Huyu Tundu Lissu alipokuja hapa Tanzania na CHADEMA kumpa ridhaa ya kugombea ubunge kama njia ya kumpoza baada ya wao Chadema kupanda njama za kumshambulia ili waichafue Tanzania, amekuwa kama mtu ambae hajui nini anakifanya majukwaani. Maana amekuwa mtu ambaye anaropoka maneno ya uchochezi ambayo nia yake ni kuleta fitina ili kuleta machafuko kwa nchi yetu.
Mgombea urais ambae unatafuta kuwa rais wa JMT huwezi kuongea hoja ambazo hata mtu ambae hana akili timamu hawezi kuziamini. Mfano mgombea urais unasimama jukwaani na kusema eti Serikali inatengeneza njama za kuweka itilafu kwenye ndege unayosafiria ili upate ajali. Sasa kama una hakika na hili kwa nini usichukue hatua stahiki. Maana ndege unayosafiria ni ya kukodi. Sasa hao wamiliki wa hiyo ndege kwa nini usiwashitaki kwa kushiriki kupanga njama kubwa kama hizo? Maana hilo sio jambo dogo.
Unaenda Zanzibar bila aibu na bila kutumia busara unatamka kuwa, upinzani umekuwa unashinda uchaguzi wa Zanzibar tokea mwaka 1995. Je, unao ushahidi juu ya hili? Unaenda Zanzibar unadai kuwa eti Tanganyika inapeleka ubabe wake wa kijeshi Zanzibar je hiyo Tanganyika unayoisema ni ipi? Maana ibara ya pili ya katiba ya JMT ilifuta kitu kinachoitwa Tanganyika.
Sina mengi ya kusema ila wewe mgombea wa urais wa Chadema hakuna unachotafuta. Hii ni kwa sababu wewe unajitambua hufai kuwa rais wa JMT bali unaeneza siasa za chuki ili kuleta mifarakano na chuki ambayo matokeo yake ni vurugu.
Naomba nikuulize.
Zanzibar ni NCHI au ni sehemu ya TANZANIA kama Mtwara, Mbeya, Mwanza, Kagera, Mara, Dodoma, Dar es salaam, Arusha, Morogoro, Shinyanga, Simiyu, Singida, Tabora, Kigoma, Ruvuma au Geita?
Je, Watanzania wa Bara Wenye shahada za kupigia kura wanaruhusiwa kupiga kura kumchagua Rais wa Serikali MAPINDUZI ya Zanzibar?
Je, Zanzibar kuna IKULU ambayo ni makazi ya Rais wa Serikali ya MAPINDUZI ya Zanzibar?
Zanzibar kuna ZEC na Bara kuna NEC,
Je, Viongozi wa ZEC huteuliwa na nani?
Je, WAGOMBEA wa Nafasi za Uongozi wa nafasi za KISIASA Zanzibar ni Wazanzibar tu au na Wabara wanaruhusiwa KUGOMBEA?
NINI MAHUSIANO YA ZEC NA NEC?
Kwa Nini TUME YA UCHAGUZI isiwe moja?
Je, Rais wa Serikali ya MAPINDUZI ya Zanzibar anaweza kutangaza VITA DHIDI YA ZANZIBAR?