Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Jamaa kawapa mifano halisi bunge lite likatulia,anasema CCM kuwepo kwa katiba mpya Zanzibar ni kunyume kabisa,na kikwete cyo amiri jeshi Zanzibar.
 
Sikutegemea kwa mtu mzima Kama lisu kumtusi muasisi Wa taifa. Alitakiwa kujenga hoja,na kwa njia ta matusi. Tumesononeka sana sisi watanzania,kauli ya mtusi mwalimu haivumiliki. Ningekuwa mimi ndio mkono Wa dola, ningechukua hatua mathubuti. Si kila kitu kazima useme, pima tumia hâta busara ya kawaida. Tunamheshimu mwl na bado tunampenda. Amani unayoiona si kwa bahati mbaya. Karibu kujizuia kwa baadhi ya mambo. Huwezi hâta kidogo wewe lisu kujilinganisha na mwl. Linda heshima yako na chama chako. Kila kona wanasema umekosea. KAzi njema.
nyoo kama umemsikiliza kaongea nn sa hv bungen utajua kuwa jamaa ni geneouz
 
Mi nimefurahishwa na Lissu kuwa amewaambia ukweli hao wanafiki wanaojifanya kumuhenzi nyerere wakati si kweli, matendo yao na maneno yao ni tofauti sana, na wanasema pembeni kwenye vikao wanainama chini sipendi unafiki wala wanafiki, Nyerere ni binadamu kama watu wengine na yeye ana makosa yake, alipokosea tunasema tunarekebisha na kusonga mbele. Na ndio maana mkapa alikuwa anafanya bila kupiga makelele alikuwa namjua Nyerere vizuri na alifanya mengi tofauti na yeye.
 
hakusema nyerere kwa maana ya kuspecify jina kama ambavyo ww unasema alisema WALIO hakusema Nyerere xo acha kulete uongo humu
 
Sijawahi hata siju moja kusikia nchi yoyote duniani mfano cuba,china akijitokeza mtu yoyote kwa cheo chake kwa elimu yake au kwa pesa zake akimtukana mwasisi wa taifa lake.....
Namuheshimu sana lisu lakini kwa hilo la kumtukana Mwl JKN kakosea...na sipatii picha angekuwa mwenyekiti ni Makinda au ndugai lisu angetolewa nje ya bunge na kuchukuliwa hatua kali sana sema ni 6 mwoga lisu ana bahati sana....

Baba yangu lisu kuwa makini sana na maneno ya mdomoni mwako...

Tumia vizuri UBONGO wako, kusema mtu fulani alikosea unakuwa UMEMTUKANA.....??? LOH...!! ama kweli we ni MZIGO kwa TAIFA
 
Hali kadhalika hata mimi napingana na J.K.Nyerere kwa mengi sana. Zanzibar Inanyonywa sana na Tanzania. Iweje vya Zanzibar viwe vya wote na vya Tanzania ni vya watanzania pekee?. Tunataka mabadiliko jamani, Mtu asiyetaka mabadiliko huyo ni MHAFIDHINA, KWANINI HATUTAKI MABADILIKO? MFUMO ULIOKUWEPO UMESHINDWA kuleta EQUALITY NA JUSTICE hii ni dhahiri kwamba endapo kutakua hakuna Usawa katika rasilimali lazima mzozo uibuke. WANACCM WANAHOFU, NA NI WALAFI WA MADARAKA, NA NI DHAHIRI KUA NA WAHAFIDHINA! Je Ni mfumo Gani utakao Ondoa mzozo huu wa muungano? Ni Serekali tatu tu ndio Suluhu! NI Hitimishe kwa kusema Changes are Inevitable' also we need to be reluctant and not rigid just as CCM LEADERS!! CRIMEA ILILIA KUJITENGA IMEFANIKIWA, ZANZIBAR INALILIA NCHI YAO LAZIMA ICHUKUE NCHI YAKE!! NI Ayo Tu! End of discussion!!
 
LISSU ni zaidi ya watu smart hapa tz.Wale wanaosema Lissu amemtukana MWL.J.K hawajielewi tu either warudi darasani ndo msaada pekee.
 
Ndiyo tatizo la Viongozi wengi nchini kutumia kivuli cha Baba wa
Taifa kufanya yaliyomahovu,anapotokea muungwana mmoja na kusimama na kuongea ukweli na hasa akitokea CDM tunaambiwa katukana.
Tunaitaji mabadiliko haijalishi km unamaslahi ktk Serikali ya CCm.
 
Nenda kachukue buku7 lkn baada ya cku 2 utakumbuka aliyosema lisu niyakwel na ww unajua kabisa Mwl. alikuwa mbabe
 
Nimeshangazwa na mwanasiasa kijana mwenye taaluma ya uchumi Mwigulu Nchemba kutamka kuwa kuendesha serikali ya Shirikisho ni gharama kwa kuwa itatugharimu Shilingi Trilioni Tatu.Sasa kwa mujibu wa utafiti uliifanywa na wasomi katika mchango wao kwenye mjadala wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere walisema Tanzania hupoteza Takribani Trilioni 2.5 kila mwaka kutokana na uzembe wa kutokukusanya Kodi.Mwigulu Nchemba ni Naibu waziri wa Fedha.Anakwepa wajibu hapa.

Ndugu Zitto Kabwe,Mwanasiasa kijana mwenye Taaluma ya Uchumi alipokua kwenye Mkutano wa Hadhara kule Shelui alisema Serikali hupoteza takribani Shilingi Trilioni 1.5 kwenye sekta ya Madini pekee kwa Mwaka.

Tunaacha kutumia raslimali zetu lakini tunatafuta balaa la kisiasa kwa kutosikiliza matakwa ya wananchi.Tunatafuta political crisis kwa nguvu

Kama serikali Tatu ni gharama ,kwanini iwe serikali mbili na sio serikali Moja ?

Nanyi wabunge wa bunge la katiba jitahidini kuwajibu watu kama hawa instantly kwa Takwimu na Facts.Ndio dawa yao tu

Kuna hoja iliyonishangaza leo,Eti Kanisa Catholic linataka kumfanya Mwalimu Nyerere kuwa Mtakatifu kwa hiyo hastahili kukosolewa?

Yaani haistahili kusema ukweli kuwa Mwalimu Nyerere ali-issue Presidential Decree(Amri ya Rais) ili kuiua Tanganyika?Kwa kawaida Presidential Decree huwa issued na Madikteta na Wafalme.Mwalimu Nyerere alishawahi kukiri kufanya makosa.Wapo baadhi ambao hawataki kujadili kwa uwazi kwa kuhofia kumdhalilisha mwasisi.Hizi ni fikra finyu zinazoendeleza uimla.

Mimi ni Mkatoliki lakini sikubaliani hata kidogo na watu wanaotumia mchakato wa kanisa kumtangaza Mwl.Nyerere kuwa Mtakatifu kama chambo katika suala la kisiasa au suala hili la katiba.

Leo wacha niseme.Tusikubali viongozi wa Dini kutuburuza kimawazo kuhusu suala hili la katiba maana baadhi yao waliwahi kutuambia baadhi ya wagombea Urais ni machaguo ya Mungu kutokana na mitizamo yao binafsi na maslahi yao yasiyokua ya kiroho(Spiritual)

Adolf Hitler alisaidiwa na Askofu Pacelli Kuingia Madarakani kabla hajawa papa.

Mauaji ya Chama cha NAZI dhidi ya Wayahudi Papa Pius Aliyakalia kimya.Adolf Hitla na Pacelli kabla hajawa Papa walikua na Mkataba(Concordat) ambao baadae waliliunganisha kanisa na kujenga uhusiano kati ya Vatican na Serikali ya Kijerumani.

Ukisoma Kitabu cha John Cornwell chenye Title 'Hitlers Pope" Utaona kwanini nasema haya

Kuna kitabu kingine 'Hitler,War and the Pope'

Sasa tujitahidi kujisomea ,tusikubali kuyumbishwa na Baadhi ya Viongozi wa Dini na mambo yao binafsi kwa maslahi binafsi

Nimethubutu kusema .

Ninashangazwa sana na jitihada za kuburuzana na wengine kushawishi kutukuza na kutakasa udikteta kuwa utakatifu.Leo watu wanathubutu kusimama na kusema sauti ya wengi ni sauti ya Mungu wakati huo huo Mtu/watu waliozuia sauti za wengi kwa zaidi ya Miaka 20 wanatakaswa.Watu waliokuta vyama vya upinzani na majukwaa ya kupaza sauti na maoni mbadala kisha akayavunja na kufuta vyama vya upinzani kama wafanyavyo madikteta wengi anaitwa Mtakatifu.

Sitawahi kushawishika kufuata misingi ya kutukuza wanaominya sauti za watu

Itoshe tu kusema kiongozi fulani alikua kiongozi mzuri kulinganisha na Madikteta wengine kama Akina Idd Amin .Basi ,Inatosha.

Mwalimu Nyerere Kuwa Baba wa Taifa ndio heshima inayostahili .Mahali alikofanya Makosa tutasema na kupendrkeza marekebisho na sio kutishana kwa kutangaziana Utakatifu ili tushindwe kukosoa na kurekebisha makosa.

Pitia kitabu Kilichoandikwa na S Mwijage 'The Dark Side of Julius Nyerere' Kilipigwa Marufuku.

Soma kitabu kingine ''Julius Nyerere :The Servant of God or Untarnished Tyrant''.Tusitishane ,tusizoeshane unafiki.Call spade a spade not a big spoon.Sasa nilivisoma na wanikamate kama watavifuta kichwanj mwangu na nahamasisha wengine wavisome soft copy.walisahau kuwa hii ni digital.Unapiga marufuku hard Copy huna uwezo wa kuzuia Soft Copy.

Jambo jingine Muhimu kuweka Kumbukumbu sawa mimi sio miongoni mwa watu wa Kilimanjaro ambao Mzee Agustine Lyatonga Mrema anadai walimtuma kuwa wanataka serikali 2.Yeye sio Msemaji wa Wachaga wala watu wa Kilimanjaro.He should speak for himself.

Wazee wanafiki kama hawa tukiwajibu ipasavyo wanaishia kutishia kutoa laana ovyo ovyo kwa mambo waliojitakia wenyewe.Wajiheshimu

Sitatoa majibu kama ya wale wahuni wa UVCCM waliodai Mzee Warioba atakufa kesho.Huko ni Kuingilia kazi ya Mungu. Tuheshimiane katika mijadala hii na tuache unafiki.Tunaitaka Tanganyika na tuna hoja nzito.Amri ya Kidikteta ya mwaka 1964 haiwezi kutuburuza watanganyika Wote na kuandika historia kwa misingi ya mawazo ya kiimla ya Mtu mmoja.Mimi sitakua mmojawapo.Tanganyika iuawe kwa maoni ya Watu wa Tanganyika na sio Uimla wa mtu mmoja.
 
What the Late Mwl. Nyerere has done for Tanzania needs to be appreciated only. Insulting him wont make any difference but it will make Lissu look like an immature politician while i believe tat he is a matured politician Nyerere was EXTRAORDINARY
 
Huwezi kumtukana Nyerere halafu ukabaki na sifa yako ya awali.
Watanzania bado wanamheshimu Mwalimu Nyerere.
 
Sikutegemea kwa mtu mzima Kama lisu kumtusi muasisi Wa taifa. Alitakiwa kujenga hoja,na kwa njia ta matusi. Tumesononeka sana sisi watanzania,kauli ya mtusi mwalimu haivumiliki. Ningekuwa mimi ndio mkono Wa dola, ningechukua hatua mathubuti. Si kila kitu kazima useme, pima tumia hâta busara ya kawaida. Tunamheshimu mwl na bado tunampenda. Amani unayoiona si kwa bahati mbaya. Karibu kujizuia kwa baadhi ya mambo. Huwezi hâta kidogo wewe lisu kujilinganisha na mwl. Linda heshima yako na chama chako. Kila kona wanasema umekosea. KAzi njema.
Acha ipimbi ni lin uliwahi kuwa CHADEMA??? Unafikiri ukibadili ID hatuta kutambua??? Kwenda na unafiki wako kimada wa ccm mkubwa.
 
Back
Top Bottom