Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na mwamko mpya kiushawishi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na mwamko mpya kiushawishi

Utakuwa na UPOFU wewe si bure. Kawaone wataalamu kabla hujapoteza kabisa hayo macho. Eti ukija huku mtaani hali ni tofauti
😂😂😂😂😂😂

Mtu ukiwa umemiss kupata likes hapa JF wewe andika tu lolote kuhusu Chadema na mgombea wake hakika utapata likes za kutosha ila in reality they mean nothing.

Ukija huku mtaani hali ni tofauti kabisa, hakuna likes bali unakutana na uhalisia wa namna Rais Magufuli alivyojijengea heshima katika jamii yetu.
 
MTAZAMO,

..wapinzani wa TL wali-underestimate uelewa wake kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi.

..binafsi sidhani kama TL amebadilika ktk kipindi hiki kifupi cha kampeni, bali naamini amepata nafasi kubwa zaidi ya kujipambanua, na kutoa nafasi kwa wananchi kumjua ni mtu wa aina gani.

..TL ni kati ya wanasiasa wanaosoma, wanaotafiti, na wenye uelewa wa mambo mengi. Naweza kumfananisha na Zitto Kabwe, isipokuwa TL ana machachari mengi hivyo huonekana ni mwanaharakati zaidi.

..Kwa maoni yangu, TL amezitendea HAKI kampeni zetu za uchaguzi wa Raisi. Kwanza, ni mjenga hoja mzuri. Pili, amekulia ktk upinzani, ni mpinzani pure. Tatu, hamuogopi mgombea wa CCM.
 
Mtu ukiwa umemiss kupata likes hapa JF wewe andika tu lolote kuhusu Chadema na mgombea wake hakika utapata likes za kutosha ila in reality they mean nothing.

Ukija huku mtaani hali ni tofauti kabisa, hakuna likes bali unakutana na uhalisia wa namna Rais Magufuli alivyojijengea heshima katika jamii yetu.

Haaaaa haaaa, eti huku mtaani, kwani sisi tunaoingia mitandaoni tumehama mitaani? Alichokifanya Magufuli miaka hii mitano ni matumizi mabaya ya madaraka na sio kukubalika kisiasa. Alihakikisha anapandikiza hofu, kufanya unyama na ukatili wa wazi, huku akiondoa uhuru wa vyombo vya habari, na kunyima upinzani kufanya kazi zake za kisiasa.

Kwa bahati mbaya hofu na kuzuia wengine kufanya siasa, ndio ikatafsiriwa kama uimara wa ccm kitu ambacho sio kweli. Huko mtaani unakosema sio kwamba anakubalika, bali kila mtu yuko kimya kuhofia maisha yake, na kulinda shughuli zake zisihujumiwe. Chaguzi zote za marudio ambazo zilikuwa kipimo cha yeye na ccm kukubalika, tulishuhudia ukatili, unyama, ushenzi na uhayawani wa wazi. Uchaguzi wa SM za mitaa ndio kukafanyika upuuzi wa kiwango cha juu kabisa. Je ni lini ccm ingeweza kudhibitisha kukubalika kwake wakati chaguzi zote ilizinajisi?

Hata sasa ccm imejifanya inafanya siasa za kistaarabu kwa tathmini waliyofanya wakiamini wanapendwa sana, na kudhani kuwa upinzani umekufa. Kumbe ukweli ni kuwa upinzani haujafaa bali watu walivunjika moyo kutokana na hujuma za kisiasa zilizoendeleshwa kwa maagizo ya Magufuli. Sasa maadam amejichanganya kuacha siasa zifanyike, yeye na ccm yake wanaona kitu ambacho hawakutegemea. Nakuhakikishia kwa mwendo huu iwapo wapinzani watasimamia mshindi halali kutangazwa, lazima mauaji yatokee iwapo polisi watatii maagizo ya ccm.
 
Uchaguzi wa kistaarabu kivipi na haujafanyika? Ndiyo kampeni sasa hivi na CCM na Magufuli wamepigwa na upepo wa kisulisuli na hawakutegemea kuwa Magufuli anachukiwa kiasi hiki mpaka kanda ya Ziwa ambayo ndiyo ilimwokoa uchaguzi uliopita?

Huu uchaguzi unaweza kuwa ndiyo wenye vurugu kuliko nyingine zote kwa sababu Magufuli anajua kabisa yuko kwenye hali mbaya na hawezi kushinda kwa kura huku wananchi wakiwa wameamua kuwa liwalo na liwe lakini kipindi hiki CCM ifikie mwisho.
.. na Lisu kasema kama kushindwa ashindwe kihalali sio figisu hapatatosha
 
Uchaguzi ni uamuzi kuhusu mustakabali wako, familia, majirani, mtaa hadi taifa.
Kura yako inaamua kuhusu maisha ya wote hao.
Hata hivyo, watu wengi ni wajinga wanaofuata mkumbo.
Tz tunakwamia hapa wajinga ni wengi na hakuna dalili yakupungua ambao ndio mtaji wa ccm
 
Tz tunakwamia hapa wajinga ni wengi na hakuna dalili yakupungua ambao ndio mtaji wa ccm
Umasikini mbaya kuliko wote ni ule wa fikra.
Afadhali uwe masikini wa mali ila uwe na fikra/ akili nzuri kwa kuwa utaweza kutafuta mali.
Tatizo ni kubwa zaidi kwa kuwa wengi wanakosa fikra/akili pia mali hawana.
Hapo huwezi tofautisha mtu huyo na mnyama anayewindwa.
 
Well said [emoji123]
 
Wakuu,

Kampeni za uchaguzi zinaendelea na kwasababu ya mabadiliko makubwa ya kiushawishi ya Tundu Lissu yanayomfanya ajipatie mashabiki kwa kasi ambayo wengi (ikiwemo mimi) hatukutegemea, nimeona niandike machache kwanini anafanikiwa;

1) Lissu alianza vibaya kampeni kwa hotuba zake kujaa hoja za kiharakati ambazo haziongezi kura. Mashambulizi binafsi kwa mgombea wa CCM yalijaa jeuri isiyojenga wala kuongeza kura hivyo kuonekana na umma kama mwanaharakati zaidi ya amri jeshi mkuu mtarajiwa.

2) Hoja namba moja ndio kiini cha Lissu kujirekebisha na kubadili upepo wa kampeni. Lissu akaanza kuacha kumzungumzia sana mgombea wa CCM na kujikita kwenye shida za watu.

3) Chadema wametafiti na kutambua maeneo ambayo hayajafanyiwa kazi na kujikita huko kuliko kuponda tu miradi ambayo hoja yao imekuwa haieleweki na wananchi wengi. Sasa Lissu anazungumza habari za bei ya Cement, kupandisha mishahara, Fao la kujitoa n.k

4) Lissu ameanza kuheshimu vyombo vya dola na hata leo amewasifia. Hii ni mbinu ya kuwachota kisaikolojia askari na watumishi wengine ili wapate ushirikiano wao kikamilifu. Nafikiri hii itazidi kumuongezea wafuasi maana anajipambanua kama Amri Jeshi mkuu mtarajiwa.

5) Pamoja na ukubwa wa CCM lakini uchaguzi huu wana tatizo kubwa kupangua hoja kwenye maeneo ambayo hawakufanya vizuri. Kwanza wanaonesha hawajui vision ya mgombea wao toka alipoingia madarakani. JPM amefanya kazi nzuri sana lakini kuna maeneo hakufanya vizuri na lazima wajipange kutoa majibu ya wazi maana Chadema wamejikita huko.

6) Kwa ujumla tulitegemea kampeni zitazotawaliwa na CCM kutokana na upinzani kuwa nusu kaputi kwa muda mrefu lakini Lissu amebadili upepo na kufanya tushuhudie moja ya uchaguzi ambao hoja ndio zitazotawala na kutoa fursa kwa wananchi kuamua yupi atawafaa.

7) Pia mnyonge mnyongeni haki yake apewe. JPM anakwenda kuandika historia ya kuendesha uchaguzi kistaarabu bila vurugu tulizoshuhudia chaguzi zilizopita. Kwasababu wengi tunasahau lakini chaguzi zilizopita ziligubikwa na mengi. Pamoja na mapungufu machache lakini kampeni zinakwenda vyema na tuendelee kuomba hali ibaki hivi hadi mwisho.

Hakika Tundu A. Lissu amebadili upepo na kuleta ladha halisi ya kampeni za ushindani kihoja.

Asanteni,
MTAZAMO.

Mimi nimependa maudhui na mpangilio mzuri wa thread yako ikiwemo numbering of ket points.

Pia, nimependa uwezo wako kufanya fair analysis kwa kuona mazuri na mapungufu kwa kila upande wa kisiasa.
 
Anachokosea JPM ni kufanyia umma hadaa na dhihaka. Kila akizungumza ni kununua ndege kujenga barabara, sijui kuwaletea maendeleo. Kuna siku nilimwambia mtu mimi ninaweza kuandika hotuba ya magufuli maana ni toka mwezi aliongelea mambo ya makinikia ndio hiyo hiyo. Sasa kaingizwa kwenye mtego mdogo sana wa kushusha simenti na vitu ambavyo vinagusa maisha ya kila siku. Yeye kila uchwao ndege ndege mara bwawa sijui na mambo mengine ya ajabu ajabu.
 
Mtu ukiwa umemiss kupata likes hapa JF wewe andika tu lolote kuhusu Chadema na mgombea wake hakika utapata likes za kutosha ila in reality they mean nothing.

Ukija huku mtaani hali ni tofauti kabisa, hakuna likes bali unakutana na uhalisia wa namna Rais Magufuli alivyojijengea heshima katika jamii yetu.
Hata mie nilikuwa naona hivyo mwanzoni lakini sasa inaanza kuona hali inabadIlika kwa kasi, nahisi kuna ujasiri wa kuzungumza umeongezeka kidogo maana wengi wamemgeukia lissu na kuahidi kumpa kura
 
Hawezi kushinda kwa kura ? Hapo ndio unapokosea kabisa. Endelea kuamini ya mitandao ila utashangaa mwenyewe .
Uchaguzi wa kistaarabu kivipi na haujafanyika? Ndiyo kampeni sasa hivi na CCM na Magufuli wamepigwa na upepo wa kisulisuli na hawakutegemea kuwa Magufuli anachukiwa kiasi hiki mpaka kanda ya Ziwa ambayo ndiyo ilimwokoa uchaguzi uliopita?

Huu uchaguzi unaweza kuwa ndiyo wenye vurugu kuliko nyingine zote kwa sababu Magufuli anajua kabisa yuko kwenye hali mbaya na hawezi kushinda kwa kura huku wananchi wakiwa wameamua kuwa liwalo na liwe lakini kipindi hiki CCM ifikie mwisho.
 
Siyo rahisi kama unavyodhani. Wapiga kura wengi huwa hawaendi mikutanoni. Subiri matokeo tarehe 30/10/2020 uone.
Vyombo vya dola sasa rasmi vimepewa commitment ya Raisi Mtarajiwa wa Tanzania 2020- 2025 kuwa hawatapoteza kazi zao wala vyeo vyao

Kwa hili namshauri ndugu Magufuli apaki tu vitu vyake kujiandaa kurudi chato baada ya Uchaguzi

Lissu is another level[emoji119]
 
Lisdu hajashinda na wala hatashinda. Msijipe matumaini yasiyokuwepo
 
Wakuu,

Kampeni za uchaguzi zinaendelea na kwasababu ya mabadiliko makubwa ya kiushawishi ya Tundu Lissu yanayomfanya ajipatie mashabiki kwa kasi ambayo wengi (ikiwemo mimi) hatukutegemea, nimeona niandike machache kwanini anafanikiwa;

1) Lissu alianza vibaya kampeni kwa hotuba zake kujaa hoja za kiharakati ambazo haziongezi kura. Mashambulizi binafsi kwa mgombea wa CCM yalijaa jeuri isiyojenga wala kuongeza kura hivyo kuonekana na umma kama mwanaharakati zaidi ya amri jeshi mkuu mtarajiwa.

2) Hoja namba moja ndio kiini cha Lissu kujirekebisha na kubadili upepo wa kampeni. Lissu akaanza kuacha kumzungumzia sana mgombea wa CCM na kujikita kwenye shida za watu.

3) Chadema wametafiti na kutambua maeneo ambayo hayajafanyiwa kazi na kujikita huko kuliko kuponda tu miradi ambayo hoja yao imekuwa haieleweki na wananchi wengi. Sasa Lissu anazungumza habari za bei ya Cement, kupandisha mishahara, Fao la kujitoa n.k

4) Lissu ameanza kuheshimu vyombo vya dola na hata leo amewasifia. Hii ni mbinu ya kuwachota kisaikolojia askari na watumishi wengine ili wapate ushirikiano wao kikamilifu. Nafikiri hii itazidi kumuongezea wafuasi maana anajipambanua kama Amri Jeshi mkuu mtarajiwa.

5) Pamoja na ukubwa wa CCM lakini uchaguzi huu wana tatizo kubwa kupangua hoja kwenye maeneo ambayo hawakufanya vizuri. Kwanza wanaonesha hawajui vision ya mgombea wao toka alipoingia madarakani. JPM amefanya kazi nzuri sana lakini kuna maeneo hakufanya vizuri na lazima wajipange kutoa majibu ya wazi maana Chadema wamejikita huko.

6) Kwa ujumla tulitegemea kampeni zitazotawaliwa na CCM kutokana na upinzani kuwa nusu kaputi kwa muda mrefu lakini Lissu amebadili upepo na kufanya tushuhudie moja ya uchaguzi ambao hoja ndio zitazotawala na kutoa fursa kwa wananchi kuamua yupi atawafaa.

7) Pia mnyonge mnyongeni haki yake apewe. JPM anakwenda kuandika historia ya kuendesha uchaguzi kistaarabu bila vurugu tulizoshuhudia chaguzi zilizopita. Kwasababu wengi tunasahau lakini chaguzi zilizopita ziligubikwa na mengi. Pamoja na mapungufu machache lakini kampeni zinakwenda vyema na tuendelee kuomba hali ibaki hivi hadi mwisho.

Hakika Tundu A. Lissu amebadili upepo na kuleta ladha halisi ya kampeni za ushindani kihoja.

Asanteni,
MTAZAMO.
hiyo # 7 sijakupatapata ndugu.

ina maana hujasikia wagombea wa upinzani walioenguliwa?

unajua kuna majimbo ambayo hakuna mgombea hata mmoja kuanzia udiwani hadi ubunge?

je, hizi siyo vurugu za serekali ya JPM?

je, huoni wanaostahili credit kwenye hili ni kambi ya upinzani ambayo pamoja na kufanyiziwa hivi bado wameendelea kuwa wastaarabu?
 
Huna lolote mtoa mada. Kwa hiyo wewe ulitaka aongee kila kitu siku moja? Au siku ya kwanza?

Mambo ya kuongelea Ni mengi Sana asingeweza kuyaeleza yote. Mambo yanaenda kwa mpango, nabado ataongea mambo mazuri na makubwa huko mbele.

Sema naona unajiandaa kisaikolojia tu. Baada ya kuona mtu wako anawekwa uchi,na Nini kitamfika.
Umemueleza ukweli mchungu. Akiri tu kuwa Magu na CCM yake wana hali mbaya kutokana na matendo ya Magufuli na serikali yake ya kutojali utu na maisha ya watu plus hali ngumu ya maisha waliyoisababisha .

Hoja kwamba Lissu mwanzoni alikuwa hana sera zaidi ya kumshambulia Magu, si ya kweli, bali anatafuta sababu tu ya kuwafanya watu waamini kuwa hakuumuunga mkono kwasababu hiyo na sasa Lissu kabadilika kumbe amegundua Lissu hakamatiki au kuna mambo alikuwa hawajui sasa Lissu kamfunulia mfano la kikokotoo baada ya 2020 kitavyokuwa.
 
Back
Top Bottom