Uchaguzi 2020 Tundu Lissu Mbona Watanzania wanakuelewa ila punguza ukali kidogo we jenga tu hoja

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu Mbona Watanzania wanakuelewa ila punguza ukali kidogo we jenga tu hoja

JERRY

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
630
Reaction score
502
Najua pengine ukali wa speech zako kwa namna Fulani unachangiwa na madhila uliyopitia ambayo Mungu wa Rehema alikuepusha.

Labda tu kukushauri unapoanza safari ndefu ya kampeni katika kuwaomba watanzania wakuchague jaribu kuwa moderate unapokuwa unatoa speech zako na pia jikite Zaidi katika kujenga hoja mbadala kupitia ilani ya chama chenu na kuzifafanua kwa kina.

Tukubali ama tusikubali JPM kwa wastani kafanya mambo mazuri sana ndani ya muda mfupi na haswa kwenye ujenzi wa miundombinu.; SGR, Bwawa la umeme, Mabarara, Vivuko, Madege,……nk

Sasa kuwaaminisha watu kwamba wewe unaweza kuyafanya Zaidi ya haya ambayo JPM tayari kasha yaanza mpaka majirani wanatuonea wivu inahitaji convincing power ya hali juu ingawa najua wewe unayo.Ila lazima jasho likutoke.

Na ukumbuke yote mazuri yaliyofanyika yanasemwa kila siku kwenye vyombo vyetu vya habari nchini ambavyo wewe kwa mazingira yaliyopo huna coverage navyo achilia mbali kualikwa kwenye interviews.

Jambo zuri kwenye kampeni hizi wagombea wote ni outspoken speakers

Kila la heri
 
Shughuli ni pevu sana kwa upinzani.
2025 sijui Nyarandu ataweza kuchuana na Hussein Mwinyi baada ya Magufuli kumaliza miaka yake 10
 
Tusubiri tu uchaguzi Mana amekuja nakasi Sana ya kuelezea wananchi wamuelew
 
Shughuli ni pevu sana kwa upinzani.
2025 sijui Nyarandu ataweza kuchuana na Hussein Mwinyi baada ya Magufuli kumaliza miaka yake 10
 
Lissu anategemea kura za huruma tu na sivinginevyo,kakazana kumshambulia Ma gufuli personal akisahau kuwa hiyo ni taasisi ,badala ya kunadi sera na vipaumbele
 
wewe kama nani wa kumshauri TAL

nyie watu ni washirikina sana
 
Lissu anategemea kura za huruma tu na sivinginevyo,kakazana kumshambulia Ma gufuli personal akisahau kuwa hiyo ni taasisi ,badala ya kunadi sera na vipaumbele

Hamna cha taasisi, rais ni rais tena kama mtu, hilo neno taasisi liko kinadharia zaidi, lakini maamuzi yanafanyika kwa utashi wake binafsi kwa 90%+
 
Ushauri wa uzi namba moja sio mbaya, iwapo Lisu atauchukua unaweza kumuongezea mbinu ya mchezo. Jambo ambalo sina shaka nalo ni iwapo Lisu atapanga mashambulizi yake vizuri, hata kama Magufuli atamshinda hata yeye atavuja jasho, na hatakuwa na uwezo wa kulazimisha kujiongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi. Na iwe isiwe, tume hii ya uchaguzi itarekebishwa,na hasa hasa katiba mpya itapatikana. Narudia tena kushauri, Lisu apange hoja zake vizuri, hata asiposhinda, impact yake itakuwa kubwa sana kwenye mustakabali wa taifa hili.
 
Lissu style yake kuongea ni ileile miaka yote. Anatakiwa asipunguze, Magufuli ambaye ndiye mshindani wake mkuu siyo wa kubembeleza.
 
Lissu anategemea kura za huruma tu na sivinginevyo,kakazana kumshambulia Ma gufuli personal akisahau kuwa hiyo ni taasisi ,badala ya kunadi sera na vipaumbele
Kama rais ni taasisi mbona kutwa anasema yeye hapangiwi cha kufanya, mpaka katiba anavunja mchana kweupe, pia asingekuwa anasema ni serikali ya Magufuli, mpaka jamaa yake Che mkapa aliyembeba anamtaka ajirekebishe kuwa sio ya Magufuli.
 
Ukali upi wa maneno aliozungumza lisu ambao umevuka mipaka au unavunja sheria, kwakusema kama kura zitaibiwa hatakubali na kuhimiza watu kuandamana!!?

Sio yeye tu ambae hatakubali wengi hatutakubali na kwakua hatuna pakusemea au pakushtakia lazima tuandamane ujumbe uifikie dunia.

Ata CCM wakilalamika kuibiwa watanzania tuko tayari kuona haki inatendeka.

Lakini hakuna mtanzania anaependa tufike uko na mwenye jukumu la kuepusha watu kuingia barabarani ni tume ya uchaguzi kwa kufanya kazi yake kwa weledi.
 
Lissu anategemea kura za huruma tu na sivinginevyo,kakazana kumshambulia Ma gufuli personal akisahau kuwa hiyo ni taasisi ,badala ya kunadi sera na vipaumbele
Acha utopolo kwa hiyo taasisi ndo inamkula Yule Dc wa.....
 
Naukubali Sana Mkwara wa lissu, Hawa ccm siyo wa kuwachekea,

Pia asipo onyesha ukali atapambana vipi na ufisadi,

Kumbuka Yule Ni amiri Jeshi mkuu kuanzia october
 
Back
Top Bottom