Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeshasema sana kuhusu huyu Jamaa yetu sii mwanasiasa kabisa sijui kwa nini Chadema wanampa jukwaa. Huyu abakie katika mambo ya sheria mahakamani tu..
Niahidi kuwa utampigia kura ya ndiyo Mh. Dr. Magufuli!
Lisu nilimsikiliza mwanzo mwisho ni kejeli tu,na kuonyesha hofu aliyo nayo kwa Magufuli muda wote aliopewa hakuzungumza nini chama chake kinataka kuwafanyia Watanzania kuelekea uchaguzi mkuu! Alijikita kumtaja mara
nyingi sana tena akimtambulisha kwa wanachadema na kutumia Air time kumnadi mgombea wa CCM bila kujijua kweli Lisu kwa mara ya kapote njia!
Mbowe, Slaa, Mnyika, Tundu, Sugu hawa kabila lao ni lipi?
Amesema kabila la magufuli ni ccm na ndo ukweli
umesema exactly alosema Lisu na ni ukweli mtupu.CCM ni kabila la mafisadi ili uwe mwana CCM lazima uwe fisadi.Magufuli ni mmoja wao amewekwa kuendelea kulinda mafisadi.
Nimesikia kauli za hatari katika harakati za kampeni za urais zinazotumiwa na Mh Tundu Lisu kwenye mikutano ya CDM. Hoja za kikabila! Oh eti JM kabila lake ni Mzinza, Msubi na siyo Msukuma kwa hiyo watu wa Mwanza wasimhesabu kama mwenzao!
Kweli tumefika huko? Wanataka kuturudisha kwenye ukabila? Wasukuma wa Mwanza hawana ukabila, ndiyo maana wabunge wao ni Wachaga na Wajaluo - hawa walichaguliwa kwa sababu ya uchapa kazi wao, wakawaacha wasukuma wenzao akina Dialo,Masha, Cheyo n.k. Wao huchagua mchapakazi, JM watamchagua kama wataamini ni mchapakazi hodari na wala siyo kwa sababu ya kabila lake. Watanzania wote watafanya hivyo.
Kama tunalitakia mema Taifa letu, tuache kabisa kuingiza masuala ya ukabila katika hizi kampeni. Afadhali hata yule Prof Safari aliyejaribu kutumia tuhuma dhidi ya JM ya ufisadi sijui wa mahindi, kugoma kuwa shahidi wa kesi ya RA, watumishi wa serikali kuuziwa kwa mkopo nyumba walizokuwa wamepangishiwa na serikali.
Mambo ya kupakana matope kwenye kampeni zinakubalika na tumezizoea. Endeleeni kupakana matope - kila upande, lakini tafadhali sana sana tusitaje mambo ya makabila.
Waelimisheni na wale Yeloo wa Arusha watulize mnkali - tunatafuta rais wa Taifa na siyo Laigwan wa Tanzania!
Dr Akili
CCM ndiyo wanataka kutumia hoja ya ukabila, Tundu lissu alichosema ,kama ulimwelewa ni kwamba ,Magufuli hata awe kabila gani, ni ccm yule yule with all Tabia za kiccm kama, Wizi, ufisadi Rushwa pamoja na kuwakandamiza wananchi kwa manufaa ya wachache. TUMIA UBONGO KUFIKIRI Ndugu ile ni kauli za kifasihi.....
CDM sikuzote hawana hoja za maana hapo ndipo akiliyake imeishia
Wanaosifia utendaji wa magufuli wanampima kwa barabara za lami. Lakini ndiyo hizi barabara zinazojengwa chini ya kiwango kila iitwapo leo.
Kwa sababu ya kujengwa chini ya kiwango tumepoteza ndugu zetu wengi kwa ubovu wa barabara. Kwa mfano, ajali ya pale Mafinga iliyoangamiza wengi ni kwa sababu ya ubovu wa barabara ambazo zimejengwa hivi karibuni.
Sifa ambazo ni za kijinga anazopata Magufuli ni barabara ikiishajengwa kufoka kwamba ipo chini ya kiwango. Swali ni anakuwa wapi mpaka asubiri zimalizike ndipo atafute TBC kwenda kututangazia kwamba jamani barabara hii chini ya kiwango, na nyingine nanyingine???.
Dr Akili
Hivi huku ndani ni kwanini watu wanatabia ya kujiita vitu wasivyo??? Yaani opposite kabisa. Huyu ni doctor BRAINLESS.