Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na Salamu za Krismas: Mwaka 2020 ulikuwa mwaka mgumu na wenye machungu mengi kwa nchi na wananchi wetu

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na Salamu za Krismas: Mwaka 2020 ulikuwa mwaka mgumu na wenye machungu mengi kwa nchi na wananchi wetu

Tutawasaliana na serikali ya ubelgiji. Ujerumani Canada uingereza na Marekani anakohaha kutafuta hadhi ya ukimbizi wasimpe kwa anajishughulisha na siasa za Tanzania wakati anaomba ukimbizi nchi zao
 
C&P


JE ! YESU ALIZALIWA MWEZI DESEMBA ?

Haya majira ya CHRISTMAS ; ni vema tukakumbushana kwa undani ni lini Yesu Kristo alizaliwa. Kwanza lazima tufahamu kwamba mwaka wa kiserikali unaanza katikati ya kalenda yetu, hii ya mfalme Gregory, yaani Julai; na utaratibu huu ulianza zamani sana uliletwa na Warumi; wakati wa kuzaliwa Yesu Kristo.

Warumi walikuwa wanatawala sehemu kubwa ya mashariki ya karibu na mbali. Na wakati huo kabla ya hii kalenda ya Mfalme Gregory, kila taifa lilikuwa na kalenda yake na zilitofautiana sana. Kwa mfano kalenda ya ISRAEL ilikuwa na miezi kumi na mbili (12).

Mwezi wa kwanza (1) uliitwa mwezi Abibu kwa sasa upo kati ya mwezi Machi na Aprili (KUTOKA ).

Mwezi wa pili (2) uliitwa mwezi Zivu kati ya mwezi Aprili na Mei (KUTOKA 23:25).

Mwezi wa tatu (3) uliitwa mwezi Sizvan kati ya mwezi Mei na Juni (1WAFALME 6:23).

Mwezi wa nne (4) uliitwa mwezi Tabuz kati ya mwezi Juni na Julai

Mwezi wa tana (5) uliitwa mwezi Abu kati ya mwezi Julai na Agosti

Mwezi wa sita (6) ulitwa mwezi Eluli kati ya Agosti na Septemba ( NEHEMIA 6:15)

Mwezi wa saba (7) uliitwa mwezi Tisri au Ethali kati ya mwezi Septemba na Oktoba (1WAFALME 8:2).

Mwezi wa nane (8) uliitwa mwezi Vuli kati ya mwezi wa Oktoba na Novemba (1WAFALME 6:38).

Mwezi wa tisa (9) ulitwa mwezi wa Tisloe kati ya mwezi wa Novemba na Desemba (NEHEMA 1:1).

Mwezi wa kumi (10) uliitwa mwezi Tebet kati ya mwezi wa Deesemba na Januari

Mwezi wa kumi na moja (11) uliitwa Sebath kati ya mwezi Januari na Februali

Mwezi wa kumi na mbili (12) ulitwa Adari kati ya mwezi wa Februali na Machi (ESTA 9:15-17)



Sasa tupige hatua kwa kutafakari Injili ya LUKA 1:26 nakuendelea; inasema wakati mimba ya Elizabeti ikiwa na miezi sita malaika alimtokea Mariamu. Wakati huo ulikuwa ni mwezi wa sita wa kutawala Herode. Kumbuka mwaka wa kiserikali unaanza mwezi wa saba inamaana ilikuwa mwezi wa 12 au Adari kwa Israel ambao ni mwezi wa Februali na Machi kalenda ya leo. Sasa toka Machi baada ya miezi tisa ni Desemba !. Tarehe inaweza kuwa sio sahihi kabisa lakini desturi za wayahudi ilikuwa kutahiriwa siku nane baada ya kuzaliwa (Lk 1: 59). Sasa toa siku nane baada ya kuzaliwa itakuwa ni Desemba 25.



Bwana awabariki sana. Amen
 
Sasa ni dhahiri Tundu Lissu ni Mcha Mungu.

==========

TUNDU LISSU: Ndugu wananchi wa Tanzania, tumsifu Yesu Kristo, Bwana asifiwe, mwanakondoo ameshinda, Assalam Aleykum Warahmatullah Wabarakatuh. Kesho ni sikukuu ya Noeli kwa wale wote wanaoamini katika dini ya Ukristo.
Kwa wakristo wote, Noeli ni sikukuu ya kuzaliwa kwa mwokozi wetu yesu Kristo aliyetolewa na Mungu kama yanavyosema maneno ya kitabu cha Yohana aya ya tatu mstari wa 16 'Ili kila mtu amuaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele'.

Sikukuu hii inatukumbusha kuhusu moyo wa kutoa na moyo wa kusamehe kwa sababu kama yanavyosema maandiko matakatifu, Yesu Kristo alizaliwa ili wote wanaomuamini wasemehewe. Katika kalenda ya Kikristo hii ndio siku ya furaha na sherehe kuliko nyingine zote lakini Krismas ni zaidi ya siku ya furaha na sherehe.

Ni siku pia ya kuwakumbuka na kuwasaidia wale wote walio na shida na matatizo mbalimbali, Mwinjilisti Ruth aliwahi kusema "Krismas ni krismas kweli tunaposheherekea kwa kuwapa mwanga wa upendo wale wanaouhitaji zaidi" Wapo wengi wanaohitaji mwanga huu wa upendo katika nchi yetu ya Tanzania katika kipindi hiki cha Noeli.

Mwaka 2020 ulikuwa mwaka mgumu na wenye machungu mengi kwa nchi yetu na kwa wananchi wetu, wote tulishuhudia haki yetu ya kuchagua viongozi tunaowataka ikipokwa kwa mtutu wa bunduki na kwa kutumia vyombo vya usimamizi wa uchaguzi na vya serikali visivotenda haki sawasawa, wapo ambao ndugu zao waliuawa au waliojeruhiwa na kulemazwa wakati wa uchaguzi mkuu na hata kabla ya hapo.

Wapo waliokamatwa na kustakiwa au wanaoendelea kushkiliwa magerezani au kwenye vituo vya polisi kwa tuhuma za uongo, uonevu na kwa sababu za kisisasa.

Wapo pia ambao wamefukuzwa kazi, wamebomolewa nyumba au kuharibiwa biashara zao au kunyang'anywa pesa na mali zao kwa madai ya uongo ya ukwepaji kodi au kwa tuhuma zisizo za kweli za uhujumu uchumi au utakatishaji fedha.

Wengine kama mimi mwenyewe wamelazimika kuikimbia nchi yetu kwa sababu ya njama na vitisho vya mauaji dhidi yao. Aidha, wapo kwa mamilioni mengi wanaosononeka kimya kimya kwasababu ya kutokupatiwa ajira au kkwa kutolipwa mishahara au pensheni zao halali au kwa kutotendewa haki zao nyingine mbalimbali.

Kwa wote hawa wenye njaa na kiu ya haki, ujumbe wangu wa Krismas ni uleule alioueleza mwandishi wa riwaya wa kimarekani, Taylor Caldwell, "Hatuko peke yetu, hata usiku unapokuwa wa giza zaidi au upepo wa baridi kali au ulimwengu unapoonekana kutokujali kabisa" Hatuko peke yetu, kwahiyo tusivunjike moyo au kukata tamaa, wiki ijayo katika salamu zangu za mwaka mpya nitawazungumza kwa kirefu kidogo juu ya maswala haya na mengine mengi na juu ya majukumu yetu kwa mwaka ujao kuhusu nchi yetu.

Nawatakieni sikukuu ya Noeli yenye furaha

View attachment 1658577
Kamanda ifike mahali uwachane na hii mambo.
 
Tutawasaliana na serikali ya ubelgiji. Ujerumani Canada uingereza na Marekani anakohaha kutafuta hadhi ya ukimbizi wasimpe kwa anajishughulisha na siasa za Tanzania wakati anaomba ukimbizi nchi zao
nani atawasilisha hayo malalamiko yako, Jiwe?!
kwa kingreza kipi hicho...kile cha kurudia rudia neno suppose kila sentensi?!?!
 
Mdomo wake umejaa matusi, hana maadali ya kikristo huyo labda kama ametubu. Amemdhalilisha sana Rais wetu, hana tofauti na Lucifer aliyewaaminisha malaika kuwa angepindua utawala wa Mungu.

Tangu nchi hii iumbwe uliwahi kumsikia Rais akiwaambia wananchi kuwa yeye Rais amekuwa akiwatukana mawaziri wake mara nyingi kuwa ni wapumbavu, zaidi ya huyu wa sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu alikosea sana kudhani kuwa uanaharaki ndiyo uongozi wa kisiasa. Uanaharakati una nafasi yake na uongozi wa kisiasa pia una nafasi yake. Nadhani kosa kubwa ni kwa wale waliomshambulia kwa vile walisababaisha aendelee kuwa relevant wakati tayari alikuwa ana fade out.
Mwenye akili hawezi kuwa relevant kwa mwendawazimu.

Kuna wakati, TL kwa wiki zima amekuwa akiandikwa na vyombo vya habari vya Dunia nzima, positively, kuliko mwanadamu yeyote. Kama hujui kuwa TL ni maarufu kiasi hicho, huo ni ujinga wako. Hakuna wa kukusaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu mnafiki sana, jamani huyu si ndio anayetaka tunyimwe hata msaada wa dawa za ukimwi eti kisa kukosa urais!! Ama kweli shetani akizeeka hujifanya malaika!
Hayo maneno kawaambir wajinga wenzio (CCM inapendwa na watu wajinga - TWAWEZA).

TL ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuomba kuwa Tanzania isiwekewe vikwazo vya kiuchumi bali vikwazo viwalenge viongozi madikteta na wale walioharibu uchaguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nani atawasilisha hayo malalamiko yako, Jiwe?!
kwa kingreza kipi hicho...kile cha kurudia rudia neno suppose kila sentensi?!?!
Wakalimani tunao kibao kwani lisu kingereza alikijulia wapi si Iliboru high school alikosomea HGL? Walimu wa HGL bado wapo hawajafa
 
Lissu alikosea sana kudhani kuwa uanaharaki ndiyo uongozi wa kisiasa. Uanaharakati una nafasi yake na uongozi wa kisiasa pia una nafasi yake. Nadhani kosa kubwa ni kwa wale waliomshambulia kwa vile walisababaisha aendelee kuwa relevant wakati tayari alikuwa ana fade out.
Tueleze pia kama 'udikteta' nao ni "uongozi wa kisiasa."

Kama unadhani "kosa kubwa ni kwa wale waliomshambulia" na kumfanya aendelee kuwa relevant, huoni kwamba unajichanganya kudhani kwamba alikosea kwa kuwa "mwanaharakati" ambaye unakiri bado yupo relevant?

Tueleze kosa lake ni nini hasa.
 
Mdomo wake umejaa matusi, hana maadali ya kikristo huyo labda kama ametubu. Amemdhalilisha sana Rais wetu, hana tofauti na Lucifer aliyewaaminisha malaika kuwa angepindua utawala wa Mungu.
Usihukumu usije ukahukumiwa
 
Tundu Lissu Mungu akubariki Sana maana hata vyombo vya ulinzi na usalama vinajua wewe unapendwa zaidi kuliko Pombe Magufuli ila kwakuwa wanatii mamlaka ya kaisari hawana namna.
 
Asante kwa taarifa mheshimiwa Rais wetu, jiwe na genge lake wanaotutawala kwa MABAVU wamepokea ujumbe wako pia.
 
Back
Top Bottom