Tundu Lissu na Albert Msando yupi ni mtaalamu zaidi wa Sheria?

Tundu Lissu na Albert Msando yupi ni mtaalamu zaidi wa Sheria?

linjo

Member
Joined
Apr 18, 2013
Posts
19
Reaction score
2
Ndugu wanajamvi naona kupata ueledi wa kutafsir na practice ya sheria kati ya wansheria hao wawili tajwa hapo juu.
 
huyo mtundu kwakweli mi namkubali siyo mchezo ingawa wakati anakabidhiwa rasimu ya katiba JK alimkejeli akisema; ''Kuna wanasheria maarufu kabisa humo kwenye hiyo kamati akiwemo bwana tundu lisu pale ingawa wakati mwingine anakorogakoroga tu sheria na watu wanamkubali''.
 
Msando ni very junior kwa lissu kwa maswala ya kesi za kikatiba
 
Utakuwa unalinganisha kichuguu na mlima na humtendei haki lissu kwa kumlinganisha na huyo kilaza! unataka utumie hii kesi ambayo ina back up ya ccm na ikulu?
 
Kwanza nitamke mwanzoni kabisa kuwa nami pia ni Wakili.Hivyo,sina upande. Kuhusu hawa wawili,wote ni Mawakili Wasomi mahiri kulingana na mashauri wanayoyawakilisha. Ndiyo maana wanaaminiwa. Hatahivyo, Mawakili hawapaswi kupambanishwa au kulinganishwa kwa namna hii. Kazi ya Wakili Mahakamani ni pamoja na kusaidia kutafsiri sheria ili Mahakama itende haki.

Kutokana na kwamba Mahakama ni chombo huru kimaamuzi, tafsiri ya Wakili Msomi yeyote yaweza kuchukuliwa na Mahakama kama ni sahihi. Hakuna upenyo wa Wakili Msomi kuilazimisha Mahakama kukubaliana naye. Na tafsiri iliyokataliwa katika kesi hii yaweza kukubaliwa katika kesi ile.


Kimsingi, umahiri wa Wakili Msomi hujitokeza katika namna ya uwasilishaji wake wa hoja akichagiza na nyaraka,vifungu vya sheria na kesi zilizokwishaamriwa. Pia, utambuzi wa haraka na kukwepa makosa ya kisheria yanayoweza kujitokeza na kupelekea kuharibiwa kwa ladha ya kesi nzima. Hata saini yaweza kuangamiza kesi nzima.

Itoshe kusema kuwa kiuzoefu na kiubobezi, Wakili Msomi Tundu Antipas Mughwai Lissu ni zaidi ya Wakili Msomi Albert Gabriel Msando. Lakini, wote wanabaki kuwa Mawakili Wasomi wazuri na wa kupigiwa mfano.
 
Ndugu wanajamvi naona kupata ueledi wa kutafsir na practice ya sheria kati ya wansheria hao wawili tajwa hapo juu.

Tundu ni Mwaasheria anayezichananya sharia, Jana kwenye press conference katangaza kwamba aliuwa anajuwa matokeo ya kesi kabla hata haijafunguliwa.........kwa hiyo alienda mahakamani kufanya nini huku vifaranga vikiripoti toka kortini kwamba jinsi inavyoenda CDM itashinda sababu Msando Kapanik,mara anatokwa na jasho....mara kesi haina msingi waiweka zuio la nini...........Poor lawyer,hamna mtu mjini atampa kesi yake labda Chadomo hadi pale Mtei/Mbowe watakapomtema..............Kama alijuwa matokeo ya kesi toka mwanzo angeenda mahakamani kutetea maslahi ya CDM kasha kukubaliana na mombi Zitto kutokmjadili...........na sio kubwabwaja kama chiriku.........mwishowe Kichapo cha aibu.
 
Wandugu tusiwe kama wajinga vile, wote hawa ni mawakili wasomi wazuri, kikubwa na uzoefu na umaarufu wa TL via ubunge tu
 
Sheria haina bingwa kwani hao wote huikoroga sheria wanavyofaham wao na huwa wakaidi kuambiwa wanakoroga na huwekwa sawa na watu wadogo tu wa sheria
 
Watanzania ni watu wajinga sana na ni watu wenye viwango vya chini sana walio wepesi sana kuwa impressed na vitu vidogo vidogo.

Naunga mkono,wanapenda kushabikia vitu vya kipuuzi,kwani kuwapambanisha mawakili huo ni mpira wa soka??Ndo useme nani mtaani jembe..Elimu tunayoipata inatusaidia vipi???
 
Lissu hana mpango wowote,anachsnhsnya sheria na kijichanganya mwenyewe
 
Mawazo duni sana yaliyopelekea swali hili.Haya maswali mara nyingi utayakuja vijiwe vya watu wasioenda shule!Niliwahi kukuta watu wakibishana eti kati ya dr Kikwete na mganga mkuu wa wilaya yetu nani bingwa?Sasa ukiona swali kama hilo huna hata haja ya kuhangaika nalo!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom