Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kuzuiwa kutumia Chopa yawa Shubiri kwa CCM

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu kuzuiwa kutumia Chopa yawa Shubiri kwa CCM

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,358
Tundu Lissu is talk of the Town au kwa lugha yetu Tundu Lissu ndiye Habari ya Mjini kwa Sasa.

Mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu ameteka nyoyo za Watanzania na ukweli kabisa bila kuongeza chumvi Tundu Lissu ndiye mgombea wa Urais mwenye mvuto kuliko mgombea mwingine yeyote katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kiliomba kibali Cha kutumia Chopa kwa mgombea wake wa Urais ili iwe rahisi kuweza kufika maeneo yote ya kampeni kwa wakati.

Hata hivyo kwa makusudi Mgombea huyo wa Chadema amewekewa vigingi na mamlaka ili kumkwamisha kutumia Chopa hiyo kwa malengo yasiyofahamika.

Tundu Lissu na wasaidizi wake walishushwa pale Airport ya Dar na mamlaka ya Anga wakiwa wameshapanda helikopta hiyo kuelekea kwenye Mkutano wa Kampeni mkoa wa Pwani.Mpaka Leo takriban mwezi Sasa bado mgombea huyo hajaruhusiwa kutumia Chopa hiyo.

Hata hivyo Mungu ana makusudi yake Pamoja na njama za kumzuia Tundu Lissu kutumia Anga bado ameweza kuhutubia mikutano yote Kama inavyoonyesha kwenye ratiba.

Pili Lissu amekuwa akikutana na watu wengi zaidi anapotumia usafiri wa Barabara kwa kusimama njiani kusalimiana na Maelfu ya watu na kuwaachia ujumbe wa kuchagua #UhuruHakiNaMaendekeoYaWatu#

Lissu amekuwa akikaribishwa kwa maandamano makubwa ya Malaki kwa maelfu ya watu kilometa 10 mpaka 20 kabla ya kuingia viwanja vya mikutano na kusindikizwa umbali huo huo baada ya mikutano kitu kinacholeta hamasa kubwa kwani Ingekuwa anatumia Chopa isingewezekana.

Wachunguzi wa siasa wanasema hata Kama Watawala watamruhusu kutumia helikopta kwa siku zilizobaki asikubali Tena kwani kutumia gari Kuna manufaa zaidi na ujumbe wa mabadiliko unafika sehemu kubwa zaidi.

Mara baada ya Tundu Lissu kuzuiwa kutumia helikopta harakaharaka CCM walileta helikopta yao na kujigamba wao wataitumia chopa kwa sababu hakuna wa kuwazuia.

CCM walidhani kwa kula njama na CDM kuzuiwa kutumia Chopa Basi ilikuwa ni pigo kubwa kwa Lissu lakini imeonekana kinyume chake na Sasa wanatamani mgombea huyo wa CDM aruhusiwe kutumia Chopa ili asiweze kukutana na Malaki kwa mamilioni ya watu anaokutana nao mabarabarani wakati akisafiri kwa gari


 
Kwa hiyo CHOPA waliyokodi Kenya wanatamani kuilusisha? Maana hapa Geita waziri Mkuu amekuja kwa gali,na yeye ame ogopa kuipanda?labda CHOPA wapewe kina Kigwangala na msukuma na wanamziki wao
 
Polepole aende polepole, asibabaike na hapaswi kujibu kila tuhuma.
 
Mleta mada ulichoandika ni sahihi kabisa. Hata Magufuli alinufaika sana kwa usafiri wa gari kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015
 
..I dont mind CHADEMA kutumia helikopta kimkakati, haswa maeneo ambayo muda siyo rafiki.

..kwamba wachanganye usafiri wa barabara na helikopta kwa ajili ya TL na Salum Mwalimu.

..lakini hakuna shaka kwamba kusafiri kwa barabara kumemsaidia TL kukutana na wananchi.
 
1601209312792.png

Spana zinazidi kukaza.
 
..I dont mind CDM kutumia helikopta kimkakati, haswa maeneo ambayo muda siyo rafiki.

..kwamba wachanganye usafiri wa barabara na helikopta kwa ajili ya TL na Salum Mwalimu.

..lakini hakuna shaka kwamba kusafiri kwa barabara kumemsaidia TL kukutana na wananchi.
Umenena vema
 
Back
Top Bottom