Tundu Lissu kutoa mada siku ya Katiba (Katiba Day)

Tundu Lissu kutoa mada siku ya Katiba (Katiba Day)

Hii ni MADA ya wanasiasa wanaotafuta unafuu wa kupenya kuingia IKULU.

Wananchi MADA yetu ni MAENDELEO STAHIMILIVU pamoja na huduma bora za kijamii.
Hayo maendeleo unayoyataka ni siasa kama ulikuwa hujui ndio ujue, ile bajeti inayosomwa kule bungeni ndio inatoa muelekeo kama taifa tunaelekea wapi kiuchumi na kijamii, ukiona watu wanapigania Katiba Mpya ujue wanataka kila mwananchi aifaidi nchi yake.
 
lisu ana kesi nyingi sana mahakamani, au umesahau ? huyu akirudi ni moja kwa moja jela
Utashangaa sana na mwisho utaona matokeo yake....

Kama shina (Mwendazake) lililosababisha na kubumba kesi hizo kwa nia OVU ya kutesa tu liko "jela ya mchangani" yaani limelala mavumbini , huyu Tundu Lissu aliye hai atakuwa jela ya wapi sasa...?

Narudia tena, kama mlivyopigwa bumbuazi na butwaa kwa kifo kisichotarajiwa cha "Mtesi mkuu" wa Tundu Lissu, ndivyo mtakavyoshtuka na kupumbaika kwa yale yajayo...

Tutasema, "...msiyempenda amekalia kiti cha enzi cha utawala wa Tanganyika...!"
 
Nasubiri kwa hamu kuu, jamaa ni kichwa saana...madini tupu!! Binafsi hajawahi niangusha hoja nzito zenye mashiko!! Hazina ya taifa.

Ni watanzajia wachache saana wenye level kama yake!!
Mimi sijui kwa nini TAL hatumiwi "fully & effectivelly" na serikali!!
Huu mtindo wa watu wenye "uwezo mkubwa wa kiakili,kifikra,kiuweledi na kizalendo" kutotumika ipasavyo kitaifa, ni wa hovyo sana sana.
 
Katiba Day ni siku ambayo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeandaa kongamano la kujadili umuhimu wa kuwepo kwa Katiba Mpya itakayotokana na Raia wote, pamoja na mjadala huo pia kutakuwa na mjadala wa kuchagiza uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi.

Tundu Lissu atakuwa miongoni mwa magwiji watakaotoa mada.

Kongamano hilo litafanyika tarehe 1 JULY 2021.

View attachment 1827616
Siku muhim Sana ,vyema ikimpendeza mh SSH ,basi ajumuike,

Hongera sana Shujaa wa Taifa, Tundu Antipas Mughwai Lissu hongera sana CHADEMA, kwa kuelimisha umma kuhusu mambo mbalimbali muhimu sana.

Nimekuwa nikifuatilia ONE ON ONE WITH TUNDU LISSU, CYBER LOUNGE zote kutoka NADJ MEDIA, na nimefaidika sana.

Ipo haja kubwa sana ya watu au vikundi wanaojitambua, kuwa jasiri na kuchochea mjadala katika jamii kuhusu Katiba Mpya.

Angalau serikali ya Rais Samia inaonekana kutoa fursa kwa mijadala hii. Hiyo ni mijadala muhimu sana. Karibuni sana kushiriki na kuelimika na kuelimisha wengine
 
Back
Top Bottom