Mwl. Nyerere hajatukanwa bali ukweli umesemwa labda useme kuwa, ukweli uliosemwa haujazoeleka Tanzania kusemwa!.
This is the point....
Katika hili la Nyerere J.K na hotuba ya Tundu Lissu, hii ndiyo HOJA na huu ndiyo UKWELI...
UKWELI unaitwa MATUSI. Hili ni tatizo kubwa linalomkabili binadamu....
Ni tatizo la kuto - acknowledge makosa na udhaifu wetu....
Akitokea mtu BOLD wa kusimama na kusema UKWELI wake au wa jambo fulani au juu ya mtu fulani, tunamshambulia na kumwita mtukanaji...!!
Kwa ujinga huu huu wa kibinadamu ilifika mahali, watu eti wakataka kumtangaza Nyerere -binadamu aliye sawa na wewe na mimi kama "mtakatifu fulani"....
Yaani binadamu amtangaze binadamu mwenzake, mtakatifu. Hii ni dhambi mbaya, hatari ya kukufuru...
Mungu aliona udhaifu huu huu enzi za Mussa kiongozi wa wana wa Israel kutoka nchi ya Misri kwenda Kanaani....
Wana wa Israel walimheshimu sana Mussa kwa sbb ya miujiza na matendo makuu aliyoyafanya ktk utukufu wa Mungu. Mungu yeye alimuona kama binadamu mwenye sifa za upungufu uleule wa binadamu wote...
Alipokufa, Mungu kwa makusudi kabisa na ili kuwaepusha kujiingiza ktk dhambi ya kuabudu " sanamu", alilificha kaburi lake mpaka leo maana kwa mioyo ya binadamu (wana wa Israel) wangeweza kuanza kuliabudu kaburi la Mussa na kumuacha Mungu wa kweli na wa haki, muumba na mwokozi wao....
Ndivyo ilivyo leo, kuwa, kuna watu wanaamini Mwl Julius K. Nyerere hakuwa binadamu wa kawaida. Hawa wanamtoa ktk level ya ubinadamu na wanataka kumpandisha level nyingine, yaa "uungu". Huku ni kuabudu "sanamu". Hili ni kosa na kufuru mbaya sana ktk sheria ya Mungu...
Generally, this is too bad...