I know you don't even begin to believe thatUmaarufu na Kujua sheria tofauti. Albert Msando ni wakili mzuri kuliko Tundu Lissu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I know you don't even begin to believe thatUmaarufu na Kujua sheria tofauti. Albert Msando ni wakili mzuri kuliko Tundu Lissu
usikurupuke kama umetoka kufumaniwa TL hajawa maarufu wa via ubunge,huyu jamaa hata mkapa anamtambua maana alisumbua sana kwenye mabo ya madini na mazingira na alishawekwa selo na Mkapa, kumbuka statement ya kikwete "Ni heri Slaa awea raisi kuliko Tundu Lisu kuwa mbunge"ujue kuwa hata jamaa alikuwa najua moto wake, maana hatetelekiWandugu tusiwe kama wajinga vile, wote hawa ni mawakili wasomi wazuri, kikubwa na uzoefu na umaarufu wa TL via ubunge tu
Tundu ni mwanasheria anayekubalika sehemu yoyote mpaka bungeni nikikumbuka sakata la escrow wakati wa kutunga sheria za kuwaadhibu wahusika spika Anna makinda alikuwa anamtegemea sana Tundu Lissu kwenye sheria kesi ya Lema Arusha ya kuvuliwa ubunge na hii ya leo ya mahakama kuu mafanikio yote yanaonyesha uwezo wa Tundu Lissu kwenye sheria.
Ndugu wanajamvi naona kupata ueledi wa kutafsir na practice ya sheria kati ya wansheria hao wawili tajwa hapo juu.
Msando ni mtaalamu wa ku post picha za magari instagram
Kwanza nitamke mwanzoni kabisa kuwa nami pia ni Wakili.Hivyo,sina upande. Kuhusu hawa wawili,wote ni Mawakili Wasomi mahiri kulingana na mashauri wanayoyawakilisha. Ndiyo maana wanaaminiwa. Hatahivyo, Mawakili hawapaswi kupambanishwa au kulinganishwa kwa namna hii. Kazi ya Wakili Mahakamani ni pamoja na kusaidia kutafsiri sheria ili Mahakama itende haki.
Kutokana na kwamba Mahakama ni chombo huru kimaamuzi, tafsiri ya Wakili Msomi yeyote yaweza kuchukuliwa na Mahakama kama ni sahihi. Hakuna upenyo wa Wakili Msomi kuilazimisha Mahakama kukubaliana naye. Na tafsiri iliyokataliwa katika kesi hii yaweza kukubaliwa katika kesi ile.
Kimsingi, umahiri wa Wakili Msomi hujitokeza katika namna ya uwasilishaji wake wa hoja akichagiza na nyaraka,vifungu vya sheria na kesi zilizokwishaamriwa. Pia, utambuzi wa haraka na kukwepa makosa ya kisheria yanayoweza kujitokeza na kupelekea kuharibiwa kwa ladha ya kesi nzima. Hata saini yaweza kuangamiza kesi nzima.
Itoshe kusema kuwa kiuzoefu na kiubobezi, Wakili Msomi Tundu Antipas Mughwai Lissu ni zaidi ya Wakili Msomi Albert Gabriel Msando. Lakini, wote wanabaki kuwa Mawakili Wasomi wazuri na wa kupigiwa mfano.
Watanzania ni watu wajinga sana na ni watu wenye viwango vya chini sana walio wepesi sana kuwa impressed na vitu vidogo vidogo.
Dogo noma ilibidi lisu aombe lugha ibadilike
Tundu la choo lisu hajui sheria ila ni mropokaji.
Chuki huwa haisaidiii... Miafrika ndivyo tulivyo.
Unajua hata maana ya doctorate?
Mwanamke ambaye ni sawa na Mama yako...dada zako....shangazi zako n.k
Si vyema kukashifu wanawake doctorate