Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na mwamko mpya kiushawishi

Utakuwa na UPOFU wewe si bure. Kawaone wataalamu kabla hujapoteza kabisa hayo macho. Eti ukija huku mtaani hali ni tofauti
😂😂😂😂😂😂


 
MTAZAMO,

..wapinzani wa TL wali-underestimate uelewa wake kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi.

..binafsi sidhani kama TL amebadilika ktk kipindi hiki kifupi cha kampeni, bali naamini amepata nafasi kubwa zaidi ya kujipambanua, na kutoa nafasi kwa wananchi kumjua ni mtu wa aina gani.

..TL ni kati ya wanasiasa wanaosoma, wanaotafiti, na wenye uelewa wa mambo mengi. Naweza kumfananisha na Zitto Kabwe, isipokuwa TL ana machachari mengi hivyo huonekana ni mwanaharakati zaidi.

..Kwa maoni yangu, TL amezitendea HAKI kampeni zetu za uchaguzi wa Raisi. Kwanza, ni mjenga hoja mzuri. Pili, amekulia ktk upinzani, ni mpinzani pure. Tatu, hamuogopi mgombea wa CCM.
 

Haaaaa haaaa, eti huku mtaani, kwani sisi tunaoingia mitandaoni tumehama mitaani? Alichokifanya Magufuli miaka hii mitano ni matumizi mabaya ya madaraka na sio kukubalika kisiasa. Alihakikisha anapandikiza hofu, kufanya unyama na ukatili wa wazi, huku akiondoa uhuru wa vyombo vya habari, na kunyima upinzani kufanya kazi zake za kisiasa.

Kwa bahati mbaya hofu na kuzuia wengine kufanya siasa, ndio ikatafsiriwa kama uimara wa ccm kitu ambacho sio kweli. Huko mtaani unakosema sio kwamba anakubalika, bali kila mtu yuko kimya kuhofia maisha yake, na kulinda shughuli zake zisihujumiwe. Chaguzi zote za marudio ambazo zilikuwa kipimo cha yeye na ccm kukubalika, tulishuhudia ukatili, unyama, ushenzi na uhayawani wa wazi. Uchaguzi wa SM za mitaa ndio kukafanyika upuuzi wa kiwango cha juu kabisa. Je ni lini ccm ingeweza kudhibitisha kukubalika kwake wakati chaguzi zote ilizinajisi?

Hata sasa ccm imejifanya inafanya siasa za kistaarabu kwa tathmini waliyofanya wakiamini wanapendwa sana, na kudhani kuwa upinzani umekufa. Kumbe ukweli ni kuwa upinzani haujafaa bali watu walivunjika moyo kutokana na hujuma za kisiasa zilizoendeleshwa kwa maagizo ya Magufuli. Sasa maadam amejichanganya kuacha siasa zifanyike, yeye na ccm yake wanaona kitu ambacho hawakutegemea. Nakuhakikishia kwa mwendo huu iwapo wapinzani watasimamia mshindi halali kutangazwa, lazima mauaji yatokee iwapo polisi watatii maagizo ya ccm.
 
.. na Lisu kasema kama kushindwa ashindwe kihalali sio figisu hapatatosha
 
Uchaguzi ni uamuzi kuhusu mustakabali wako, familia, majirani, mtaa hadi taifa.
Kura yako inaamua kuhusu maisha ya wote hao.
Hata hivyo, watu wengi ni wajinga wanaofuata mkumbo.
Tz tunakwamia hapa wajinga ni wengi na hakuna dalili yakupungua ambao ndio mtaji wa ccm
 
Tz tunakwamia hapa wajinga ni wengi na hakuna dalili yakupungua ambao ndio mtaji wa ccm
Umasikini mbaya kuliko wote ni ule wa fikra.
Afadhali uwe masikini wa mali ila uwe na fikra/ akili nzuri kwa kuwa utaweza kutafuta mali.
Tatizo ni kubwa zaidi kwa kuwa wengi wanakosa fikra/akili pia mali hawana.
Hapo huwezi tofautisha mtu huyo na mnyama anayewindwa.
 
Well said [emoji123]
 

Mimi nimependa maudhui na mpangilio mzuri wa thread yako ikiwemo numbering of ket points.

Pia, nimependa uwezo wako kufanya fair analysis kwa kuona mazuri na mapungufu kwa kila upande wa kisiasa.
 
Anachokosea JPM ni kufanyia umma hadaa na dhihaka. Kila akizungumza ni kununua ndege kujenga barabara, sijui kuwaletea maendeleo. Kuna siku nilimwambia mtu mimi ninaweza kuandika hotuba ya magufuli maana ni toka mwezi aliongelea mambo ya makinikia ndio hiyo hiyo. Sasa kaingizwa kwenye mtego mdogo sana wa kushusha simenti na vitu ambavyo vinagusa maisha ya kila siku. Yeye kila uchwao ndege ndege mara bwawa sijui na mambo mengine ya ajabu ajabu.
 
Hata mie nilikuwa naona hivyo mwanzoni lakini sasa inaanza kuona hali inabadIlika kwa kasi, nahisi kuna ujasiri wa kuzungumza umeongezeka kidogo maana wengi wamemgeukia lissu na kuahidi kumpa kura
 
Hawezi kushinda kwa kura ? Hapo ndio unapokosea kabisa. Endelea kuamini ya mitandao ila utashangaa mwenyewe .
 
Siyo rahisi kama unavyodhani. Wapiga kura wengi huwa hawaendi mikutanoni. Subiri matokeo tarehe 30/10/2020 uone.
 
Lisdu hajashinda na wala hatashinda. Msijipe matumaini yasiyokuwepo
 
hiyo # 7 sijakupatapata ndugu.

ina maana hujasikia wagombea wa upinzani walioenguliwa?

unajua kuna majimbo ambayo hakuna mgombea hata mmoja kuanzia udiwani hadi ubunge?

je, hizi siyo vurugu za serekali ya JPM?

je, huoni wanaostahili credit kwenye hili ni kambi ya upinzani ambayo pamoja na kufanyiziwa hivi bado wameendelea kuwa wastaarabu?
 
Umemueleza ukweli mchungu. Akiri tu kuwa Magu na CCM yake wana hali mbaya kutokana na matendo ya Magufuli na serikali yake ya kutojali utu na maisha ya watu plus hali ngumu ya maisha waliyoisababisha .

Hoja kwamba Lissu mwanzoni alikuwa hana sera zaidi ya kumshambulia Magu, si ya kweli, bali anatafuta sababu tu ya kuwafanya watu waamini kuwa hakuumuunga mkono kwasababu hiyo na sasa Lissu kabadilika kumbe amegundua Lissu hakamatiki au kuna mambo alikuwa hawajui sasa Lissu kamfunulia mfano la kikokotoo baada ya 2020 kitavyokuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…