Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Nimesikia kauli za hatari katika harakati za kampeni za urais zinazotumiwa na Mh Tundu Lisu kwenye mikutano ya CDM. Hoja za kikabila! Oh eti JM kabila lake ni Mzinza, Msubi na siyo Msukuma kwa hiyo watu wa Mwanza wasimhesabu kama mwenzao!
Kweli tumefika huko? Wanataka kuturudisha kwenye ukabila? Wasukuma wa Mwanza hawana ukabila, ndiyo maana wabunge wao ni Wachaga na Wajaluo - hawa walichaguliwa kwa sababu ya uchapa kazi wao, wakawaacha wasukuma wenzao akina Dialo,Masha, Cheyo n.k. Wao huchagua mchapakazi, JM watamchagua kama wataamini ni mchapakazi hodari na wala siyo kwa sababu ya kabila lake. Watanzania wote watafanya hivyo.
Kama tunalitakia mema Taifa letu, tuache kabisa kuingiza masuala ya ukabila katika hizi kampeni. Afadhali hata yule Prof Safari aliyejaribu kutumia tuhuma dhidi ya JM ya ufisadi sijui wa mahindi, kugoma kuwa shahidi wa kesi ya RA, watumishi wa serikali kuuziwa kwa mkopo nyumba walizokuwa wamepangishiwa na serikali.
Mambo ya kupakana matope kwenye kampeni zinakubalika na tumezizoea. Endeleeni kupakana matope - kila upande, lakini tafadhali sana sana tusitaje mambo ya makabila.
Waelimisheni na wale Yeloo wa Arusha watulize mnkali - tunatafuta rais wa Taifa na siyo Laigwan wa Tanzania!