Ni muda wakusikia madini kutoka kwa Mhe. Tundu Lissu akiwa live VOA akichambua hoja na kujibu maswali mbalimbali kutoka katika chombo hiki cha kimataifa.
Karibu tumsikilize , nilitamana sana mahojiano Kama haya yangekuwa yanafanywa na televisheni na media zetu kama ilivyokuwa enzi ya JK lakini Sasa hivi wenye akili wanatakiwa wakae kimya na wasijadili chochote against current regime.
Ninachojiuliza Marekani imewahi kuacha kupiga hatua kwa ukosoaji unoendelea?
Kenya majirani zetu wamewahi kupoteza mikakati ya maendeleo kwa Uhuru wakuhoji na kujieleza?
Kwanini sisi tunataka kuwaaminisha watu maendeleo ni kunyamazisha vyombo vya habari.
Tundu Lisu alichaguliwa kwa mbwembwe kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema na wafuasi wa upinzani wakawa na matumaini makubwa kuwa atakuja na mawazo mapya ya kuinua Chadema na Upinzani kwa ujumla nchini. Laa! Kama ilivyokuwa alipochaguliwa kuwa rais wa TLS badala ya kufanya kazi za taasisi iliyomchagua Lisu yuko bize kufanya kazi zake na kujiimarisha yeye binafsi!
Tundu Lisu tokea achaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema hamna clip wala mkutano wowote akiipromote Chadema lakini anaendelea kulipwa mshahara mnono kama makamu mwenyekiti wa Chadema!!
Hili halikubaliki Lisu ni mfanyakazi hewa wa Chadema na anatakiwa kutumbuliwa haraka.
Bavicha amkeni mhoji matumizi ya hela za Chadema maana Mbowe ni mwenyekiti bubu