🚮
 
Wapwa
Akiwa hapa Ifakara kwenye kampeni zake, Lissu anaendelea kutema cheche

Anasema kila Mtanzania ana hadithi yake ya maumivu. Ameomba kura kutoka vyama vyote na kuahidi mambo mengi ikiwemo kufuta machozi mengi ya wana Ifakara na Tanzania nzima.

Je wewe hadithi yako ni ipi.?

Haki huinua Taifa.
Yapo maumivu kwenye kuzaa kitu chochote cha thamani,ila Utukufu, ubora wa kizaliwacho huwa na thamani kuliko maumivu yenyewe. Kwa nchi yoyote iliyoamua kujitegemea kiuchumi, tena kwa kubana matumizi, kuziba mianya ya rushwa, lazima kuwe na maumivu. Sasa tundu Lissu asidanganye watu hapa, hatuna shangazi, wala mjomba wa kutusaidia. Maendeleo ya kweli tutayaleta sisi wenyewe, na sio hao mabeberu anaowategemea.
 
Mbona deni limeongezeka mara mbili
 
Twende na Hashimu Rungwe ...ameahidi kupeleka bahari dodoma na pia wali kupita kwenye mabomba. Bila kula hatutaweza kufanya kazi, ivyo Rungwe kwanza.
#inRungweWeTrust.
#RungweRaisiAjaye.
#NIYEYE
 
Back
Top Bottom