Tundu Lissu na Magufuli, mtaondoaje mirundikano ya kesi mahakamani?

Tundu Lissu na Magufuli, mtaondoaje mirundikano ya kesi mahakamani?

Paschal Matubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2008
Posts
235
Reaction score
304
Katika kipindi hiki cha kampeni nimesikia kila mgombea akinadi atakavyoboresha maeneo ya sekta kadhaa ya nchi yetu.

Lakini sijasikia mgombea aliyeahidi kuboresha mahakama zetu na ziondokane na misongamano iliyopo kule.

Nimeona uhuru wa mahakama ukiongelewa kwa juu juu. Nadhani wanasiasa wote wa, CHADEMA, ACT, CCM hawaoni kama hili ni eneo lenye kura nyingi. Hivyo hawaliingii kwa undani.

Hadi sasa kinachoongelewa kuhusiana na mahakama ni mashehe wa uamsho na kesi chache za ucheleweshaji . Hata mimi ninaafiki mashehe wa uamsho wanaonewa kwa kesi yao kuchelewa.

Lakini pia lipo kundi la watu kwenye kesi za madai halina wa kuwasemea wakati ndilo kubwa. Hivyo huwezi kuwaongelea mashehe wa uamsho tu na kuacha hili kundi kubwa ambalo kesi zao zimerundikana mahakamani.

Imefika mahali ukiwa na kesi Mahakama Kuu (High Court) basi hujui kesi yako itachukua miezi au miaka mingapi hata kama umekamilisha taratibu zote (technicalities). Ukiwa na kesi yako Mahakama ya Rufani basi itachukua si chini ya miaka minne pale.

Imefika mahali mtu akikutishia ukorofi halafu ukasema utamshitaki basi ndiyo kwanza anafurahi akijua muda utakaoupoteza mahakamani utakukomesha.

Wakorofi yaani watu binafsi na makapuni wanajua haki yako mahakamani utaipata lakini si chini ya miaka sita kama hujaathirika kisaikolojia kwa kucheleweshwa kwa kesi kwa mrundikano unaoitwa backlog.

Ukishasumbuka hivyo siku nyingine hutatetea sheria, utaishia kuivunja kama wanavyoivunja wengine. Kama ni ufisadi pale ofisini kwako utaona ni bora ufanye kama wenzako ambao hawaogopi sheria. Hivyo ucheleweshaji wa kesi unazalisha wavunja sheria kila leo.

Ukitaka kujua tatizo hili tembelea mahakama zetu uone misongamano huko. Tembelea mahakama za mwanzo, za wilaya, za hakimu mkazi, mahakama kuu na Divisions zake, Mahakama ya Rufani.

Kote huko kumejaa misongamano ya kesi (backlog). Hakimu au Jaji akikurupuka akatoa hukumu mbovu, sheria inakutaka ukate rufani. Unaenda kukata rufani huko nako unakuta msongamano wa rufani.

Sasa hivi Mahakama ya Rufani (Court of Appeal) eti ndiyo imeanza kusikiliza rufani zilizoingia pale mwaka 2016 na chache za mwaka 2017.

Mahakamani kuna mtindo unaitwa FIFO yaani First In First Out yaani kesi iliyoanza kuingia ndiyo inayoanza kusikilizwa. Hivyo Mahakama ya Rufani bado haijaanza na haiwezi kusikiliza kesi za mwaka 2018, 2019 na 2020 wakati ndiyo kwanza sasa imeanza kuzisikiliza za mwaka 2016 na 2017.

Hii maana yake ukipeleka pale rufani yako leo basi usubiri hadi mwaka 2024 isikilizwe! Kimsingi kila mtanzania unaonywa kwamba uombe Mungu kesi yako isifike Mahakama ya Rufani.

Hakuna tofauti kati ya mahakamani na hospitalini. Hata ukiishi kiutakatifu kama malaika unaweza kujikuta umeingia mahakamanani hata kwa kusingiziwa au kwa kudhulumiwa.

Sasa kama mrundikano wa kesi kwenye wa mahakama zetu ni huu basi wewe na utakatifu wako unaweza kuishia kufa kwa pressure kwa sababu ya kesi iliyochelewa kwa miaka nenda rudi.

Tundu Lissu na John Magufuli wote haongelei hili. Sijasikia kwa mfano Magufuli au Tundu Lissu akisema kwa ngazi ya Mahakama Kuu (High Court) amepanga kwa wastani kesi ikianza imalizike ndani ya muda gani.

Sijasikia Magufuli au Tundu Lissu akisema kwa ngazi ya mahakama ya Rufani (Court of Appeal) amepanga kesi imalizike ndani ya muda gani.

Kiujumla sijasikia wote hawa wakiinadi sera ya kupunguza misongamano ya kesi mahakamani wakati ndilo janga la kitaifa mahakamani kuliko hata rushwa.

Wagombea wetu watueleze ili tuwapime watakavyoondoa msongamano wa kesi kuanzia mahakama ya mwanzo hadi mahakama ya Rufani (Court of Appeal).

Karibuni kwenye mjadala.

Asanteni.
 
Hilo swali linapaswa kumlenga TL maana huyo mmoja halimhusu
Pengine naweza sema limeshamshinda
 
Tatizo kubwa zaidi ni mrundikano wa mahabusu. Kuna mgombea mmoja wa Urais anasema yeye akifanikiwa kushinda Urais atapeleka mswada bungeni wa kufuta sheria ya kuzuia dhamana. Kwamba mashitaka yote yawe yanadhaminika

Nakuhakikishia wakifanikiwa kwenye hilo mrundikano wa kesi utapungua sana kwenye mahakama zetu maana kuna watu wanatumia sheria hii kukomoa wenzao. Unapomuweka mahabusu mtu kwa zaidi ya miaka mitano huku kesi haijaanza kusikilizwa kimsingi unakua umemuadhibu na ndio raha ya wenye kuitetea sheria hiyo
 
Hiki ndio CHAMA CHA MAPINDUZI na mifumo yake.

Jiwe ameweka kila kitu mfukoni.
 
Back
Top Bottom