Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kukosa pesa ya kampeni

Rebeka 1

Member
Joined
Aug 11, 2020
Posts
34
Reaction score
37
MGOMBEA URAIS CHADEMA AISHIWA FEDHA ZA KAMPENI

Na Humphrey Shao

Ikiwa ni katika hatua ya awali ya mchakato wa Uchaguzi mkuu kwa wagombea Urais wakiwa katika hatua ya kukusanya wadhamini nchi nzima, kwa upande wa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameishiwa fedha za mafuta na Posho za wasaidizi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizotufikia sauti ya Wananchi kutoka chanzo chetu cha uhakika zinaeleza mpaka sasa Chadema hawana fedha za kuendeshea kampeni licha ya kuchukua ruzuku kwa kipindi cha miaka yote mitano.

Chanzo hicho kinasema Lissu ameunda kamati kadhaa za kukusanya fedha kutoka kwa marafiki na wafanyabiashara ili waweze kufanikiwa katika mchakato wa uchaguzi.

"Kama unavyotuona tupo hapa Msimbazi kwa ajili ya kikao na mimi mmoja ya wanakamati wa kuchangisha fedha kwa ajili ya mgombea wetu wa Urais lakini hali ni mbaya kila tunayemgusa hayupo tayari kutusaidia wanasema tuachane na huu ujinga" kimesema chanzo chetu.

Amesema hali ya kiuchumi ya Chadema ni mbaya kwani Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe amegoma kutoa fedha kwa ajili ya shughuli za kampeni za mgombea urais.

“Kwasasa zimeundwa kamati mbalimbali katika kanda tofauti kuhakikisha tunafanikisha hili, hali ya kifedha ndani ya chama si shwari na kila tunayemgusa anataka mahesabu ya Ruzuku na michango ya wabunge.

Licha ya kamati hizi kuwepo maswali ya fedha za Ruzuku na michango ya wajumbe yamekuwa mengi kuliko kawaida maana wanachama wanataka kujua fedha ya chama chao ipo wapi,” kimeeleza chanzo hicho.

Aidha chanzo hicho kimesema jambo hilo linawapa wakati mgumu na kufanya wasifikie lengo na Mwenyekiti Mbowe kajiweka pembeni na hataki aulizwe juu ya fedha hizo.
 
Hali ni mbaya kwa kweli.ni swala la muda tu ila CDM wana hali mbaya ya uchumi.
 
Lissu pesa za kampeni hana, sio siri.

Mbowe asilaumiwe Ruzuku haipo Tena chache zilizobaki Ni kwa ajili ya kulipa wafanyakazi wa Chadema Kama maofisi, madereva, gharama za ofisi nk.

Tulisema humu toka mwanzo kuwa Chadema watajuta mbele ya safari kumteua mgombea Maskini.

Chama kingekuwa kina pesa haina shida. Lakini chama pesa hakina Halafu kinateua mgombea masikini asiye na pesa.

Hawakuwa maamuzi sahihi. Sasa Kama pumzi ya pesa imekata kwenye kutafuta wadhamini tu ikifika kampeni si itakuwa hatari.
 
Okey

Ule utaratibu mpya uliyotolewa na BOT wa ubadilishaji pesa za kigeni ndiyo unaosababisha hilo tatizo la ukosefu wa pesa ndani ya chadema!!
Hakuna binadamu aliyeweza mzidi akili bindamu mwenzake ukiwaza hiki wenzio wanawaza kile, pesa sio ishu na njia sio lazima iwe moja ya kuingiza.
 
njaa na mateso mliyotutendea watz kwa 5 yrs ni hatari ya kuichagua ccm agin 5 yrs ni kampeni tosha
Sema hamjui. Mwaka huu CCM itahsinda. Mwaka 2025 inaleta mtu wa aina mnayotaka.

2015 mlitaka Rais Mkali. Sasa mnataka Rais Mpenda watu. CCM inahazina kubwa. January ataingia kwenye ulingo 2025 na agenda yenu itabadilika kabisa.
 
Sema hamjui.. Mwaka huu CCM itahsinda .. Mwaka 2025 inaleta mtu wa aina mnayotaka.

2015 mlitaka Rais Mkali.. Sasa mnataka Rais Mpenda watu..CCM inahazina kubwa. January ataingia kwenye ulingo 2025 na agenda yenu itabadilika kabisa.
Ukali bila tija ya kuboresha maisha ya watu inasaidia nini, ukali wa dabo standard, wasio na chapa ndo wako ndani uhujumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…