Pre GE2025 Tundu Lissu: Mbowe ndiye alimualika Rais Samia kama mgeni rasmi kwenye Kongamano la BAWACHA na kumuandalia Tuzo ya Maridhiano

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Lissu anazidi kumwaga mchele! Anasema kwenye mkutano ule BAWACHA hawakumualika Rais Samia kama mgeni rasmi bali aliakiwa na Mbowe! Baada ya kuwa kamualika ndio alikuja kuwajulisha wengine kuwa amemualika Samia kama mgeni rasmi.

Lissu anasema kwenye hili pia waliamua kukaa kimya na kuficha aibu hii aliyoleta Mbowe, lakini hili waliliobgea kwenye kamati kuu baada ya kutokea.

Lissu amelichomekea hili wakati anaongelea suala la maridhiano baada ya Mbowe kusema maridhiano yana faida wakati alienda kuongea na Samia kinyume na makubalino ya chama.

Pia soma:
Ambapo aliongeza pia hata tuzo ya maridhiano aliyokabidhiwa Rais Samia siku hiyo ilikuwa imendaliwa na Mbowe; "Yalikuwa ni maamuzi ya Mwenyekiti pekee yake kwa haya mambo mawili. Hakuna kikao kilikaa kamati kuu kumwalika Rais Samia au kumpa tuzo," alisema Lissu, akimtaka Mwenyekiti Mbowe kuhojiwa kwa nini alitoa tuzo hiyo na kumleta Samia, wakati chama cha CCM kilikuwa hakijakubali chochote kuhusu maridhiano kati ya pande hizo.

Mbowe mbona anazidi kuwa CCM kuliko CHADEMA?!

Lissu ameyasema haya kwenye session inayoendelea club house leo Dec 23, 2024.
 
BAWACHA WENYEWE WANASEMAJE??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…