Kwa kuongezea, watu wengi humu hawamfahamu Mao Zedong, huyu bwana alikuwa mwenyekiti wa chama cha kikomunisti cha china, na raisi wao kwa kipindi kirefu mara baada ya mapinduzi ya miaka ya 40.
Huyu bwana amefanya mambo mengi sana sana china, hakuna mchina ambaye hajawa affected na maamuzi yake, na asilimia kubwa mno, si watu kumi au ishirini, mamilioni ya watu wasiopungua milioni 300 na kuendelea walipata shida sana wakati wa utawala wa huyu bwana. Alikuwa dikteta kamili, alikuw ani sheria, alikuwa ni alfa na omega. Watu wengi sana walimchukia ndani ya China.
Sasa kilichotokea baada ya Kufariki wale waliokuwa wanamchukia wakachukua hatamu, kundi la shanghai la kina Deng Xiaoping na wenzie, hawa mabwana walipata shida sana wakati wa Mao, kwani sera zao hazikupewa nafasi.
Baada ya deng Xiaoping kuchukua nchi akatangaza "Gaiga Kaifang", aka the great opening to the world. China ikaanza kufungua milango yake kwa dunia, ikaanza michakato ya kujiunga IMF n.k.
Hayo yote yakiendelea,ambayo yalikuwa kinyume na wakati wa MAO, Wachina hawakuwahi kumtukana MAO hadharani, hakuna mwanasiasa anayethubutu kumsema vibaya Mao, hata Deng Xiaoping mwenyewe hakuwa na Mafua hayo, kwani Mao alipendwa na watu wengi Mno China, aliwapa wachina kitu kinaitwa sense of security and pride as a nation baada ya kipindi kirefu cha mateso ya wajapani na washirika 7 walioivamia china. Wachina walikuwa tayari ku-sacrifice maisha yao kutimiza Vision ya Mao.
Deng Xiaoping na Timu yake kwa kuwa hawakuwa Vichaa kama kina lisu, waliendelea Kuyatukuza mema ya Mao, na mchanganyiko huu wa mema ya Mao na Mema ya Deng Xiaoping Ndio unaifanya China iwe Taifa linaloogopeka Dunia nzima.
Deng Xiaoping aliendeleza mkono wa chuma alioachiwa na Mao huku akitoa uhuru wa kiuchumi kwa wananchi wake kwa awamu. Miaka 40 toka Mao afariki, wachina wengi waliokuwa hawampendi Mao sasa wanampenda kuliko ilivyokuwa awali, wameelewa sacrifice alizozifanya kwa taifa ili kuwepo na usawa, heshima, nidhamu na mafanikio kwa kila mmoja. Wengi waliompenda Deng Xiaoping hapo mwanzoni, sasa hawawapendi "protege" wake ambao walichukua sera za Deng Xiaoping pure bila kuchanganya na za Mao.
Ukisoma kwa makini utagundua kuwa kati ya hawa viongozi wawili, kila mmoja alifanya makubwa mema, na kila mmoja alikosea kwingi, lakini nia yao kuu ilikuwa kuifanya China iwe sehemu bora kwa kila Mchina. Hakuna upande uliowaita wenzie Matapeli, kwa kuwa wote wamejaaliwa busara. Sera walizotofautiana wanazirekebisha kistaarabu na kubalance kwa manufaa ya wote.
Huyu Nyerere mnayemtukana ndio ametengeneza amani iliyokuwepo sasa, ndio aliyetumia udikteta wake kulinda mipaka ya Tanzania ilipovamiwa, ndio alitumia udikteta wake kuwafanya mabeberu watuheshimu na umasikini wetu, ingawa heshima hiyo inaanza kutoweka kwa kasi, ndio alifanya kila awezalo kwa uwezo wake kuhakikisha elimu inakuwa bure kwa wote, mpaka hao kina Lisu, Slaa, na wazazi wako wewe wakasoma bila shida.
Leo hii kuna Mpuuzi anasimama Bungeni na kumuita Tapeli?seriously?