Pre GE2025 Tundu Lissu: Mbowe alimtuma Wenje agombee nafasi yangu ili waniondoe, nikasema sasa nitagombea nafasi ya huyo aliyekutuma

Pre GE2025 Tundu Lissu: Mbowe alimtuma Wenje agombee nafasi yangu ili waniondoe, nikasema sasa nitagombea nafasi ya huyo aliyekutuma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu

Tundu Lissu "Ninajua kuwa Mbowe ndiye aliyemtuma Wenje agombee nafasi ya Makamu Mwenyekiti nikasema sasa nitagombea nafasi ya huyo aliyekutuma"
View attachment 3194129
Huu mchongo wa wa Mbowe kupanga kumuondoa Lissu na ndipo Lissu akaamua kumkabili ulishajulikana kitambo na mimi niliufungula uzi humu.

Tundu tunza kauli kaka,

Siasa zina pande nyingi sana.... Unless ujiandae kuwa kama kina Che Guavara

Duniani sio kila kitu cha kusema kuna vingine vya kuzikwa navyo.

Hiyo grandiosity na self inflicted grandiosity haikufikishi popote...

Unataka kusema Wenje ana udogo gani kwenye siasa za CDM kukuliko?

Unakumbuka unachangisha mchango wa gari ni mwaka sasa hujafikisha mil 150? Jiulize tu kuna nini? Hawa washabiki kwanin huwaoni kwenye course zako?
Unapoteza muda wako...kila chenye mwanzo kina mwisho...
 
Move ya Mwenyekiti kumleta aliyekula pesa za Abduli ndo ikawa kichocheo zaidi kwa mheshimiwa Lissu kuona kuwa hapa sasa hatuna mwenyekiti bora aende akarekebishe mambo!

kwa hiyo kumbe hata plan za jinsi atakavyoivusha chadema kama mwenyekiti hana, sababu KUU ya kugombea ni kukomoana? yaani mwaga mboga nimwage ugali? chadema deserves better, man …
 
Lissu na Mbowe hawapikiki tena chungu kimoja.

Huu uchaguzi utakiacha Chadema njia panda.

Fundi Mchundo Tindo
Kabisa Mkuu. Na haikupaswa kabisa kuwa hivyo. Mimi bado naamini kuwa wafuasi wa Lissu (bila shaka kwa baraka zake) wasingeanza kwa shari kampeni yake, Mbowe angestaafu. Sasa hivi yeyote atakayeshinda atakuwa na chama chenye majeraha makubwa. Labda wanaamini kuwa CDM ilipofika haiwezi kuwa kama TLP au NCCR Mageuzi.! Wanaweza kushangazwa.

Amandla...
 
Hivi hawa si huwa wanatuhubiria demokrasia?! Sasa imefika muda wa wao kuonyesha demokrasia kwa vitendo wanataka kuuana
 
Kwa Mujibu wa Dialo huko Club house Dr Slaa alikula hela za JPM na Hela za Edo ... Baada ya kuahidiwa na ubalozi akaona akimbie mazima

Wanasiasa vishoka wana midomo mipana sana
Dr Slaa Ndiye aliyeratibu ziara ya Papa Yohanne Paul II

Baada ya ile ziara ndio Rais Mwinyi akamuomba aingie serikalini mazima

Usimchukulie poa 😂😂🔥🔥🔥🔥
 
Kabisa Mkuu. Na haikupaswa kabisa kuwa hivyo. Mimi bado naamini kuwa wafuasi wa Lissu (bila shaka kwa baraka zake) wasingeanza kwa shari kampeni yake, Mbowe angestaafu. Sasa hivi yeyote atakayeshinda atakuwa na chama chenye majeraha makubwa. Labda wanaamini kuwa CDM ilipofika haiwezi kuwa kama TLP au NCCR Mageuzi.! Wanaweza kushangazwa.

Amandla...
Haiwez kuwa NCCR instantly..
Ila ukata utaitafuna sana CDM huyo jamaa akishinda.

Atapigwa na usaliti huu anouona kwa Mwenyekiti cha mtoto..

Miaka miwil atarudi Belgium..

Kura kwa upinzani zipo za kutosha ila kwa muktadha na wakati ni mwendo wa kupigwa viatu na matokeo Urais ni asilimia 99😂
 
Back
Top Bottom