Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
siku zote Tundu Lisu ni mlopokaji na asieweza kudhibiti hisia zake anaposhangiliwa anaondoa kabisa hadhi ya upinzani nchini. Na hili ndio tatiizo la upinzani, hawa jamaa hawana uzalendo, heshma wala miiko.
JULIUS NYERERE-Humanist,Politician ,and Thinker.-POLE SANA TUNDU LISU,HUNA HADHI YA KUMKEJELI BABA WA TAIFA,JIKITE KATIKA KUJENGA HOJA ZAKO TU,UTAELEWEKA.
Huyu mganga njaa anaropoka kuwafurahisha MABWANA, lakini akumbuke kuna leo na kesho..........atapata hizo helkopta na nini.......lakini mwisho wake ni nini ?
Hapo tu alipo amebakiza muda mfupi sana ataanza kubeba makopo......sijui ni wangapi wanadhani jamaa yupo timamu upstairs.
Kati ya wanasiasa ambao wanatakiwa kufungwa gavana ni Tundu lisu. Kwenye Bunge hili la katiba wajumbe wako pale Kujenga ni kubomoa. Kama kuna makosa na dosari katika muundo wa muungano huu ndo wakati wake na si kupokea waasisi wa muungano. Bila hao waasisi ambao waliusimamia muungano ambao hadi leo miaka 50 upo, si wa kubezwa hata Kidogo. Mchango wao ni mkubwa mno kulinganisha na Lisu ambao kazi yake ni kuponda na katika nchi mchango wake katika Kujenga umoja, mshikamano, kudumisha amani hatujauona zaidi ya siasa za uhasama na utengano
Bwa mdogo hatofika mbali.Huyu kilaza hajui yeye asingekuwa bungeni kama sio kazi. Ya Mwalimu
Namuheshimu Lissu kwa michango yake bungeni lakini katika hili amenikera mno.alikuwa wapi kuyasema hayo enzi ya uhai wa Nyerere. Kama aliogopa kuchapwa viboko na akae kimya milele.
Tundu Lissu, kwenye ili la kumponda Nyerere, pro-Chadema wapo kimya masikini.
sijapenda kauli ya lissu na kama hakuwa na hoja ya kushauri juu ya serikali tatu ajuwe amepoteza yeye na wenzake wote waliokuwa wanatoa ufafanuzi juu ya hoja ya serikali tatu, na kama wanafikiri kupigiwa makofi ndio kukubalika kwa hoja yao watambue kuwa wamejifunga goli.
would've been "shocked" had you spoken something different!Punguza udini utaeleweka. Lissu hajachambua mambo kidini bali kisiasa na ameeleweka vizuri sana. Sasa wewe na makuwadi wenzio mnapoanza kutuletea habari za Kariakoo na misikitini hamueleweki. Mnafiki mkubwa wewe.
Bwa mdogo hatofika mbali.Huyu kilaza hajui yeye asingekuwa bungeni kama sio kazi. Ya Mwalimu
Nani kakwambia Waislam walikuwa wanaikubali Bakwata sababu ya Mufti Hemed Bin Jumaa?Ona sasa, wakati wa Sheikh Hemed Bin Jumaa Bin Hemed Bakwata yake ilikuwa sio iliyoundwa na Nyerere, au hamkujua kuwa waislam wote hawako chini ya Bakwata hadi mtu wa Shinyanga alipochaguliwa kwa haki kuiongoza?
Bibi yako Faiza Foxy ndio ameenda mbali zaidi kwa kuweka dharau kuwa Mh Sitta hajakutana na kiongozi wa Waislam, anadai Sitta alikutana na Pengo peke yake, kukutana na Sheikh Simba ni sawa na kutokutana na mtu. Acheni dharau zenu nyie watu wa pwani. Ni sawa na mzee wenu mwingine Mohamed Said anayedai kuwa uhuru wa Tanganyika uliletwa na kikundi fulani cha ma Alwatan wa pale Kariakoo,,, watu wa pwani mnajiskia sana nyie...
Tarehe 19 Desemba, 1968 serikali kama vile imegutushwa na taarifa ya Kwikima, iliipa BAKWATA Cerificate of Exemption na kuifungia EAMWS.[SUP]72[/SUP] Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya kwa niaba ya serikali alitoa taarifa fupi:
Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama.[SUP]73[/SUP]
Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao. Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo hilo.
Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS. Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama. Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza. Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam. Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA. Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe. Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu. BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa. Hivi ndivyo halikadhalika moto wa Waislam uliowashwa kwa kupatikana kwa uhuru waliopigania hadi ukapatikana ulivyokufa. Moto huu ulikuja ukawaka tena, lakini hiki ni kisa kingine. Insha Allah Mwenyezi Mungu akipenda tutakuja kukieleza.
Huu ndiyo ukawa mwisho wa kile kilichokuwa kikijulikana kama mgogoro wa Waislam ulivyomalizika. Mgogoro ambao ulianza pale mwalimu wa shule ya msingi asiyefahamika na yeyote alipofanya maandamano katika mitaa ya Bukoba akimuunga mkono Julius Nyerere na Azimio lake la Arusha na ukaishia kwa mwalimu huyu akiwa na nafasi juu katika jumuiya ya Kiislam ambayo ilikuwa ikichukiza machoni mwa Waislam. Mwalimu huyu ambae sasa amekuwa Makamu Katibu Mkuu wa BAKWATA alianza kazi yake kwa kuwashutua Waislam. Katika mkutano wa waandishi wa habari Adam Nasibu aliiomba TANU na ASP kujikinga na watu wanaohujumu umoja wa nchi kupitia dini. Akaendelea na kusema kuwa BAKWATA ni sawa na Baraza la Kikristo la Tanzania. [SUP]74[/SUP] Kwa kuwa Waislam walinyimwa fursa ya kujadili "mgogoro' hivi sasa kilichobaki na dhana tu, kuwa nini kingelitokea endapo wangeliruhusiwa kufanya mkutano ule ulioitishwa na EAMWS. Waislam wa Bukoba ambao ilitaarifiwa kuwa walifanya maandamano kuunga mkono Azimio la Arusha hawakutayarisha maandamano ya kuunga mkono BAKWATA. Dar es Salaam na katika miji mingi ya Tanzania, neno BAKWATA halina tofauti na tusi. Kumuita Muislam kuwa yeye ni mwanachama wa BAKWATA ni sawa na kumuita Mkristo mfuasi wa Yuda Iscariot, aliyemsaliti Yesu kwa vipande thelathini vya fedha.
He's so naive. Anapaswa kufahamu kwenye siasa hakuna `ukweli' udumuo na hali kadhalika uongo.Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost
NOMA SANA BABA wa TAIFA AMEMVUA NGUO,KILA NIKIFIKIRIA INAUMA.BUSARA HAIKUEPO.