Wee unadhani hao wenye mawazo kama huyo uliyemjibu hapa hawajui ukweli ulivyo ueleza hapa? Wanajuwa sana; na hata Magufuli mwenyewe angekuwepo wakati huu dhamira ingekuwa inamshtaki sana.Unaongea jambo usilolijua kabisa. Lissu hakumpinga Magufuli juu ya makinikia bali alimshauri njia bora ya kudili na hao mabeberu lakini kwa vile Jiwe alikuwa kilaza kwenye maeneo hayo akatafsiri ushauri wa Lissu kuwa ni usaliti na akaamuru Lissu auwawe kwa kupigwa risasi. Lissu hakufa na yale yote aliyoshauri yalikuja kutokea vile vile, makinikia yalikwenda na tumeshitakiwa na kulipishwa mabilioni ya shilingi na kesi nyingine bado zipo mahakamani.
Naamini alikufa akijutia kosa hili alilofanya kwa pupa zake tu.