Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu iliyokuwa inaendelea Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imeahirishwa kwa muda usiojulikana mpaka pale shauri la mapitio lililowasilishwa Mahakama ya Rufaa na jamhuri kukamilika.
Leo Februari 24, 2026 baada ya kusikiliza wasilisho la upande wa mashtaka juu ya rufaa waliyowasilisha Mahakama ya Rufaa, akijibu taarifa hiyo mahakamani Lissu aliuomba upande wa Jamhuri kumkabidhi nakala ili aweze kujiandaa na shauri hilo la mapitio.
Lissu ameieleza mahakama kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 8(2D) cha sheria ya Mamlaka ya Rufaa kwamba hakiruhusu rufaa wala mapitio wala marejeo ya maamuzi ya mahakama ambayo hayamalizi shauri la msingi.
Ameeleza kuwa anafahamu hilo limefanyika kwa lengo la kurefusha mashauri haya ili aendelee kukaa gerezani “Hilo lengo ni kupeleka huko huku yasimame ili huyu mbaya wao aendelee kukaa gerezani.”
Amesisitiza “kwa vile wanalipeleka mahakama ya rufani nitawafuata huko huko na kwenda kuwashughulikia huko huko. Najua nitakaa gerezani lakini nitarudi hapa na tutakaporudi hapa tutaona jinsi ambavyo kesi yao ilikuwa imekufa” Lissu akizungumza kwa uchungu
Pamoja na hayo Lissu aliwasilisha changamoto anayopitia ya kukosekana kwa usiri akitembelewa na washauri wake wa kisheria jambo ambalo Ofisi ya DPP kupitia Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude umeeleza kuwa watayarekebisha malalamiko yote ya Lissu.
Soma