Tundu Lissu kutoa mada siku ya Katiba (Katiba Day)

Tundu Lissu kutoa mada siku ya Katiba (Katiba Day)

Katiba Day ni siku ambayo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeandaa kongamano la kujadili umuhimu wa kuwepo kwa Katiba Mpya itakayotokana na Raia wote, pamoja na mjadala huo pia kutakuwa na mjadala wa kuchagiza uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi.

Tundu Lissu atakuwa miongoni mwa magwiji watakaotoa mada.

Kongamano hilo litafanyika tarehe 1 JULY 2021.

View attachment 1827616

Kamanda Sirro na kamanda Muliro wafahamishwe katiba day haiahirishwi wala kusitishwa sitishwa tu kama Mambosasa na Muroto walivyojisikia kufanya.

Tujipange zaidi kwa hili.
 
Hizo fedha zinazotumika, ni aheri zikaelekezwa kujenga ofisi za chama

Sababu moja tu, Mpaka muda huu, Jambo la katiba ni kama linsonekana ni la kichama zaidi kuliko kuonekana ni la kitaifa na la wananchi wote?

Kulifanyika makosa makubwa sana kipindi kile ilipopatikana fursa ya kuandikwa kwa katiba mpya, matokeo yake kama nchi tukapata Ukawa, kitu ambacho kama wananchi, hutukuwaagiza hivyo waliopata fursa ya kutuwakilisha na wakaamua kutuletea dubwasha hilo lisilo na maana
 
Hizo fedha zinazotumika, ni aheri zikaelekezwa kujenga ofisi za chama

Sababu moja tu, Mpaka muda huu, Jambo la katiba ni kama linsonekana ni la kichama zaidi kuliko kuonekana ni la kitaifa na la wananchi wote?

Kulifanyika makosa makubwa sana kipindi kile ilipopatikana fursa ya kuandikwa kwa katiba moya, matokeo yake kama nchi tukapata Ukawa, kitu ambacho kama wananchi, hutukuwaagiza hivyo waliopata fursa ya kutuwakilishe kutuletea dubwasha hilo lisilo na maana
UKAWA ni matokeo ya unajisi uliofanywa na CCM dhidi ya mchakato wa kuandika Katiba.Wakati ule CCM na wapambe wao walihofia anguko lao kwenye kipengele cha Muungano wa
serikali tatu.
Tusipotoshane.
 
BAVICHA_&_CHASO_on_Instagram:_“✌️✌️✌️”%22_.jpg
 
Back
Top Bottom