Tundu Lissu kurejea nchini hivi karibuni. Kipaumbele itakuwa kupambania Katiba mpya na mikutano ya siasa ya hadhara.

Tundu Lissu kurejea nchini hivi karibuni. Kipaumbele itakuwa kupambania Katiba mpya na mikutano ya siasa ya hadhara.

Kwani SSH ameshatoa tamko? Au jamaa ameamua kujirudisha tu bila tamko? Amesubiri tamko akaona imekula kwake!
 
Yeye aje atulie nyumbani aendelee na maisha yake tu! Tanzania ni ile ile na itaendelea kuwa ile ile.
 
Tamko hilo hapo
JamiiForums1829156142.jpg
 
Chadema kaeni mkao wa kula maana sasa mpambano kwa ajili ya katiba mpya na mikutano ya hadhara umeiva.

Lissu sio wa mchezo linapokuja suala la haki za wananchi
πŸ‘‡Lissu asisitiza Katiba mpya, atangaza kurejea nchini Lissu asisitiza Katiba mpya, atangaza kurejea nchini
Tunamkaribisha sana na kumsubiri kwa kinachopaswa kudaiwa ni like tuu ambacho ni haki. Kwa vile Tanzania inayo katiba, kinachotakiwa kufanywa sio kudai katiba mpya bali Ku lobby tufanye mabadiliko ya Katiba na ikiwezekana kupata katiba mpya kwa kutumia lobbying and advocacy.

Kwa vile suala la katiba mpya lilikuwepo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, JPM akasema katiba sii kipaumbele chake, na hatukumshinikiza.

It's very unfortunately hoja ya Katiba mpya sasa haipo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM hii ya sasa ya Mama Samia, hivyo kama JPM hatukumshinikiza, then na Mama, tusimshinikize, tutumie zaidi dialogues, lobbying and advocacy and not confrontation.

Lissu karibu sana Nyumbani, Tanzania ni nchi yetu, east west, home is best.
P.
 
Chadema kaeni mkao wa kula maana sasa mpambano kwa ajili ya katiba mpya na mikutano ya hadhara umeiva.

Lissu sio wa mchezo linapokuja suala la haki za wananchi
[emoji116]Lissu asisitiza Katiba mpya, atangaza kurejea nchini Lissu asisitiza Katiba mpya, atangaza kurejea nchini
Yeye aje maana hapa ndipo nyumbani kwao.

Haya mengine atayakuta kama alivyoyaacha.

Sasa hivi wazungu akili yote iko kwa Putin na jinsi ya kuzihami nchi zao dhidi ya janga la uchumi linaloinyemelea Dunia kwa sasa.

Masuala ya kufananisha yanayotokea kenya na Tanzania wala haimpi Lissu credit ya kisiasa.

Kenya iko kwenye kampeni za uchaguzi mkuu kwa sasa.

Sio siri kwamba Rutto na chama chake cha UDA,amemkalia vibaya mpinzani na kinara wa siasa za kenya Raila Odinga ambaye ndie Chaguo la Rais Kenyatta anaemaliza muda wake kikatiba.

Ni wazi Uhuru ameitumia Nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi kama turufu ya kampeni kwenye coalition yake yeye Raila na Kalonzo Musyoka ya "Umoja" ametumia ile methali maarufu ya Penye Udhia Penyeza Rupia.

Watanzania wanataka mwanasiasa anayepambania haki zao dhidi ya madhalimu wachache wanaounda mitandao ya wizi wa maliasili za nchi hii kwa maslahi yao binafsi.

Ingawa katba ni suala muhimu lakini kiuhalisia sio kipaumbele cha wapiga kura bali ni takwa lao wanasiasa kwa maslahi ya kisiasa ili kuipenya geti ya Ikulu.
 
Najaribu ila siwezi kutenganisha CCM NA LISSU.


πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸšΆπŸšΆπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜ŽπŸ™πŸ˜²πŸšΆπŸ˜ŽπŸ˜ŽπŸšΆπŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜€πŸ˜€
 
Back
Top Bottom