Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Mimi nakushauri usijiondoe kwani hata kwetu wapo, we endelea na chadema yako ila ni wewe ndo mwenye jukumu la kumshauri Lisu aache hako kamchezo kachafu ili hata wewe na chadema muwe wasafi. Kumbuka hauko chadema kwaajili ya Lisu bali ni kwaajili ya watanzania wote
 
Kadi yako namba ngapi? tofautisha mwanachama na shabiki!
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Tundu lisu anatishia ustawi kukua na maslahi ya chama tawala. Hii imejionyesha dhahiri kwa michango yake mizito yenye facts na ukweli mtupu Jana na Leo kwenye bunge la katiba.
Hapana chezea weye
 

Huwaoni waliyo sababisha ! Unakataa kuonyesha hati ya muungano zaidi ya miaka 30 .alafu siku unatoa unasema hii hapa na tutaiweka makumbusho ya taifa kila mtu aone .sasa ulikuwa umeificha kwa sababu zipi .wakat kumbe ata ikiwekwa makumbusho ya taifa .sio tatizo !! .yeye arudi zake ccm asitafute kisingizio afuate bk 7
 
TUNDU ni mwiba mkali magamba akisikia jina tu wanaweseka tuuu
 
Hahaaa...... wasio na hoja na wenye upungufu wa akili huishia kutoa matusi....pole sana Kingukitano na Mungu akusaidie uache kutusi mama zetu
 
Amemkashifu baba wa taifa ila hajamtukana.
Hata hivyo ameonyesha ndimi mbili za Nyerere.Hivi tunamtaja Nyerere wakati tunatafuta nini?
Mana wengi waliokua wanajiganya wamechikizwa ndio walioshiriki kuliua azimio la Arusha ambalo ni msingi wa utu na usawa! Kuondoka kwa Azimio la Arusha ndio kumeleta WanaCCM kuwaona wasio wanaCCM hawastahili hata kuishi.Muungano unaonyesha wazi kwenye Mkataba kuwa ni wa Tanganyika na Zanzibar na sio Tanzania bara na Zanzibar.Mkataba utahatamisha katiba yoyote isiyoitambua Tanganyika.Waliokua wanautafuta walikua na akili sana
 
Haaa!!!
Mimi nilidhani uliondoka baada ya Zitto kuvuliwa nyadhifa zake, kumbe ulibaki?
Wenzio waliondoka.
 
Mimi Sijui matusi mnayapimaje! nimeisoma hotuba ya Lissu yooote lakini sijaona anapotukana tuelimishane tusi gani alilolitoa Lissu
 
Mfa maji hakosi kutapatapa.... !
Their days are numbered.
 
We tokea lini ukawa CDM? Na Nora umekimbia IBM hujatambulika maana una mawazo mgando km CCM, bends CCM ambapo watu wanafikiri kwa kutumia........... Malizia wewe
 
Ndimu au Ndamu...!hujawahi kuwa Chadema member na hutakuja kuwa Chadema member! Chadema si Chama Cha Mashoga, huku kazi tuu! Ukiboronga hata kama una ndevu futi ishirini tutakupa ukweli na kama hupendi sepa!

Next time usianzishe maneno mbofumbofu mbele ya wanaume!
 
re: Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu!

Nakubaliana na ndugu Ng'wamapalala kwamba Waheshimiwa Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wameacha kazi waliotumwa na Watanzania: "kumalizia mchakato wa Katiba", na badala yake wadandia hoja ya kuhoji uhalali au ubatili wa Muungangano. Katika hali ya kawaida, ikiwa kweli Waheshimiwa Wabunge, akina Tundu Lissu, wangekuwa na lengo moja la kutunga Katiba kwa maslahi ya Wananchi wa Tanzania na Muungano wao wasingeanzisha hoja ya kutaka kujua kama Muungano ni halali au la. Katika maisha ya kawaida, watu wawili walioishi pamoja kama mume na mke kwa zaidi ya miaka kumi, achia mbali miaka 50 ya Muungano, wakianza kuhoji uhalali ndoa yao ni kwamba hawataki kuendelea katika mahusiano yao hivyo wanatafuta njia rahisi ya kuvunja mahusiano yao haraka. Sasa, Waheshimiwa Wabunge wanapohoji uhalali wa Muungano tuwaeleweje? Sasa wakitoka na jibu kwamba Muungano ni batili haukuwapo, kuna haja gani ya kutunga Katiba? Watunge Katiba kwa ajili ya nani na kwa lengo gani? Mimi nilidhani jukumu la Bunge letu Maalum lilikuwa kuweka utaratibu (KATIBA) wa kuimarisha na kudumisha uhusiano wetu ambao tumekuwa nao kwa miaka 50. Hivi hili nalo linahitaji kuwa na elimu ya Chuo Kikuu kuweza kulielewa? Hivi ni kweli akina Tundu Lissu na wenzake wakiwauliza wananchi wa kawaida wa Singida, au wafugaji wa Loliondo, au wavuvi na wakwezi wa Mkunazini na Wete kwamba ni kitu gani wanachohitaji Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakifanye ili kuimarisha Muungano wetu, wananchi hao watajibu kwamba wanahitaji kujua kama Muungano huu ni halali au la! Naiwapo jibu la wananchi halitarajiwi kuwa hilo, hawa Waheshimiwa wetu na hoja yao ya uhalali au ubatili wa Muungano wametumwa na nani? Hivi hawa si wanajigamba kuwa ni wawakilishi wa wananchi - "wananchi" hao wanaowawakilisha ni wapi? Mimi ninashauri hawa akina Tundu Lissu, waache utundu na waanze kujadili kupata Katiba itakayoimarisha mahusiano na ushirikiano wa wananchi katika Muungano, na kwa maoni yangu Katiba hiyo ni ile itakayoweka MUUNDO WA SERIKALI MOJA.
 
Ndio. Nasikia kuna kipindi alikuwa ni yeye anamiliki tv kisha anaangalia matukio na kijifanya mtabiri. Ukweli ni binadam na angeweza kuishi kama binadamu wengine. Yeye hakuwa malaika.
 
Kwa kuongezea, watu wengi humu hawamfahamu Mao Zedong, huyu bwana alikuwa mwenyekiti wa chama cha kikomunisti cha china, na raisi wao kwa kipindi kirefu mara baada ya mapinduzi ya miaka ya 40.
Huyu bwana amefanya mambo mengi sana sana china, hakuna mchina ambaye hajawa affected na maamuzi yake, na asilimia kubwa mno, si watu kumi au ishirini, mamilioni ya watu wasiopungua milioni 300 na kuendelea walipata shida sana wakati wa utawala wa huyu bwana. Alikuwa dikteta kamili, alikuw ani sheria, alikuwa ni alfa na omega. Watu wengi sana walimchukia ndani ya China.

Sasa kilichotokea baada ya Kufariki wale waliokuwa wanamchukia wakachukua hatamu, kundi la shanghai la kina Deng Xiaoping na wenzie, hawa mabwana walipata shida sana wakati wa Mao, kwani sera zao hazikupewa nafasi.

Baada ya deng Xiaoping kuchukua nchi akatangaza "Gaiga Kaifang", aka the great opening to the world. China ikaanza kufungua milango yake kwa dunia, ikaanza michakato ya kujiunga IMF n.k.

Hayo yote yakiendelea,ambayo yalikuwa kinyume na wakati wa MAO, Wachina hawakuwahi kumtukana MAO hadharani, hakuna mwanasiasa anayethubutu kumsema vibaya Mao, hata Deng Xiaoping mwenyewe hakuwa na Mafua hayo, kwani Mao alipendwa na watu wengi Mno China, aliwapa wachina kitu kinaitwa sense of security and pride as a nation baada ya kipindi kirefu cha mateso ya wajapani na washirika 7 walioivamia china. Wachina walikuwa tayari ku-sacrifice maisha yao kutimiza Vision ya Mao.

Deng Xiaoping na Timu yake kwa kuwa hawakuwa Vichaa kama kina lisu, waliendelea Kuyatukuza mema ya Mao, na mchanganyiko huu wa mema ya Mao na Mema ya Deng Xiaoping Ndio unaifanya China iwe Taifa linaloogopeka Dunia nzima.

Deng Xiaoping aliendeleza mkono wa chuma alioachiwa na Mao huku akitoa uhuru wa kiuchumi kwa wananchi wake kwa awamu. Miaka 40 toka Mao afariki, wachina wengi waliokuwa hawampendi Mao sasa wanampenda kuliko ilivyokuwa awali, wameelewa sacrifice alizozifanya kwa taifa ili kuwepo na usawa, heshima, nidhamu na mafanikio kwa kila mmoja. Wengi waliompenda Deng Xiaoping hapo mwanzoni, sasa hawawapendi "protege" wake ambao walichukua sera za Deng Xiaoping pure bila kuchanganya na za Mao.

Ukisoma kwa makini utagundua kuwa kati ya hawa viongozi wawili, kila mmoja alifanya makubwa mema, na kila mmoja alikosea kwingi, lakini nia yao kuu ilikuwa kuifanya China iwe sehemu bora kwa kila Mchina. Hakuna upande uliowaita wenzie Matapeli, kwa kuwa wote wamejaaliwa busara. Sera walizotofautiana wanazirekebisha kistaarabu na kubalance kwa manufaa ya wote.

Huyu Nyerere mnayemtukana ndio ametengeneza amani iliyokuwepo sasa, ndio aliyetumia udikteta wake kulinda mipaka ya Tanzania ilipovamiwa, ndio alitumia udikteta wake kuwafanya mabeberu watuheshimu na umasikini wetu, ingawa heshima hiyo inaanza kutoweka kwa kasi, ndio alifanya kila awezalo kwa uwezo wake kuhakikisha elimu inakuwa bure kwa wote, mpaka hao kina Lisu, Slaa, na wazazi wako wewe wakasoma bila shida.

Leo hii kuna Mpuuzi anasimama Bungeni na kumuita Tapeli?seriously?

China kuna mfumo wa vyama vingi?Nadhani Communist Party bado kimeshika hatamu ya nchi,China kuna uhuru wa vyombo vya habari na kutoa Maori yako kwa uhuru,mfumo aliouacha Mao ndo mfumo huo huo unaondelezwa China hadi leo na hivyo si rahisi mtu kumkosoa Mao ndani ya china akawa salama ilhali Mao ndo mwasisi wa mfumo huo.
 
Tundu Lissu amejenga hoja lakini ni Kwanini katika ujengaji hoja wake unaangazia tu upande mmoja tu wa mabaya aliyoyafanya Mwalimu, Watanzania Mimi naamini Mwalimu kama binadamu wengine alikosea mambo kadha wa kadha. Lakini vile vile amefanya mazuri mengi sana ambao hata Tundu leo hii anafurahia matunda yake. Kumuita Mwalimu ni muhuni na muongo nikuishiwa hoja na kukosa busara.
 
Back
Top Bottom