Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na Salamu za Krismas: Mwaka 2020 ulikuwa mwaka mgumu na wenye machungu mengi kwa nchi na wananchi wetu

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na Salamu za Krismas: Mwaka 2020 ulikuwa mwaka mgumu na wenye machungu mengi kwa nchi na wananchi wetu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Sasa ni dhahiri Tundu Lissu ni Mcha Mungu.

==========

TUNDU LISSU: Ndugu wananchi wa Tanzania, tumsifu Yesu Kristo, Bwana asifiwe, mwanakondoo ameshinda, Assalam Aleykum Warahmatullah Wabarakatuh. Kesho ni sikukuu ya Noeli kwa wale wote wanaoamini katika dini ya Ukristo.
Kwa wakristo wote, Noeli ni sikukuu ya kuzaliwa kwa mwokozi wetu yesu Kristo aliyetolewa na Mungu kama yanavyosema maneno ya kitabu cha Yohana aya ya tatu mstari wa 16 'Ili kila mtu amuaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele'.

Sikukuu hii inatukumbusha kuhusu moyo wa kutoa na moyo wa kusamehe kwa sababu kama yanavyosema maandiko matakatifu, Yesu Kristo alizaliwa ili wote wanaomuamini wasemehewe. Katika kalenda ya Kikristo hii ndio siku ya furaha na sherehe kuliko nyingine zote lakini Krismas ni zaidi ya siku ya furaha na sherehe.

Ni siku pia ya kuwakumbuka na kuwasaidia wale wote walio na shida na matatizo mbalimbali, Mwinjilisti Ruth aliwahi kusema "Krismas ni krismas kweli tunaposheherekea kwa kuwapa mwanga wa upendo wale wanaouhitaji zaidi" Wapo wengi wanaohitaji mwanga huu wa upendo katika nchi yetu ya Tanzania katika kipindi hiki cha Noeli.

Mwaka 2020 ulikuwa mwaka mgumu na wenye machungu mengi kwa nchi yetu na kwa wananchi wetu, wote tulishuhudia haki yetu ya kuchagua viongozi tunaowataka ikipokwa kwa mtutu wa bunduki na kwa kutumia vyombo vya usimamizi wa uchaguzi na vya serikali visivotenda haki sawasawa, wapo ambao ndugu zao waliuawa au waliojeruhiwa na kulemazwa wakati wa uchaguzi mkuu na hata kabla ya hapo.

Wapo waliokamatwa na kustakiwa au wanaoendelea kushkiliwa magerezani au kwenye vituo vya polisi kwa tuhuma za uongo, uonevu na kwa sababu za kisisasa.

Wapo pia ambao wamefukuzwa kazi, wamebomolewa nyumba au kuharibiwa biashara zao au kunyang'anywa pesa na mali zao kwa madai ya uongo ya ukwepaji kodi au kwa tuhuma zisizo za kweli za uhujumu uchumi au utakatishaji fedha.

Wengine kama mimi mwenyewe wamelazimika kuikimbia nchi yetu kwa sababu ya njama na vitisho vya mauaji dhidi yao. Aidha, wapo kwa mamilioni mengi wanaosononeka kimya kimya kwasababu ya kutokupatiwa ajira au kkwa kutolipwa mishahara au pensheni zao halali au kwa kutotendewa haki zao nyingine mbalimbali.

Kwa wote hawa wenye njaa na kiu ya haki, ujumbe wangu wa Krismas ni uleule alioueleza mwandishi wa riwaya wa kimarekani, Taylor Caldwell, "Hatuko peke yetu, hata usiku unapokuwa wa giza zaidi au upepo wa baridi kali au ulimwengu unapoonekana kutokujali kabisa" Hatuko peke yetu, kwahiyo tusivunjike moyo au kukata tamaa, wiki ijayo katika salamu zangu za mwaka mpya nitawazungumza kwa kirefu kidogo juu ya maswala haya na mengine mengi na juu ya majukumu yetu kwa mwaka ujao kuhusu nchi yetu.

Nawatakieni sikukuu ya Noeli yenye furaha

 
Tangu lini 'mshitaki wa watu wa Mungu' (shetani) akawa mcha Mungu na kuwatakia watu kheri ya Krismas? Makubwa haya!
Aliwadanganya Adam na Eva kwa kujifanya ni malaika wa nuru, kumbe hakuna lolote.
Mwambie tumeshituka, hatudanganyiki na salamu za kizandiki.
 
Tangu lini 'mshitaki wa watu wa Mungu' (shetani) akawa mcha Mungu na kuwatakia watu kheri ya Krismas? Makubwa haya!
Aliwadanganya Adam na Eva kwa kujifanya ni malaika wa nuru, kumbe hakuna lolote.
Mwambie tumeshituka, hatudanganyiki na salamu za kizandiki.
Huwa nafurahishwa sana na wanaoongea kinyume nyume ili kukwepa kutekwa
 
Tangu lini 'mshitaki wa watu wa Mungu' (shetani) akawa mcha Mungu na kuwatakia watu kheri ya Krismas? Makubwa haya!
Aliwadanganya Adam na Eva kwa kujifanya ni malaika wa nuru, kumbe hakuna lolote.
Mwambie tumeshituka, hatudanganyiki na salamu za kizandiki.
Mbona hivyo mrembo, punguza kudakia mambo yalio nje ya uwezo wako.. Sawa bibie.. Ni ushauri tu.
 
Asante mbeba maono. Mungu awe nawe huko uliko. Japo upo mbali nasi kimwili, kiroho, kifikra lkn ugumu wa maisha unatufanya tusikusahau.

Uliyotuambia wakati wa kampeni yameanza kutimia mhe rais wa mioyo ya wananchi wa Tanzania.

Lile joka (jiwe) sasa limeanza kunya moto. Kijiji cha Chato kinazidi kutengewa fedha mabilioni kwa mabilioni. Tunaambiwa campus za vyuo vyote zitahamishiwa Chato. Bandari ya Dar itaenda Chato. Mlima Kilimanjaro utabebwa na kupekekwa Chatto.

Waziri wa mali asili kateuliwa na kupewa maagizo kuhakikisha wanyama aina zote wanahamishiwa Burigi.

Mbeba maono nisikuchoshe. Nikupe moja la mwisho. Wale wakurugenzi waliohujumu ushindi wako wameanza kusomeshwa namba.

Xmass njema baba, mbeba maono, rais wetu tuliyekuchagua kwa kura lkn dola ikakudhulumu.
 
Aliyewekwa na vikosi vya ulinzi na usalama wala hajaweza kupata maono ya kulihutubia taifa. Amepofushwa na mwenyezi Mungu akajikuta anayasaliti mamlaka feki aliyojivika

Mungu amempa maono ya kulihutubia taifa yule aliyempa ushindi kupitia kura za wananchi ndugu TAML.

Mungu wetu kweli ni mwaminifu.
 
sawa.. mwambie tumepokea salamu.. ila atusalimie kwa French siku ingine.. hajajifunza ya nchi yake mupya? au tutachangishana ajifunze.. 😀

Kwa wasiojua hata kiingereza tufanyeje mkuu?
 
Lissu alikosea sana kudhani kuwa uanaharaki ndiyo uongozi wa kisiasa. Uanaharakati una nafasi yake na uongozi wa kisiasa pia una nafasi yake. Nadhani kosa kubwa ni kwa wale waliomshambulia kwa vile walisababaisha aendelee kuwa relevant wakati tayari alikuwa ana fade out.
 
Back
Top Bottom