Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Hahahaaa! Kufukia makaburi huku balaa. Ila Jamaa mnansafisha sana. Siamini kama alikosea. Nakumbuka kina clip Mwalimu alikiri kikosea piabktk uongozi wake
 
nyerere ni binaadamu tu sio mtakatifu wala malaika ... Lissu alikuwa na Point hapa
 
Unaweza kusema mengine yote lakini tukubaliane tu kuwa, Mwl. Nyerere hakuwa mtu wa kawaida. Historia inabainisha hivyo na wala siyo yeye anayebainisha kwenye historia. Think bigger!.

Tunapokubaliana kuwa hakuwa mtu wa kawaida, basi ni lazima tukubaliane na kuainisha kuwa huo "uspesho" wake hata awe "mtu asiye wa kawaida" ni wa namna gani...

Uspesho wa Nyerere, binafsi naweza kusema kuwa ndiyo huu uliochambuliwa kwa ufasaha na Tundu Lissu....

Ni mtu aliyejitengenezea mazingira ya kiasi cha baadhi ya watu kuanza kutaka kumuabudu kama ka - mungu fulani hivi....

Alijitengenezea mazingira kiasi ambacho sauti na mirindimo yake tu ndiyo isikike pote na wakati wote....

Huyo kidogo kidogo anaanza kupata mrithi wake ndg John Magufuli (Rais wa JMT wa sasa)....

Huyu naye (Magufuli) taratibu anaanza kuzoea vya kunyonga tu, vya halali kamwe hatakuja kuviweza....!!

Huyu (Magufuli) ni mtu ambaye kwa kiasi kikubwa amezoea kuishi kwa UONGO na UDANGANYIFU na ndiyo maisha anayoyaishi sasa....
 
Mwl. Nyerere hajatukanwa bali ukweli umesemwa labda useme kuwa, ukweli uliosemwa haujazoeleka Tanzania kusemwa!.

This is the point....

Katika hili la Nyerere J.K na hotuba ya Tundu Lissu, hii ndiyo HOJA na huu ndiyo UKWELI...

UKWELI unaitwa MATUSI. Hili ni tatizo kubwa linalomkabili binadamu....

Ni tatizo la kuto - acknowledge makosa na udhaifu wetu....

Akitokea mtu BOLD wa kusimama na kusema UKWELI wake au wa jambo fulani au juu ya mtu fulani, tunamshambulia na kumwita mtukanaji...!!

Kwa ujinga huu huu wa kibinadamu ilifika mahali, watu eti wakataka kumtangaza Nyerere -binadamu aliye sawa na wewe na mimi kama "mtakatifu fulani"....

Yaani binadamu amtangaze binadamu mwenzake, mtakatifu. Hii ni dhambi mbaya, hatari ya kukufuru...

Mungu aliona udhaifu huu huu enzi za Mussa kiongozi wa wana wa Israel kutoka nchi ya Misri kwenda Kanaani....

Wana wa Israel walimheshimu sana Mussa kwa sbb ya miujiza na matendo makuu aliyoyafanya ktk utukufu wa Mungu. Mungu yeye alimuona kama binadamu mwenye sifa za upungufu uleule wa binadamu wote...

Alipokufa, Mungu kwa makusudi kabisa na ili kuwaepusha kujiingiza ktk dhambi ya kuabudu " sanamu", alilificha kaburi lake mpaka leo maana kwa mioyo ya binadamu (wana wa Israel) wangeweza kuanza kuliabudu kaburi la Mussa na kumuacha Mungu wa kweli na wa haki, muumba na mwokozi wao....

Ndivyo ilivyo leo, kuwa, kuna watu wanaamini Mwl Julius K. Nyerere hakuwa binadamu wa kawaida. Hawa wanamtoa ktk level ya ubinadamu na wanataka kumpandisha level nyingine, yaa "uungu". Huku ni kuabudu "sanamu". Hili ni kosa na kufuru mbaya sana ktk sheria ya Mungu...

Generally, this is too bad...
 
Hata ukisikiliza hotuba za viongozi wa CCM na serikali wanakubali hilo. Jafo jana tu kasema tokea Uhuru mpaka 2015 kulikuwa na vituo vya afya 70 lakini kutoka 2015 -2020 vimejengwa 90 vya ziada. Kwa tafsiri fupi ni kuwa hata Nyerere hakufanya lolote la maana! Zaidi ya kudanganywa tu kama ndiye baba wa Taifa na mkombozi wetu.

Munapoipongeza pombe yenu inapokuwa ishawalevya mukasema ," tokea tulipopata uhuru.... haijawahi.kutokea blah blah blah. . " . Munamaanisha kuwa Nyerere naye alikuwa msanii tu. Na hata pombe yenu nayo hutamka maneno kama, "Nchi hii ilikuwa ni kama shamba la bibi ama ilikuwa ikiliwa tu"
 
Hata ukisikiliza hotuba za viongozi wa CCM na serikali wanakubali hilo. Jafo jana tu kasema tokea Uhuru mpaka 2015 kulikuwa na vituo vya afya 70 lakini kutoka 2015 -2020 vimejengwa 90 vya ziada. Kwa tafsiri fupi ni kuwa hata Nyerere hakufanya lolote la maana! Zaidi ya kudanganywa tu kama ndiye baba wa Taifa na mkombozi wetu.

Munapoipongeza pombe yenu inapokuwa ishawalevya mukasema ," tokea tulipopata uhuru.... haijawahi.kutokea blah blah blah. . " . Munamaanisha kuwa Nyerere naye alikuwa msanii tu. Na hata pombe yenu nayo hutamka maneno kama, "Nchi hii ilikuwa ni kama shamba la bibi ama ilikuwa ikiliwa tu"
Kutokuwa na akili nacho ni kipaji.
Wakati Nyerere anachukua uongozi wakati wa uhuru, population ya Tanganyika ilikuwa watu milioni tisa, leo kuna watu milioni 50.
Sasa nyie msio na akili mnafananisha miaka 60 iliyopita na leo 2020, mna akili ya kuwasaidia kweli?
 
Km Nyerere ni muongo mlikuwa wapi kumsema? Mbona wote ni wazee sana. Wengi walimkubali Africa na Dunia. Km aliweza kudanganya Dunia na ikakubali uongo wake basi ana uwezo, unaokaribia utakatifu.

Kudhiti na kulinda wazo la wengi siyo uzandiki ndiyo maana ya Siasa. Tundu Lissu ni dhaifu sana.Wajerman wanamtumia kurejesha Tanganyika yao! Hati za Tanganyika land bado ziko Vatican na hamzidai. Ila mnaona za muungano tu. Ambazo haziko Vatican. Wazo la kibeberu hili.l
 
Tundu lisu nilidhani ana akili kumbe jinga kabisa Blakoo tu. Analialia na kukimbiakimbia km demu, aje hapa afie hapa, Mandela hakumkimbia kaburu alijua atakufa tu na bora afe akipigana..mwanaume hukimbii mapambano. km Nyerere alivofanya ha kumkimbia mkoloni alimkabili pamoja na kuwa na kundi kubwa lenye maarifa kumzidi ila alisimama imara. Mleta mada ulitaka uongozwe na nani zaidi ya Nyerere? Jinga kabisa nitatspika bure Iwapo hata umonita tu haukuupata?
 
Wapiga kura wanaangalia vitu vingi na kikubwa ni uzalendo wa mgombea.

Kwa upande wa urais CHADEMA kuna Lazaro Nyalandu na Tundu Lissu wakati ACT - Wazalendo kuna Benard Membe.
Sisi tunawaheshimu wagombea wetu wote.

Ila ni lazima tuchukue tahadhari dhidi ya Tundu Lissu kwa sababu aliwahi kumsimanga kipenzi cha watanzania, baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(RIP) kwenye bunge la katiba kwamba alikuwa akiishi kwa uongo.

Kiukweli Tundu Lissu alitukosea sana watanzania na hachaguliki labda atoke hadharani na kutuomba radhi.

Nawatakia Jumatatu yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwani kuwa mzalendo ni lazima uwe mnafiki? Tatizo lenu mnatakakusikia mambo yanayowafurahisha nyie pekee.

Dunia ya sasa imeshabadilika
 
ACHA WOGA MKUU! LISSU NDIO RAIS

CHADEMA ipo kwenye mioyo ya watz wkt ccm ipo kwenye mioyo ya polisi na tume ya uchaguzi.....
Ndio maana ccm wanaogopa time huru, wanaogopa katiba ya wananchi, hawataki chadema wafanye siasa, lkn wanaogopa hata uchaguzi wenyewe maana wanajua hapa tulipo hakuna mkulima, mfanyakazi, mfanyabiashara au mwanafunzi anaweza kuipigia kura ccm.....

Wanahofu sn jamaa
 
Wapiga kura wanaangalia vitu vingi na kikubwa ni uzalendo wa mgombea.

Kwa upande wa urais CHADEMA kuna Lazaro Nyalandu na Tundu Lisu wakati ACT wazalendo kuna Benard Membe.
Sisi tunawaheshimu wagombea wetu wote.

Ila ni lazima tuchukue tahadhari dhidi ya Tundu Lissu kwa sababu aliwahi kumsimanga kipenzi cha watanzania, baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(RIP) kwenye bunge la katiba kwamba alikuwa akiishi kwa uongo.

Kiukweli Tundu Lissu alitukosea sana watanzania na hachaguliki labda atoke hadharani na kutuomba radhi.

Nawatakia Jumatatu yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!

Inakuhusu vipi wakati hata akiwa nani hutampigia kura? Aidha, kwa vile adhma yako ni mgombea wako ashinde kwa namna yeyote bila shaka ungependa wapinzani wako waweke mtu ambae atatoa ushindani dhaifu.

Waachien wenye vyama vyao wafanye uamuzi wao kama nyie mlivyofanya.

Amandla...
 
Back
Top Bottom