1. Mwinyi na Mkapa ni vikaragosi vilivyowekwa na Nyerere na alikuwa akiviendesha kwa remote kutokea Bustiama na Msasani.
Kikwete, kathubutu kuanza mchakato wa kuibadili katiba na ndiyo maana unayaona yote hayo yanaibuka. Kikwete ni ngoma nzito.
2. Miak kumi kumi ni mfuno tu wa demokrasia. Nyerere alikaa miaka 24 na hakuna la maana alilofanya ukichanganya na vikaragosi vyake, Mwinyi na Mkapa unapata jumla ya uongozi wake miaka 44.
Utawala wa Kikwete ndio uliothubutu, kuipa uhai mpya nchi hii kwa kuanzisha huu mchakato wa kujipatia katiba mpya. Kikwete anastahili kila sifa kwa hili na mengine mengi tu.
3. Ndio yapo katika kuibuliwa ili yaachwe. Bila kuwa na katiba mpya utayaachaje?
Bila kuwachana na fikra za Nyerere tutabaki kuwa maskini wa kutupwa. Na njia ya pekee ya kuachana nayo ni kuyaainisha mabaya yake yote. Kwa sasa naona yanaanza kuwaingia, maana Uamsho na Wazanzibari wengine wengi na wengineo wa hapa bara walikuwa wakiyainisha haya, wengine tumeyaandika humuhumu JF. Mkatuona hatumpendi Nyerere mkatushambulia. Nakuuliza hivi, mtu uliyemuamini ukajuwa kuwa si muaminifu na ni muonngo, utaendelea kumuenzi?
Kwasababu umemsingle out kikwete tumjadili tuone amethubutu katika yepi. kipofu huitwa makengeza anapopendeka.
1. Hoja ya katiba mpya
Hii haimo katika sera za ccm, aliikurupukia akijuwa itamjenga na amekuja kushituka kwamba haikuwa alivyotegeme..
a) Tume aliyoiteuwa kukusanya maoni amekuwa mpinzani wa tume hiyo bila aibu tena hadharani asifahamu anapinga mawazo ya wanachi- huku siokuthubutu nikujikanyaga na hajielewi analenga nini maana anakana yaliyokusanywa nini lengo lake.....?
b) Kama kawaida ya ccm wote ukiwemo Faizafoxy, kama kikwete amethubutu
-kwanini yeye na ccm yake mnapinga mawazo ya watanzania bara na visiwani? kunakuthubutu au kukengeuka..
-kama amethubutu vipi asiwakemee ccm kubadili utaratibu wa haki ya mpiga kura ilikulinda umoja haki na demokrasia yampiga kura?
Je tukifikia bunge la katiba kujadili mambo yanayohusu imani hususani ukristu/uislam mfano mahakama ya kadhi
a) Wakristu wanalindajwe nakura ya wazi kujenga staha na kuaminiana? lazima upige ya wazi ukienda sirini wenzio na waumini wako watakuchukia tu watajuwa umewazunguuka.
b)Waislam wanalindajwe nakura ya wazi kujenga staha na kuaminiana? lazima upige ya wazi ukienda sirini wenzio na waumini wako watakuchukia tu watajuwa umewazunguuka.
c) unawezaje kuwa na kura mbili kwa jambo moja kwa wakati mmoja? huu nao ni uthubutu kwa kikwete?
2. Elimu
kwa miaka yote, chini ya kikwete Elimu imehujumiwa na kupoteza ubora wake maradufu, kama ukikusanya data nakuchura graph, elimu imeshuka vibaya tena exponentially.
-kwa mara ya kwanza Kikwete ame-register failure ya zaidi ya 80%
-Kwa mara ya kwanza kikwete chini ya kawambwa na aliyekuwa naibu waziri mulugu wamebadili daraja la zero kuwa div-five hii niabu kubwa kuwa nakiongozi anayeendekeza siasa kwenye utiwa mgongo wa taifa lolote.
-Kwa mara ya kwanza tanzania imegeuka kituko na aibu kwa watanzania kushindwa kupandisha hadhi za walimu eti serikali haina fedha lakini fedha za yeye kuruka hewani kama popo tena mfululizo zipo
Sawa unapokuwa nakiongozi anayethubutu katika kuangamiza taifa ukamuona anafaa huo nao ni ujinga wa aina yake.
3. ufisadi, mali asili na utalii
-Majina ya majangili ninayo (kikwete) lakini amethubutu bila aibu kukaa kimya bila hatua zozote
-Kwa mara ya kwanza chini ya utawal;a wa kikwete twiga, swala nk wamesafilishwa hadharani kwa kutumia ndege ya jeshi la nchi nyengine, hii ni aibu ya aina yake hapa pia amethubutu kuhakikisha waarabu wanapata mifugo yetu ya asili bila idhini ya wamasai wala watanzania
4. Madawa ya kulevya
Kikwete amethubutu kukalia majina ya wauza dawa za kulevya maana, kama kawaida yake aliwaasa wajisalimishe kilichotokea nisiri yake yeye na mama salma
-Nikatika utawala wa kikwete Uvutaji na utumiaji wa madawa ya kulevya umeshika kasi tanzania, sababu zake niuthubutu wake kuwanyamazia wafanyabiashara hiyo, raia na watoto wa tanzania wakiteketea.....
5.Ukosefu wa fedha na misamaha kwa wezi
Kikwete ndiye rais wakwanza aliyethubutu kuwasamehe wezi wa fedha za umma na kuwaambia warudishe na huo ni upepo mbaya utapita, wezi wa kuku .a karanga wanafungwa....
6. Afya na matibabu
nikatika utawala wa huyu kikwete nidham na weledi wa huduma bora za afya umetoweka kabisa, amethubutu kuibadili muhimbili kuwa gofu la kufia maskini raia wa Tanzania wasio na uwezo huku yeye na wote wenye uwezo wakikimbilia India, Germany na kwingineko, cha ajabu wenzetu kenya wanaimarika kwa kila nyanja.
Heshima ya Muhimbili wakati ule na hospitali za Rufaa sehem mbalimbali nchi ilikuwa juu sana lakini pia imefifia kabisa na kukosa hadhi chini ya huyu msubutu wa ccm ya sasa kikwete
Hivi unaposema kikwete amethubutu kwa kivipi hasa?
Faizafoxy
-mpaka leo bado unalalama kuhusu bakwata-Mbona huyu mzee wa kuthubutu hajafanya mabadiliko yayosababishwa na mapungufu ya nyerere???
-Mpaka leo bado unapiga kelele na serikali mbili na michakatuo ya uhuru na madaraka kamili ya Zanzibar, mbona huyu kikwete wakuthubutu asilekebishe makosa ya nyerere?
-Bila aibu alisimama kwenye bunge la katiba akitetea serikali mbili badala ya mabadiliko, uthubutu wake uko wapi?
-Kama kikwete amethubutu, kwanini asikae kimya aache maoni ya wanachi yajadiliwe badala yake bila aibu anaiponda tume aliyoiunda na kuzifinyanga taarifa na maoni ya wanachi?
Huyu alievunja rekodi ya kusafiri duniani kwa maraisi hathubutu bali nimtafuta sifa kwa mambo asiyoyaweza .
