Tundu Lissu nenda taratibu, tumia hekima na busara kumaliza tofauti zako na Freeman Mbowe. Vinginevyo mnaiua CHADEMA

Mbona tofauti ziko kwenye mitandao tu!

Hapana ni tofauti ktk uhalisia wake kabisa japo Tundu Lissu huwa yuko very technical kila anapojaribu kueleza mambo yasiyo sawa ndani ya chama chao....

Na kwa wenye akili kupitia maelezo yake huweza kugundua moja kwa moja kuwa kuna makundi kinzani mawili ndani ya chama hicho, moja likienda na msimamo wa M/Kiti na jingine likiunga mkono msimamo wa M/M/kiti...

Hata hivyo, mimi tofauti kubwa ninayoiona kati ya hii miamba miwili ya siasa za vyama vilivyo nje ya serikali - opposition parties (i.e Freeman Mbowe & Tundu Lissu) ndani ya CHADEMA ni kuwa mmoja (TL) hana kifua cha mtu wa kufichaficha na kulealea mambo yasiyoenda sawa ndani ya taasisi...

Huyu nyeusi huisema ni nyeusi na sio bluu na koleo hulisema ni koleo na sio Kijiko kikubwa hadharani na popote...

Kwa mwenzie wa upande wa pili (FM), yeye ni aina ya wanasiasa wale wa kuuma na kupuliza huku waki - pet - peti na kubembeleza mbembeleza watu wakiamini kuwa "chama ni watu..."

Mara nyingi wanasiasa wa aina ya Freeman Mbowe huwa ni wanasiasa opportunists. Unaweza kuwa mbaya ndani ya chama lakini kama una maslahi fulani, hata ufanyeje utapetiwa petiwa tu. Lakini ukiwa mwanasiasa mzuri na ukaonekana uko kinyume na maslahi ya wanasiasa dizaini ya Freeman Mbowe, wanaweza kukufurusha asubuhi na mapema kabisa...!
 

Naona unaelezea tofauti za personality sio sera. Watu kutofautiana personality ni sawa kabisa hamuwezi kukubaliana kila kitu
 
Naona unaelezea tofauti za personality sio sera. Watu kutofautiana personality ni sawa kabisa hamuwezi kukubaliana kila kitu
Unaongelea kitu kimoja kilekile, yaani tofauti za kimitizamo inayotokana na kutokubaliana juu utekekezaji na uelekeo wa sera fulani ya chama ba inavyotendewa kazi...

Mfano sera za fedha za chama; zinavyopatikana na namna zinavyotoka na kutumika jambo ambalo linailetea shida kidogo CHADEMA na hii hutumiwa na wapinzani wao kama nyundo ya kuwapondea..

Kwa tofauti hizi za kimitizamo ya kisera ndani ya chama, obviously watu (wakiwemo viongozi) watatofautiana tu. Na namna kiongozi anavyozi - handle tofauti hizi na kuzielezea akiwa nje ya mifumo ya kichama ikiwemo vikao, moja kwa moja zita - expose personality ya mtu/kiongozi huyu huku nje....

Huu ndiyo msingi wa maelezo yangu hapo juu. Na ofcoz ndiyo msingi wa ushauri wangu kwa Tundu Lissu...

Na ndugu Kamundu, viongozi wanaongoza taasisi fulani huwa Kuna kitu kinaitwa "uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) bila kujali yamefanyika maamuzi sahihi au siyo sahihi..

Na kama kuna kiongozi anayeona kuwa hawezi kushiriki maamuzi ya namna fulani na wenzake, busara huelekeza kujitoa ktk maamuzi hayo kwa kuachia ngazi au kuachana na taasisi hiyo..

I know hiki anachokifanya TL ni kujaribu kuhakikisha taasisi hii (CHADEMA) inafanya maamuzi sahihi...

Lakini I know pia kuwa, kama hali hii itaendelea hivi, kuna hatari ya hawa watu kutengana na ikitokea na kwa hali ilivyo CHADEMA yaweza kukumbwa na msukosuko ambao haujawahi kutokea. Tundu Lissu si Dr Slaa wala Zito Kabwe wala Peter Msigwa...

CCM wako chobiz wanachochea mgogoro kwa nguvu sana. Hii colabo ya CHADEMA & Tundu Lissu & Freeman Mbowe hawaitaki na mataminio yao siku zote ni kuivuruga....

Wanasubiri uive kisha wapasue nazi...
 
Ukishaona imefika mahari watu ni wakubwa kuliko chama, ujue hapo hakuna chama kuna kikundi tu cha watu
 
Mmawia aione hii
 
Waendelee kukaza kiwakute cha boss wake na Marim seif
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…