Wanabodi.
Kwa maoni yangu, uchaguzi wa 2020, utakuwa sio uchaguzi bali utakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, sasa badala ya kufanya igizo la uchaguzi , si ni bora tumwache tu Magufuli aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?, na badala yake hizo fedha za uchaguzi zikaelekezwa kwenye maendeleo ?
11. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM, kwa Tume hii hii, na mazingira haya haya ukategemea kuna ushindani?, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli, bado kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea urais au kugombea ili kujifurahisha tuu?, ni kama kugombea kisu cha makali kuwili huku mmoja ameshika mpini, wengine kwenye makali kuwili, unategemea nini?, au hata ikitokea Mungu akafanya muujiza, huyo mgombea wa upinzani akashinda kwa muujiza wa Mungu, jee atatangazwa?.
Kwa maoni yangu, 2020 hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, kutakuwa tuu na igizo tuu la uchaguzi, na kwenye ubunge na udiwani , kwa udikiteta huu, sijui kama kuna mpinzani atatoboa!, uchaguzi wa 2020 itakuwa ni uchaguzi wa CCM only and only CCM!. Uchaguzi mwingine wa rais na uchaguzi wa vyama vingi ni uchaguzi wa 2025 only if ...(Mungu hatafanya yake hapa katikati)
Hayo ni maswali tu nimeanza kujiuliza aloud.
Je, wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?
Paskali