Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Ndio keshaibadili sasa! Mie mwenyewe sikuwahi kuhisi udikteta wa mwalimu, ila jana nimejua nini mwalimu alicho fanya. Hadi TBC wakafanya Yao.
 
Tundu Lissu, kwenye ili la kumponda Nyerere, pro-Chadema wapo kimya masikini.

kakudanganya nani? Zanzbr wanajua haya yote yaliyosemwa na Lissu ndo maana wapo tayari kukacha hii kitu kiini macho iliyopewa jina muungano! haya maneno ya Lissu ni mageni kwa WaDANGANYIKA TU.
 
Last edited by a moderator:
hao waheshimiwa wanapoteza muda wetu wananchi.
Hata kama ndoa haikufungwa kanisani au msikitini, mtoto
aliezaliwa ametimiza miaka 50 mnauliza leo hati ya ndoa
iko wapi.
 
Lissu aendelee kupiga misumari hata kwa waasisi wa taifa hili lakini atumie lugha staha kwa wazee wetu hawa waliofanya mengi kwa taifa hili.
 
Siyo kweli umeamua kutuwekea maneno kwenye midomoni mwetu.

Kwa kukusaidia tu ufahamu Waislam hawapo chini ya Bakwata.

Bakwata iliundwa na Nyerere kwa kazi maalum.

Ona sasa, wakati wa Sheikh Hemed Bin Jumaa Bin Hemed Bakwata yake ilikuwa sio iliyoundwa na Nyerere, au hamkujua kuwa waislam wote hawako chini ya Bakwata hadi mtu wa Shinyanga alipochaguliwa kwa haki kuiongoza?

Bibi yako Faiza Foxy ndio ameenda mbali zaidi kwa kuweka dharau kuwa Mh Sitta hajakutana na kiongozi wa Waislam, anadai Sitta alikutana na Pengo peke yake, kukutana na Sheikh Simba ni sawa na kutokutana na mtu. Acheni dharau zenu nyie watu wa pwani. Ni sawa na mzee wenu mwingine Mohamed Said anayedai kuwa uhuru wa Tanganyika uliletwa na kikundi fulani cha ma Alwatan wa pale Kariakoo,,, watu wa pwani mnajiskia sana nyie...
 
Lissu aendelee kupiga misumari hata kwa waasisi wa taifa hili lakini atumie lugha staha kwa wazee wetu hawa waliofanya mengi kwa taifa hili.

Lissu hajatumia hiyo Lugha hapo, hebu pitia hotuba yake. Hili kombamwiko la CCM limeamua ku spin maneno ili Lissu aeleweke vibaya. Lissu ameongea facts tupu
 
Mimi huwa nadhani wanasheria ni watu wazuri sana katika uwanja wa siasa hasa ukiangalia kwa kutumia darubini katika siasa za nchi za magharibi utakuta kuwa, viongozi wengi wa nchi hizo ni wanasheria na wamefanikiwa/wanafanikiwa katika siasa zao.

Kama hoja yako ni kweli, kwa nini inakuwa tofauti kwa Mh. Tundu Lissu?.

Kila siku nakuambia wewe ni jinga kubwa lakini hujijui. Alichokisema Lissu kila mtu amekielewa isipokuwa wewe tu
 
Unaweza kutoa ushauri ukaona ni mzuri. Lakini wenye historia ya huyo mheshimiwa wangetusaidia kujua pengine tangu shule alikuaje. Je babake au mamake huwa anaongea naye vipi kwenye mazingira ya hoja tata za kifamilia ???
lissu aendelee kupiga misumari hata kwa waasisi wa taifa hili lakini atumie lugha staha kwa wazee wetu hawa waliofanya mengi kwa taifa hili.
 
hao waheshimiwa wanapoteza muda wetu wananchi.
Hata kama ndoa haikufungwa kanisani au msikitini, mtoto
aliezaliwa ametimiza miaka 50 mnauliza leo hati ya ndoa
iko wapi.
Off course kama unajitambua utauliza hati ya ndoa iliko ili ukifika wakati wa mirathi ijulikane kuwa ndoa ilikuwa halali. Nyie mmezoeshwa na CCM kuishi kwa ghilba ndio maana ukweli unapowekwa hadharani mnapaniki.

Mlisema serikali mbili ndio mpango wenu mzima, wenzenu wanawaonyesha kwa data kuwa serikali mbili ni ghilba. Mmeyataka wenyewe na sasa mmevuliwa nguo mnapaniki
 
Nyerere si mungu, naye alisema mwenyewe kuwa alikosea mara nyingi. Tumechoka kuishi kiuongo uongo.

Mkuu hii ndio tabu kubwa sana ya Watanzania...tumeaminishwa kupenda kuishi kiungo uongo na kiwizi wizi sana. Mahali tulipofika sasa ni lazima ukweli usemwe no matter what.!! Big up sana Lissu
 
Mimi nipotoshe ili inisaidie nini?. Mh. Tundu Lissu alianisha mambo manne katika muktadha wa makundi ndani ya CCM na kila jambo lilikuwa na kundi lake. Jambo la nne lilikuwa linamhusu Mwl. Nyerere na siasa za Zanzibar kama nilivyobainisha hapo juu. Jaribu kuangalia video yake ili upate ukweli na kubainisha vizuri ninachokisema.
hoja ni kwamba aliyeongea kweli ni JKN au Tl basi! mengine ni ya kusherehesha ili kutengeneza miungu! Kumbuka ukweli mara zote humuweka Mkweli Huru!
 
siku zote Tundu Lisu ni mlopokaji na asieweza kudhibiti hisia zake anaposhangiliwa anaondoa kabisa hadhi ya upinzani nchini. Na hili ndio tatiizo la upinzani, hawa jamaa hawana uzalendo, heshma wala miiko.
 
Lissu hajatumia hiyo Lugha hapo, hebu pitia hotuba yake. Hili kombamwiko la CCM limeamua ku spin maneno ili Lissu aeleweke vibaya. Lissu ameongea facts tupu

Lissu ni mkweli kusema Nyerere ni Dikteta, muongo wala hajakosea.
 
Pro CHADEMA ni kama Bendera na upepo. kifupi wapowapo tu.
jana wamemsifia samuel sita eti ni kiongozi mwenye ueledi mkubwa sana,kisa amesema lisu atamalizia jumatatu kuuza nyago TBC.
 
Wewe tokea Jamaa yako awe Mbunge wa Mahakama umekuwa hovyo kabisa na inaonesha umepatwa na msongo wa mawazo kabisa.
Wewe ni mfano wa watu ambao wanatenda based on interpretation ya akili za watu wengine.
Ahsante sana! Mkuu umepiga ikulu...huyo jamaa THE BOSS ni mpambe wa MM aka mbunge wa mahakama.
Yaani anafikiri na kudhani kuwa watu hawamsomi between the line.
 
Ona sasa, wakati wa Sheikh Hemed Bin Jumaa Bin Hemed Bakwata yake ilikuwa sio iliyoundwa na Nyerere, au hamkujua kuwa waislam wote hawako chini ya Bakwata hadi mtu wa Shinyanga alipochaguliwa kwa haki kuiongoza?

Bibi yako Faiza Foxy ndio ameenda mbali zaidi kwa kuweka dharau kuwa Mh Sitta hajakutana na kiongozi wa Waislam, anadai Sitta alikutana na Pengo peke yake, kukutana na Sheikh Simba ni sawa na kutokutana na mtu. Acheni dharau zenu nyie watu wa pwani. Ni sawa na mzee wenu mwingine Mohamed Said anayedai kuwa uhuru wa Tanganyika uliletwa na kikundi fulani cha ma Alwatan wa pale Kariakoo,,, watu wa pwani mnajiskia sana nyie...
hemed bin jumaa alikwenda kinyume na matakwa ya alieiunda bakwata,that is why hakuchukua round,alikufa.
 
Back
Top Bottom