Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Kigeni hapo ni labda...yakua hayo maneno yamesemwa hadharani na huyo Mbunge "muadilifu" wa "sera za Chadema"!?
Alhaji, aina maana it is convincing, au tusubiri kesho atufafanulie zaidi umuhimu wa hati maana argument yake imekatikia kwenye UN kutaka hati zifikishwe hili Tanzania ipate usajili, sasa ikawaje tukapata usajili kama hati ndio kila kitu umoja wa taifa na kama hati hiyo ndio njia halali ya kuvunja muungano? Mwisho wa siku hati hiyo raia waliofanya maamuzi yao kwa uelewa wa muungano walio uziwa hata kama kwa mkataba wa muda inawalinda vipi kwa sasa hapo ndio kunaishia sio Jumbe aliochosema au alichopendekeza. Unaweza kuona kwanini akachukuliwa kama mhaini wa taifa.
 
Mwanasheria Mkuu Wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, ambae yupo kwenye bunge maalum Dodoma, alisema kujificha kwa Tanganyika kwenye Serikali ya Muungano, ni fitna kubwa inayoudhoofisha Muungano.

“Uruhani wa Tanganyika ndiyo fitna kubwa ya Muungano, Mzee Jumbe (Aboud Jumbe Mwinyi, Rais wa Pili wa Zanzibar) alitaka kuja na hirizi ya huyu ruhani akamchukue na akamzike.”

“Kwa bahati mbaya alidhalilishwa mbele za watu kwa kuambiwa eti hajui hesabu moja na moja anasema tatu. Hivi kweli Mzee Jumbe msomi mzima hajui hesabu? Huu uruhani wa Tanganyika ndiyo fitna kubwa ya Muungano, ipo haipo. Lakini akipanda kichwani anasema nipo, sasa inataka kutumia jina letu la pamoja.”

Othman alikumbusha mkasa uliomtokezea Mzee Jumbe ambaye mwaka 1984, akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, aliandaa waraka wa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kutaka mfumo wa serikali tatu kwa kutokana na kile alichoamini kuwa “moja na moja ni tatu.” Alimaanisha serikali ya Zanzibar iliyopo wazi, serikali ya Muungano iliyopo wazi na serikali ya Tanganyika iliyojificha.

Soma zaidi: FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI

Waraka huo ulinaswa na mashushushu waliokuwa Ikulu ya Zanzibar kabla hajaondoka kwenda mkutanoni Dodoma, na hatimaye akalazimishwa na Mwalimu Julius Nyerere kujiuzulu.

Duuh! Teeeh! Teeh! Teeeh!

Yamekua haya tena...yaani leo Watanganyika wanaitwa maruhani!? Daah!

Lakini haya matusi na tashtit zoote katuanzishia na katuletea yule Nyerere! Daah! Inasikitisha!

Shukran Mkuu FaizaFoxy kwa hizi bayana murua!
 
Alhaji, aina maana it is convincing, au tusubiri kesho atufafanulie zaidi umuhimu wa hati maana argument yake imekatikia kwenye UN kutaka hati zifikishwe hili Tanzania ipate usajili, sasa ikawaje tukapata usajili kama hati ndio kila kitu umoja wa taifa na kama hati hiyo ndio njia halali ya kuvunja muungano? Mwisho wa siku hati hiyo raia waliofanya maamuzi yao kwa uelewa wa muungano walio uziwa hata kama kwa mkataba wa muda inawalinda vipi kwa sasa hapo ndio kunaishia sio Jumbe aliochosema au alichopendekeza. Unaweza kuona kwanini akachukuliwa kama mhaini wa taifa.

Duuh! Hicho cheo cha Alhaj mie sijafikia Dadangu...lakini nashukuru for such a beautiful compliment!

Kwa kifupi,haya masuala mie binafsi nayafuatilia kiundani mno tangia early 80's! Ndo maana pia si mshabiki nayo mno kwa hivi sasa!

Yaani nakhis bado ni political acrobats...na wenye kuyumba kifikra na labda pia kimaendeleo ni Wananchi walio wengi huko Vijijini!

Kwa hiyo nakubaliana na hoja yako ya awali, kwa kiasi fulani...yakua ukitazama kiundani/kwa mapana...hakuna jambo jipya mno aliloongea yule Tundu Lissu...na hata hii tathmini nzima ya muundo wa Muungano,nalo pia si jambo geni kwa wasikizaji na wafuatiliaji wa haya majambo!?

Kama usemavyo...labda tutege tena masikio kujua hiyo kesho,atasemani!?

Ahsanta sana.
 
Mkuu gombesugu

Mimi nipo huku Karatu sina habari zozote haya ebu nipe hizo bayana kuna jipya gani huko kutoka kwa Lissu.
 
Last edited by a moderator:
Nimechukua mda kuijibu thread hii,
Maana nlkuwa naisoma halafu narudi kusoma hotuba ya Lissu.
Baada ya kuisoma hotuba nzima ya Lissu tena na tena....
Nashangaa ni vipi hoja zote zile zijibiwe na upuuzi kama huu wa mleta Maada.
Lissu ameweka fact, ambazo nyingi kwa kipindi kile zilikuwa ni "siri kuu za nchi" not for public consumption,
leo tupo kwenye zama za pazia la hekalu kupasuka,
ya chumbani kuja sebuleni.
Hii ni nchi yetu, tunaifuma upya kuelekea karne nyingine,
ni lazima kila kitu kije upya sababu zote ziwe challenged hadharani na majibu sahihi yapatikane hyo ndio amani yetu na huo ndio utakuwa mustakabali wetu mpya na muafaka wa kitaifa.
Hizi porojo za kitoto na siasa za kipuuzi eti oh sijui katukana, hamna tusi pale ila its just ukweli umekaa uchi unatuangalia,
shurti kama taifa tuukabili na tuukumbatie nao utaliponya hili taifa.
Nje ya hapo ni kutaka kuendelea na mchezo wa kuuzunguka mbuyu.
Kuukubali ukweli huu wengine kwetu hakuondoi heshima ya Mwalimu Nyerere ila kunatutamanisha kumjua zaidi na kuielewa ndoto yake hasa maana mpaka sasa hata hawa watawala na "vijana" wake wamedhihirisha walikuwa hawajui kitu kuhusu ndoto ya Mzee
 
Yamekuwa hayo tena, haya kesho maalim (au huko pia bado)

umeona tatizo la wasiotaka kukubalia uhalali wa muungano kidogo tu wakiambiwa hiki hata kisicho na tija tayari munkeri wakati amna la msingi linaloongelewa mara nyingi.

Sidhani ata kama kesho kutakuwa na jipya. Jipya ni wananchi kudai kura ya maoni pekee, so far ni jambo linalo wafurahisha viongozi tu kuliongela na kulipa kipaumbele sanasana wa upinzani waliokosa hoja za kimaendeleo.
 
Mkuu gombesugu

Mimi nipo huku Karatu sina habari zozote haya ebu nipe hizo bayana kuna jipya gani huko kutoka kwa Lissu.

Duuh! Hilo si ndo jimbo la yule Daktari wa Theology ya Kikatoliki aka Baba Junior,au!?

Mkuu kwa kifupi, Muheshimiwa Tundu Lissu kwa niaba ya Edwin Mtei na Chadema woote...ameamua kumwaga ugali na kutoboa sufuria!? Daah! Teeeh! Teeeh! Teeeh!

Yaani amemvua nguo Baba wa Taifa, hata huko kaburini alipo! Daah! Chadema bana!

Nyerere alikua ni muongo,mnafiki,mchafuzi wa mazingira ya kisiasa,mzandiki na msaliti wa Tanganyika! - By Tundu Lissu Chadema MP and Political Strategist!

Ahsanta.
 
Last edited by a moderator:
Nimechukua mda kuijibu thread hii,
Maana nlkuwa naisoma halafu narudi kusoma hotuba ya Lissu.
Baada ya kuisoma hotuba nzima ya Lissu tena na tena....
Nashangaa ni vipi hoja zote zile zijibiwe na upuuzi kama huu wa mleta Maada.
Lissu ameweka fact, ambazo nyingi kwa kipindi kile zilikuwa ni "siri kuu za nchi" not for public consumption,
leo tupo kwenye zama za pazia la hekalu kupasuka,
ya chumbani kuja sebuleni.
Hii ni nchi yetu, tunaifuma upya kuelekea karne nyingine,
ni lazima kila kitu kije upya sababu zote ziwe challenged hadharani na majibu sahihi yapatikane hyo ndio amani yetu na huo ndio utakuwa mustakabali wetu mpya na muafaka wa kitaifa.
Hizi porojo za kitoto na siasa za kipuuzi eti oh sijui katukana, hamna tusi pale ila its just ukweli umekaa uchi unatuangalia,
shurti kama taifa tuukabili na tuukumbatie nao utaliponya hili taifa.
Nje ya hapo ni kutaka kuendelea na mchezo wa kuuzunguka mbuyu.
Kuukubali ukweli huu wengine kwetu hakuondoi heshima ya Mwalimu Nyerere ila kunatutamanisha kumjua zaidi na kuielewa ndoto yake hasa maana mpaka sasa hata hawa watawala na "vijana" wake wamedhihirisha walikuwa hawajui kitu kuhusu ndoto ya Mzee
Kwanza niseme hakuna sehemu nimesema Mh. Tundu Lissu ametukana.

Pili, naomba tukubaliane kuwa tusi ni relative term. Kila unachikiona ni tusi mwingine anaweza akaona ni salamu!.

Uwongo na udanganyifu ni mambo ambayo yanaeleweka na hayana tafsiri kifikra na kiuhalisia kulingana na sehemu au mahali popote.

Mh. Tundu Lissu anaposema, Mwl. Nyerere alidanga inaeleweka uwongo ni nini. Mh. Lissu anaposema, Mwl. Nyerere ni mdanganyifu inaeleweka udanganyifu ni nini.

Inawezekana hii comment haikunihusu kwa sababu niliyoyasema ni tofauti sana na unachodai nimekisema.
 
Habari yako ina chumvi sana, nilimsikiliza mwanzo hadi mwisho
 
Yamekuwa hayo tena, haya kesho maalim (au huko pia bado)

umeona tatizo la wasiotaka kukubalia uhalali wa muungano kidogo tu wakiambiwa hiki hata kisicho na tija tayari munkeri wakati amna la msingi linaloongelewa mara nyingi.

Sidhani ata kama kesho kutakuwa na jipya. Jipya ni wananchi kudai kura ya maoni pekee, so far ni jambo linalo wafurahisha viongozi tu kuliongela na kulipa kipaumbele sanasana wa upinzani waliokosa hoja za kimaendeleo.

Mkuu nimekusoma!

Haya ndo matatizo ya vyama fake vya upinzani...yaani hawa Viongozi wachache wa Chadema wanatumja siasa za kumchafua Baba wa Taifa kwa manufaa ya matumbo yao!? Daah!

Yaani inasikitisha mno kuona yakua...hao Viongozi/Wanasiasa takriban woote wa upinzani...wanatumia udhaifu wa fikra mgando za sisi Watanzania wengi wa hali ya chini,khasa tuliopo huku Vijijini kama ndo mtaji wao wa kibiashara,na kujinufaisha kibinafsi!? Daah!

Nastaajab,baadhi ya vyama vya kisiasa/kibiashara...yaani mpaka leo wameshindwa kuwasilisha hata mwenendo/uhalali wa matumizi yao ndani ya vyama vyao kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali...kama kanuni za Msajili wa Vyama inavyotaka!¿

Hao Chadema kwa mfano...mpaka leo wameshindwa hata kufanza uchaguzi wa ndani ya chama chao kwenye nafasi za juu za uongozi!¿ Daah¡

Na kila Mwanachadema mwenye kuhoji hayo...basi ati inaamrishwa na uongozi wa juu wa Chadema...yakua apigwe vitofali,kufukuzwa chama,kuchafuliwa kisiasa...au hayo yoote kwa pamoja!? Daah!

Shukran Mkuu...mie hapa kijijini ndo najitayarisha kuzima kibatari changu! Alamsik!

Ahsanta.
 
Habari yako ina chumvi sana, nilimsikiliza mwanzo hadi mwisho

Embu tufahamishe weye jinsi huyo Tundu Lissu alivyosema/alivyodai!?

Hiyo chumvi unayodai imewekwa na Bwana mleta mada...ni ipi hiyo!? Embu tudadavulie kwa hoja na vipengele unavyo-dispute!?

Kama vipi,kwanini na wewe usifungue thread yako nyangine kuonyesha hizo "facts" zako...nasi Wasomaji/Wachangiaji pia tutakuja huko...badala ya kuendelea kumbughudhi mleta mada,au!?

Mjumbe hauwawi...kama "kosa" basi ni la Tundu Lissu kwa kusema kweli na kuivua nguo maiti ya Baba wa Taifa!?

Tatizo la Tundu Lissu...hata kama alosema takriban yoote ni kweli...but,his approach n the way he articulated the whole issue,that's the problem I think!?
 
The excerpt Tundu Lissu used (kuhusu Nyerere na msimamo wake juu ya Zanzibar) comes from an article Nyerere wrote to explain why Tanzania recognised Biafra. Hayakuwa ni mahojiano na Nyerere na gazeti hilo kama Lissu alivyosema. But that's besides the point. What is important here is to understand the full context in which Nyerere wrote the article and why he articulated the position he did on Zanzibar in relation to Biafra. The article, "Why We Recognised Biafra," was published in The Observer, London, 28 April 1968. It was reprinted, in its entirety, in Godfrey Mwakikagile, Nyerere and Africa: End of an Era, pp. 277 - 279:

"Leaders of Tanzania have probably talked more about the need for African unity than those of any other country. Giving formal recognition to even greater disunity in Africa was therefore a very difficult decision to make. Our reluctance to do so was compounded by our understanding of the problems of unity - of which we have some experience - and of the problems of Nigeria. For we have had very good relations with the Federation of Nigeria, even to the extent that when we needed help from Africa we asked it of the Federation.

But unity can only be based on the general consent of the people involved. The people must feel that this state, or this nation, is theirs; and they must be willing to have their quarrels in that context. Once a large number of the people of any such political unit stop believing that the state is theirs, and that the government is their instrument, then the unit is no longer viable. It will not receive the loyalty of its citizens.

For the citizen's duty to serve, and if necessary to die for, his country stems from the fact that it is his and that its government is the instrument of himself and his fellow citizens. The duty stems, in other words, from the common denominator of accepted statehood, and from the state government's responsibility to protect all the citizens and serve them all. For states, and governments, exist for men and for the service of man. They exist for the citizens' protection, their welfare, and the future well-being of their children. There is no other justification for states and governments except man.

In Nigeria this consciousness of a common citizenship was destroyed by the events of 1966, and in particular by the pogroms in which 30,000 Eastern Nigerians were murdered, many more injured, and about two million forced to flee from the North of their country. It is these pogroms, and the apparent inability or unwillingness of the authorities to protect the victims, which underlies the Easterners' conviction that they have been rejected by other Nigerians and abandoned by the Federal Government.

Whether the Easterners are correct in their belief that they have been rejected is a matter for argument. But they do have this belief. And if they are wrong, they have to be convinced that they are wrong. They will not convinced by being shot. Nor will their acceptance as part of the Federation be demonstrated by the use of Federal power to bomb schools and hospitals in the areas to which people have fled from persecution.

In Britain, in 1950, the Stone of Scone was stolen from Westminster Abbey by Scottish Nationalists while I was still a student at Edinburgh. That act did not represent a wish by the majority of the Scottish people to govern themselves. But if, for some peculiar reason, that vast majority of the Scottish people decided that Scotland should secede from the United Kingdom, would the Government in London order the bombing of Edinburgh, and in pursuing the Scots into the Highlands, kill the civilians they overtook? Certainly the Union Government would not do this; it would argue with the Scots, and try to reach some compromise.

As President of Tanzania it is my duty to safeguard the integrity of the United Republic. But if the mass of the people of Zanzibar should, without external manipulation, and for some reason of their own, decide that the Union was prejudicial to their existence, I could not advocate bombing them into submission. To do so would not be to defend the Union. The Union would have ceased to exist when the consent of its constituent members was withdrawn. I would certainly be one of those working hard to prevent secession, or to reduce its disintegrating effects. But I could not support a war on the people whom I have sworn to serve - especially not if the secession is preceded by a rejection of Zanzibaris by Tanganyikans.

Similarly, if we had succeeded in the 1963 attempt to form an East African Federation, or if we should do so in the future, Tanzania would be overjoyed. But if at some time thereafter the vast majority of the people of any one of the countries should decide - and persist in a decision - to withdraw from the Federation, the other two countries could not wage war against the people who wished to secede. Such a decision would mark a failure by the Federation. That would be tragic; but it would not justify mass killings.

The Biafrans now feel that they cannot live under conditions of personal security in the present Nigerian Federation. As they were unable to achieve an agreement on a new form of association, they have therefore claimed the right to govern themselves. The Biafrans are not claiming the right to govern anyone else. They have not said that they must govern the Federation as the only way of protecting themselves. They have simply withdrawn their consent to the system under which they used to be governed.

Biafra is not now operating under the control of a democratic government, any more than Nigeria is. But the mass support for the establishment and defence of Biafra is obvious. This is not a case of a few leaders declaring secession for their own private glory. Indeed, by the Aburi Agreement the leaders of Biafra showed a greater reluctance to give up hope of some form of unity with Nigeria than the masses possessed. But the agreement was not implemented.

Tanzania would still like to see some form of co-operation or unity between all the peoples of Nigeria and Biafra. But whether this happens, to what extent, and in what fields, can only be decided by agreement among all the peoples involved. It is not for Tanzania to say.

We in this country believe that unity is vital for the future of Africa. But it must be a unity which serves the people, and which is freely determined upon by the people.

For 10 months we have accepted the Federal Government's legal right to our support in a ‘police action to defend the integrity of the State.' On that basis we have watched a civil war result in the death of about 100,000 people, and the employment of mercenaries by both sides. We have watched the Federal Government reject the advice of Africa to talk instead of demanding surrender before talks could begin. Everything combined gradually to force us to the conclusion that Nigerian unity did not exist.

Tanzania deeply regrets that the will for unity in Nigeria has been destroyed over the past two years. But we are convinced that Nigerian unity cannot be maintained by force any more than unity in East Africa could be created by one state conquering another.

It seemed to us that by refusing to recognise the existence of Biafra we were tacitly supporting a war against the people of Eastern Nigeria - and a war conducted in the name of unity. We could not continue doing this any longer."
 
Nyerere alikuwa dicteta period na hakuna wa kumtetea kaua na kuweka watu wengi vizuizini mpaka leo na wengine hawajulikani hata makaburi yao yalipo

Mh. Tundu Lissu yeye amesimama kwenye hoja kwa jinsi anavyomuona Mwl. Nyerere katika siasa zake za kigeugeu.

Kama kuna watu wanafuata watu, well, Tundu Lissu atakuwa amewachanganya kwa sababu hawasimami kwenye nguzo ya hoja.
 
Tundu Lissu ni smart lawyer na very good mwanaharakati but he is a lousy politician....huwezi mtukana Nyerere na isi ku cost

Nimemsikia Lissu akinukuu aliyosema Nyerere kupitia lile gazeti la uingereza, na pia kupitia kitabu chake na vyote kuhusu jambo moja. Swali ni je ni kweli (moyoni mwake) kwamba alimaanisha alichokuwa anakisema kama Wazanzibar hawataki muungano hatawagusa?? Ni kwa nini Jumbe (tena rais!!) alifukuzwa na kuwekwa kizuizini? Mbona G55 hawakufukuzwa?? Je kama mambo yanavyokwenda sasa ikatokea kwamba mfumo wa serikali 3 ukapita kama walivyopendekeza akina Jumbe nani atalipa machungu na fedheha aliyopata Jumbe?? Nini hasa misingi na kauli thabiti za viongozi ambao wameaminiwa na wanaowaongoza??
 
Mkuu,

Yaani umezungumza kwa uchache mno...lakini hoja zako na masuali yako yana mantik kubwa mno,na pia yanafikirisha!?

Inabidi Taifa liwe na watu wengi wa sampuli yako na Mkuu Ng'wamapalala...ili tuzidi kuelimishana na kuondokana na ile nidhamu ya woga alotufundisha na kutwachia yule Nyerere....as part of his bigger indoctrination plan/system!? Daah!

Ahsanta.
 
Sidhani kama kwa sasa kunasababu ya kumuita Mwl. J.K. Nyerere majina yoote hayo, cha muhimu kuzingatia the country was given to him for the first time (zngatia ugumu wa kazi 4the 1st time), kwa malengo nisioyajua akaamua kufanya wanacho kiita muungano (yeye na karume na mashaidi na mawakili nawengine wengi). BUNGE LA KATIBA LIJADILI KWA VIGEZO NA MISINGI NA UMAKINI HIYO KATIBA MPYA NA SIO UTENDAJI KAZI WA NYERERE (THERE TIME HAS PASSED OUT IT IS OURS NOW) JUZI TU WAMEOMBA KUONGEZEWA MUDA THEN WANAPGA BLA BLA TUU
 
Nyerere alikuwa binadamu kwa sehemu mjanja,kwa sehemu mbabe,kwa sehemu muumini wa ukristo kwa sehemu nyingine mshirikina-angalia mwenge na kadhia hizo.sasa kama hati ya muungano haipo un wala ikulu ya znz wala magogoni,tukisema huyu mzee alikuwa tapeli ila tu alikuwa si hatari kama hawa aliowaachia nchi,hatujatukana.mazuri anayotenda mtu anakwenda nayo kaburini,yale maovu yanabaki yakinuka na kumsuta!tunapoishi tuwe makini lissu huna kosa kweli itatuweka huru! Tusijetetea muungano kama ndege kasuku wakati hauna uhalali kisheria!
 
Gombesugu,kuna wengi walipoteza maisha kwenye utawala wa mkono wa chuma wa awamu ya kwanza,unayefikiri kavuliwa nguo ujue kasamehewa tu ana damu nyingi zisizo na hatia kichwani mwake!mwombee rehema za mungu huko aliko!na wewe usifanye aliyoyafanya hata kwa familia,ni uovu unaonuka!
 
Mkuu, mbona unatukia ghadhabu dhidi ya ndugu yetu mleta mada hapa jamvini!¿ Daah¡
hakuna ghadhabu hapa gombesugu dhidi ya mleta mada, sasa mtu anakuja anasema Tundu Lissu ni debe tupu bila ya uthibitisho wakati yeye Lissu anaongea kwa vithibitisho na haya yote anasababisha mleta mada kwa lengo lake hilo hilo ambalo watu wanaanza kutukana mtu bila ya hoja eti kisa amesoma title tu ya huyu mleta mada
Kama "kosa" la kusema ukweli juu ya yule Julius Nyerere...basi mlaumu yule MP wa Chadema Bwana Tundu Lissu!
Sasa nimlaumu vipi Tundu Lissu wakati alieleweka vizuri halafu alikuwa haropoki, tunaweza tukawa tunajadili kumbe hatuelewani tuna jadili kitu gani, yamkini pia unaweza ukawa unadandia treni kwa mbele

Nyerere aliishi kwa urongo,unafiki,uzandiki,vitisho dhidi ya wenzie na kuwachafua kisiasa. Pia Nyerere alizoea vya kunyonga,ndo maana hakutamani vya kuchinja!? - By Tundu Lissu Chadema MP!
Dah! huu ni uongo sasa unaosema, umesikia wapi Tundu Lissu ametamka hayo maneno, ndio maana nakwambia mleta mada amewaingiza chaka na wewe kwa kuongozwa na chuki umeingia kingi yaani unacheza ngoma ambayo hauijui,wapi Tundu Lissu amesema Nyerere alizoea vya kunyonga ndo maana hakutamani vya kuchinja? eti FaizaFoxy unaweza kumsaidia nduguyo...
Wako wapi wale Chadema wafia Unyerere akina Mag3,Nguruvi3,Mwanakijiji na wafuasi wao/vilaza wenzi wao!? Daah!
Mbona hueleweki unataka kujenga hoja gani hapo!?
Weye mfia Unyerere wa kambi ya CCM aka Chama wa Gongo la Mboto uko wapi!?
cc chama
Mnaona sasa,mpaka Wabunge wenu wachovu,nao sasa wameanza kuamka na kupata Darsa za Mkuu FaizaFoxy...kukhusu unyama wa yule Dikteta Nyerere!? Daah!
acha uongo mkuu gombesugu yaani Tundu Lissu amepata darsa kutoka kwa FaizaFoxy nadhani hapo unatania tu, sidhani kama huko sawa, misimamo ya Tundu Lissu inajulikana toka zamani sasa iweje leo awe mchovu, kipindi fulani aliongea kuhusiana na Zanzibar kukiuka au kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizomewa na kutukanwa tu bila hata ya hoja na ma ccm pamoja na wabunge kutoka Zanzibar, lakini yeye huwa anasimamia ukweli kwa maana yeye hajazoea vya kunyonga kama watu wa ccm, au kusema hasioyatenda kama kina Mwakyembe huku anaaandika hivi kule anapinga alichokiandika yaani ni ujanja ujanja tu, sasa unatudanganya eti Tundu Lissu kapata nondo kutoka kwa FaizaFoxy nadhani hapo umeongozwa na hisia bila ya uhalisia wowote...
Kikwete...tafadhali kamwombe radhi Rais Mzee Aboud Jumbe, kwa niaba ya Watanzania soote wapenda ukweli;haki na amani!
Kwa hiyo hapo unamaanisha baada ya kumwomba radhi na yeye pia abadirishe misimamo yake? kwa hiyo inawezekana hata yeye mwenyewe alikuwa hajielewi mpaka nondo zilipotoka kwa Tundu Lissu!?
Ahsanta sana.
Ahsanta sana pia...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom