Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na mwamko mpya kiushawishi

You are the man, you nailed it Mtazamo, one of the best members of jf
 
Uchaguzi huu ni point kubwa sana kwa serikali kwa jamii ya kimataifa, Inaweza ikawa kweli or siyo kweli ila kuna uwezekano mkubwa sana Tundu ni mtu wa system, give them what they want/democracy. Mwisho wa siku lets fight kwa ajili ya Tz, our beautiful country.
 
Naona umeanza kuelewa sasa!! karibu kundini!!
 
Endelea kujiaminisha ujinga.
Kitu kimoja anachosahau MTAZAMO ni kwamba bila Mh. Tundu Antiphas Lissu kumshusha Magufuli kutoka umungu hadi ubinadamu, anayeweza kupingwa na kukosolewa kama binadamu wengine hali haingekuwa hivi.

Ni sasa wananchi wengi wamezinduka na kumuona kama binadamu mwenzao na kama Lissu hakuwatoa watu uwoga tangu mapema kampeni hii haingefikia ilipofikia na watu hawangejitokeza kwa wingi kwenye mikutano yake.

Mwanzoni wananchi waliogopa hata kujihusisha na Lissu wakiogopa kushukiwa na vyombo vilivyopaswa kuwalinda lakini vikajisahau na kufikiri ni walinzi wa serikali na si wananchi na hata Bunge ni mfano mojawapo katika vyombo hivyo.

Lugha sahihi ya kinachoitwa busara ya Magufuli ni ujasiri wa Mh. Tundu Antiphas Lissu by grabbing the bull by its horns. Tanzania ni nchi iliyojaa wanafiki na waoga ambao hawako tayari kudai haki zao zinapoporwa na utawala wa kibabe.
 
Hivi wewe hio mitaa unaishi peke yako?? sisi hatuko mitaani eee??
 
Ahsante Mkuu kwa kuliona hili.. Ila nina wasiwasi na huko tuendako maana matukio ya kuwatia watu hofu kama yale ya Soweto huko Arusha watu wabaya wanaweza kuyatengeneza..
 
Hakika nimeshuhudia fikra yakinifu kutoka kwa mtu makini mwenye hakika ya anachokiandika, Ingekuwa vizuri Kama ungekuwa Fanani wa hadhira chache isiyokuwa na uhakika katika mtazamo.
 
Siyo rahisi kama unavyodhani. Wapiga kura wengi huwa hawaendi mikutanoni. Subiri matokeo tarehe 30/10/2020 uone.
Endeleeni kuishi na akili za mwaka 47. Vijijini huko hawataki kabisa kumsikia magufuli. Ameharibu kupindukia biashara za mazao za wakulima na sasa wanasumbuliwa na umaskini uliopindukia. Si tumbaku, si kahawa, si chai, si korosho, si pamba si mbaazi wala si mahindi
 
Mtazamo Ana chuki na CDM,
Lissu mwenyewe alituahidi kuwa "mwaka huu ni mwaka wa kusema na atasema mengi,anayo mengi sana ya kusema"
Kwa hiyo asingeweza kuongea mambo yote siku ya kwanza.
Sasa ameanza kuongea,na bado Ana mengi ya kuongea.
Huyu jamaa kaona Moto wa Lissu unakole kila siku,na atashinda Sasa jamaa analisubiri Basi la Mageuzi kwenye kituo Cha mbele Sana,anaona aibu kipandia hapo alipo.
 
Mkuu
 
Uchaguzi wa kistaarabu sababu keshabanwa na wakuu wa dunia kwamba chumba chake kinasafishwa the Hague achague moja the Hague au Chato, maana wamechoka kuhudumia wakimbizi sababu ya watawala waliokosa malezi Bora utotoni.
 
Acha utani wewe... yaani kwako unaona JPM kwa hili anastahili kupongezwa?!

Yaani unampongeza mzazi kumwandikisha mtoto shule wakati ni WAJIBU wake kufanya hivyo?!

Yaani "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni" kwa mwalimu kuingia darasani kufundisha au daktari kumtibu mgonjwa wakati ni WAJIBU wao?!

Yaani "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni" kwa serikali kulipa mishahara ya watumishi wa umma wakati ni WAJIBU wake kufanya hivyo?

Yaani JPM apongozwe kuendesha uchaguzi eti "Kistaarabu" wakati ni WAJIBU wa serikali kuhakikisha HAWATUMII vyombo vya dola kufanya uhuni?

Yaani "Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni" kisa tu Mshindani yule yule Mhuni ambae pia ndie mwenye nguvu ya dola na kufanya uhuni for almost 5 years in a row ili kuwavunja nguvu washindani wake lakini siku ya kupanda uliongoni "anajifanya muungwana" ndo ndo unataka apongezwe kwa "uungwana fake" aliofanya dakika za mwisho wakati ameshafanya uhuni wa kutisha dhidi ya mahasimu wenzake kabla ya kupanda ulingoni?

Uchaguzi ni MCHAKATO, na mchakato huu hauanzi na kuishia kwenye kipindi cha kampeni!!

Pamoja na uhuni mwingine, pia amefanya UHUNI Tanzania mzima kupitia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuhakikisha Upinzani hawana uongozi ngazi za chini halafu bila aibu unasema eti JPM apongezwe?! Kwa lipi?!

Yaani kwa akili yako kuwepo kwa hicho unachoita uchaguzi wa "kistaarabu" unaona ni favor kwa upinzani kutoka kwa JPM, au?!
 
Ccm awakujipanga kwa hoja sababu wakizuiwa wapinzani wasiongee 5 yrs wangewaacha waongee wangejua jinsi ya kupangua hoja.
Ccm walijipanga na flyover, sgr, bwawa, mabeberu, corona, ndege hizi hoja haziuziki vijijini kumwambia mtu wa kijijini aelewe flyover, sgr, ndege Ni lzm uwe na projecta plus dictionary ili wakuelewe, thus tumeona Hadi vijijini eti wanawahidi ndege, sgr. Awajui kipi waongee kulingana na mahitaji ya eneo husika.
Cdm kampeni meneja wao wako vizuri Sana this time wanagusa hoja za wananchi husika, plus njaa na mateso ya miaka hii 5 ccm imesaidia Sana kuwapigia kampeni upinzani. Hata waunga juhudi waliingizwa kingi na jiwe kwamba atawarudisha bungeni wanajutia maamuzi yao.
Kama tu Kanda ya ziwa ngome yao ccm umepelekewa Moto hatari wa gesi vipi Kanda walizozibagua au walizozulumu mazao yao. Mwaka huu ccm itashinda dodoma na tabora pekee, mikoa yote inayopakana na nchi jirani ccm haiuziki
 
Mpaka sasa ni kama hawakuandaa majibu ya mapungufu yao. Ni vyema PhDs za akina Dr Bashiru zifanye kazi sasa maana Chadema wamepata hoja za kujidai na ambazo zinagusa wananchi moja kwa moja.
 
Hivi mbona sijasikia hoja ya viwanda kutoka kwa ccm. Viwanda vyoooote walivyovijenga kwa miaka 5 hawataki hata kuvisemea kuwa wataviboresha? Siyo haki kabisa.
Mkuu acha kuboresha tu... Huwezi kuongelea kitu ambacho hakipo.

Hii nchi miradi ya kwenye maandishi ni mingi kuliko uhalisia wake.
 
Uchaguzi upi wa kistaharabu wakati mmewaengua wagombea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…