Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,116
- 8,652
Lisu nilimsikiliza mwanzo mwisho ni kejeli tu,na kuonyesha hofu aliyo nayo kwa Magufuli muda wote aliopewa hakuzungumza nini chama chake kinataka kuwafanyia Watanzania kuelekea uchaguzi mkuu! Alijikita kumtaja mara nyingi sana tena akimtambulisha kwa wanachadema na kutumia Air time kumnadi mgombea wa CCM bila kujijua kweli Lisu kwa mara ya kapote njia!
nadhani kabila lao ni UKAWA.
Acha uongo. Kama wewe ni kiziwi omba uambiwe kilichoongelewa acha kukurupuka kama brother K.
Lisu nilimsikiliza mwanzo mwisho ni kejeli tu,na kuonyesha hofu aliyo nayo kwa Magufuli muda wote aliopewa hakuzungumza nini chama chake kinataka kuwafanyia Watanzania kuelekea uchaguzi mkuu! Alijikita kumtaja mara nyingi sana tena akimtambulisha kwa wanachadema na kutumia Air time kumnadi mgombea wa CCM bila kujijua kweli Lisu kwa mara ya kapote njia!
CCM ndiyo wanataka kutumia hoja ya ukabila, Tundu lissu alichosema ,kama ulimwelewa ni kwamba ,Magufuli hata awe kabila gani, ni ccm yule yule with all Tabia za kiccm kama, Wizi, ufisadi Rushwa pamoja na kuwakandamiza wananchi kwa manufaa ya wachache. TUMIA UBONGO KUFIKIRI Ndugu ile ni kauli za kifasihi.....
Dr Akili kampeni za urais zimeshaanza?Ni Magufuli na nani wanapambana kwenye kiti cha Urais?
Mbowe, Slaa, Mnyika, Tundu, Sugu hawa kabila lao ni lipi?
Tundu si nasikia ana kale kagonjwa ka kupelekwa Milembe. Utatumiaje dakika 35 unazungumzia ukabila wa Magufuri mara si msukuma, si mzinza si msubi nani alitaka kujua upuuzi huo. Mbona wewe hujisemi ni mdudu gani toka msitu upi!!! Halafu kuna mburura humu wanatetea ujinga. Hata huyo sijui Prof gani amabaye kasoma wala hakuelewek, anakuja na ngonjela dhaifu hazina ushahidi na mburura kama kawaida wanakenua meno. Hii taabu hii.Lissu Unaleta hofu katikati ya kandamnasi ili uonewe huruma. KWISHA KWISHA KABISA. AKA KAJITU NI HATARI KATENGWE KAMA KALIVYO
Mkuu Paschal hao wanaoeneza habari kuwa Tundu Lissu katika hotuba yake ya Mwanza ameendekeza ukabila, hao ni Propagandists wakubwa ambao humu JF huwa 'tumewabatiza' kama Buku 7 Lumumba Sports Club.Km ulifuatilia alisema magufuli hajasimama km mmoja wa hayo makabila bali kasimama kama ni miongoni mwa kabila la ccm na si kama ulivyotoa maada. Usipotoshe umma kama hukuelewa ungeuliza nini alichosema kwa walioelewa wangekusaidia kuliko kudakia kutoa maana ukiwa hujui ata kipi kilichosemwa.
Km ulifuatilia alisema magufuli hajasimama km mmoja wa hayo makabila bali kasimama kama ni miongoni mwa kabila la ccm na si kama ulivyotoa maada. Usipotoshe umma kama hukuelewa ungeuliza nini alichosema kwa walioelewa wangekusaidia kuliko kudakia kutoa maana ukiwa hujui ata kipi kilichosemwa.
CCM imeingiwa hofu, Magufuli kuwa shughuli
KUNA hofu imetanda ndani ya CCM; hofu ambayo inajaribu kufichwa mapema kwani kama mambo hayatobadilika ndani ya miezi hii mitatu hivi iliyobakia kabla ya Uchaguzi Mkuu basi chama hiki kikongwe zaidi nchini kinaweza kujikuta kikipumzishwa kutoka madarakani kwa nguvu. Dalili ya hofu hii imeonekana baada ya kutangazwa kwa mgombea wao wa kiti cha Urais Dk. John Pombe Magufuli.
Mojawapo ya mambo ambayo yametokea baada ya Magufuli kutangazwa ni kauli za kuwa yeye anakubalika na anachagulika. CCM imetaka kuliaminisha taifa kuwa Magufuli siyo tu anajulikana kwa utendaji kazi wake, na kuwa wananchi wengi wanampenda na wanaweza kumchagua. Kiasi kwamba wametaka watu waamini kuwa Magufuli ni Rais anayesubiria (President in waiting). Kwamba, upinzani hauna nafasi hata kidogo ya kumnyanganya uwezekano huo.
Ukweli ni kuwa matendo ya CCM hayaoneshi kujiamini huku. Kama kweli CCM inaamini Magufuli anajulikana na kazi zake zinakubalika nchi nzima kwa nini juhudi kubwa sana inajaribu kufanywa ya kumtambulisha. Unamtambulisha vipi mtu ambaye tayari unaamini anajulikana, kufahamika na kukubalika? Ukiangalia utaona kuwa CCM inataka kumtumia Magufuli kukibeba chama; tatizo ni kuwa Magufuli mwenyewe ukiondoa kukariri kwake takwimu mbalimbali utendaji kazi wake una shaka. Tayari wizara ambayo amekalia imeshagubikwa na kashfa lukuki na hili peke yake lingetosha hata kumchafua. Akija mgombea mzuri kutoka upinzani na akajizibu hizi takwimu za Magufuli, basi Magufuli na CCM iko matatani. Yote haya yanatosha kufanya watu wajiulize mara mbili kama kweli Magufuli hatokuwa shughuli kweli kweli.
CCM imepasuka, rekodi yake mbovu, na upinzani ukimsimamisha mgombea makini, Magufuli ataweza vipi kushinda? Njia pekee ya kushinda katika mazingira ya namna hiyo ni matumizi makubwa ya nguvu, vyombo vya dola na hata kuliingiza jeshi katika siasa kama walivyofanya chini ya Jenerali Shimbo mwaka 2010. Vyovyote vile ilivyo hata hivyo kuna hofu imetanda kwa CCM; hofu kama vile wingu zito la mvua lenye dalili ya radi na ngurumo. CCM hawajui sasa wafanye nini zaidi ya kuombea Magufuli aweze kuwaokoa. Akishindwa je Hili ndilo swali la kuogopesha zaidi kwa kila mwana CCM
Chanzo: Raia Mwema (22, July 2015)
CDM sikuzote hawana hoja za maana hapo ndipo akiliyake imeishia