Tetesi: Tundu Lissu kujiunga ACT Wazalendo, Abdul Nondo naye kuula!

Tetesi: Tundu Lissu kujiunga ACT Wazalendo, Abdul Nondo naye kuula!

Status
Not open for further replies.

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Ndugu zangu,

Bado ni tetesi lakini hapa JF ni muhimu huu mjadala ukawepo kwa afya ya siasa za nchi.Zitto Kabwe ndiye mwanasiasa pekee aliyemtembelea Tundu Lissu mara tano hospitalini,mara tatu Ubelgiji mara mbili Nairobi.Inasemekana ziara za Ubelgiji zaidi zilijawa na mazungumzo kuhusu hatma ya Lissu kisiasa kwa mazungumzo ya wiki mbili zilizopita kuna uwezekano mkubwa Tundu Lissu akajiunga na ACT Wazalendo ili kuendelea na shughuli za siasa.

Bado haijaeleweka kwanini Lissu anafikiri kuondoka Chadema hizi ndio siasa na mauzauza yake,huenda kuna alama za nyakati zimesomwa.

Zaidi ya hilo kijana Abdul Nondo ambaye miezi michache alitumika na Mbowe ili kufifisha nguvu za Zitto Kigoma sasa rasmi ACT Wazalendo ambapo wakati wowote atapewa majukumu ndani ya chama hicho baada ya kumaliza masomo yake UDSM.

Habari nyingi huanza kama tetesi hapa JF mwishowe hubainika kuwa ni za kweli.
 
Acacia wamesimamia na kufadhili vikao vya Kuwaunganisha Zitto na Lissu

Lissu, Zitto, Jussa, Seif Sharif, Nyalandu ni Muungano hatare kwa Maslah ya Taifa na Chama uangaliwe kwa macho makini

Dola isimame na Chadema dhidi ya ACT

ACT ni kirusi cha Mabeberu kinachonenepeshwa kwa kasi ya ajabu
 
Ndugu zangu,

Habari nyingi huanza kama tetesi hapa JF mwishowe hubainika kuwa ni za kweli.
Mkuu Kaka Wakudadavua, kwanza naunga mkono hoja, ila duh...!. Kiukweli hii kali!.

Hata hivyo asante Kaka Wakudadavua, kutudadavulia hii, umetupakulia ikiwa ya moto moto, kwa jinsi unavyopata taarifa za ndani za vyama, nakuvulia kofia, Musiba atasubiri!, hongera unafanya kazi nzuri Kaka Wakudadavua. Asante tena. Na kiukweli nakukubali sana...basi tuu, kwa vile wewe ni Kaka, ungekuwa Dada, uvumilivu ungenishinda!.

P
 
Hujui siasa wala huwajui wanasiasa. Kwani maalim seif ambaye aliungana na chadema na akaungwa mkono urais kupitia ukawa mbona alihamia ACT kabla ya chadema? Kwani chadema walimfanya nini?
Hawa vijana uwezo wao kuchanganua hoja no mdogo mno
 
Kwani dirisha lausajili limeshafunguliwa? Kuanzia sasa mpaka mwakani kipindi chauchaguzi sidhani kama kuna kiongozi anawaza maendeleo yawananchi Zaid yakuwaza uchaguzi
 
Inawezekana ni Kweli Kwanini Lisu Kakataa Kurudi Tarehe 7 -09 - 2019 akaongeza gia angani ( kaongeza siku mbele ) ni baada wiki moja mbele tukamsikia zitto kwamba alienda juzi juzi kumtemberea hospitalin atujui walitete nini pia akasema yeye na lisu sio maadui namwisho amemsifia sana na kumponda slaa na wengineo kawaweka kapuni ambao nikama ndio waliwachonganisha kipind yupo chadema sasa leo baada ya siku moja na masaa kaza katokea mtu na habari hii hapo juu anasema tetesi inawezekana ni kweli wakuu
 
Ninachokiona mimi ni Zitto kuwa mgombea mwenza wa Lissu come 2020
 
Tatizo linalozidi kukua hapa Tz, ni watu kupenda kubisha kwa sababu tu yeye hajui/hana taarifa. NDUGU, yafaa ujifunze kubisha kwa sababu unajua/una facts. Kwenye mambo ambayo hakuna uhakika ni bora kunyamaza. Itakujakusaidia kauli zako kuheshimika.
Hujui siasa wala huwajui wanasiasa. Kwani maalim seif ambaye aliungana na chadema na akaungwa mkono urais kupitia ukawa mbona alihamia ACT kabla ya chadema? Kwani chadema walimfanya nini?
 
Acacia wamesimamia na kufadhili vikao vya Kuwaunganisha Zitto na Lissu

Lissu, Zitto, Jussa, Seif Sharif, Nyalandu ni Muungano hatare kwa Maslah ya Taifa na Chama uangaliwe kwa macho makini

Dola isimame na Chadema dhidi ya ACT

ACT ni kirusi cha Mabeberu kinachonenepeshwa kwa kasi ya ajabu
Duh, hapo umeuwa mkuu, "dola isimame na Chadema". Cku kijani itaungana na gwanda kuimaliza ACT kutakuwa na kupatwa kwa Lumumba.
 
Acacia wamesimamia na kufadhili vikao vya Kuwaunganisha Zitto na Lissu

Lissu, Zitto, Jussa, Seif Sharif, Nyalandu ni Muungano hatare kwa Maslah ya Taifa na Chama uangaliwe kwa macho makini

Dola isimame na Chadema dhidi ya ACT

ACT ni kirusi cha Mabeberu kinachonenepeshwa kwa kasi ya ajabu
Mkuu mbona ata CCM ni mawakala wa mabeberu wa Kichina au ilo naro mpaka uende chuo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom