The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Mimi The Palm Beach si mwanachama wa CHADEMA ila ni mpenzi na mfuasi wake na nakiunga mkono kwelikweli chama hiki...
Ni wazi kuwa Kuna mgogoro mkubwa kati ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wake Tundu Lissu ndani ya CHADEMA
Nitasikitika na kuumia sana kama chama hiki cha siasa kilicho tegemeo pekee la Watanganyika nacho kitafuata njia ya CUF, TLP na NCCR - MAGEUZI kujidhoofisha na kisha kwenda kujifia zake huko.
Na naona wazi kabisa, kazi hii ya kukisambaratisha chama hiki inafanywa na viongozi wenyewe kwa kujua au kutojua.
Mpaka hatua hii, haina shaka kuwa iko shida ndani ya CHADEMA hususani kwa viongozi wakuu wa chama. Ili kukiokoa chama hiki na kuhifadhi moto wake uliowashwa kwa miaka takribani 30 sasa usizimike ni lazima ifanyike intervention ya haraka kuzuia hali hii isifikie point of no return.
Press Conference ya Tundu Lissu huko Singida leo imethibitisha shaka yangu hii.
Kila alichoki - address kule Singida mbele ya waandishi wa habari kuhusu uchaguzi wa serikali za vijiji na mitaa hakina shida, ni kizuri na ni kweli hali ndivyo ilivyo
Lakini mwishoni alipoulizwa swali na waandishi wa habari kama hiyo ni kauli ya chama ama la na yeye kujibu kuwa, kila alichokisema hapo ni cha yeye Tundu Lissu na sio kauli ya chama na kwamba baadaye ndio atapeleka hoja hizo ndani ya chama na kushinikiza ziwe ni kauli rasmi ya chama, nikawa shocked kidogo na kuliona tatizo hili ninalolisema hapa kwa uwazi kabisa...
Hii ya Singida ni mwendelezo wa tukio na kauli nyingine aliyoitoa kule Same - Kilimanjaro. Hii ya Same ilimshambulia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe moja kwa moja bila kificho....
Kauli ya Tundu Lissu kule Same - Kilimanjaro aliitoa baada ya kusambaa kwa tuhuma kuwa, ule mkutano uliokuwa uhututubiwe na yeye huko Same, eti ulizuiliwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kwa kushirikiana na CCM kwa kutumia Polisi...
Ieleweke kuwa hoja hapa si kuzuiliwa kwa mkutano huo iwe ni kwa sababu hiy kweli au nyingine....
Tatizo ni namna Tundu Lissu alivyoshughulikia tuhuma hizo zilizomuhusisha Mwenyekiti wake...
Kauli yake kule Same Kilimanjaro ilikuwa hii, nanukuu;
"........Kama ni kweli, basi nyie ndiyo wenye chama, ndio wanachama wa chama hiki. mnapaswa kujiuliza Je, kila anayevaa makombati haya ni mwenzetu kwa kiasi gani kama anaweza kushirikiana na wabaya wetu kutuhujumu. Ila kama tuhuma hizi sio za kweli, basi mtanisamehe.."
Hii statement ni tata sana. Ni kama vile Makamu Mwenyekiti alishajiridhisha kuwa ni kweli Mwenyekiti wake ametenda hivyo na akaisema indirectly ili kupeleka ujumbe mahususi kwake...
Kwa kawaida, mimi nilifikiri kuwa, kabla ya kusema lolote, basi Makamu Mwenyekiti alipaswa kutumia hekima kidogo ya kuwasiliana na Mwenyekiti wake na kupata kauli yake juu ya tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake. Na majibu ya Mwenyekiti ndiyo yalipaswa kuwa mwongozo wake kujibu hoja hiyo hadharani mbele ya umma...
Lakini kwa kauli yake hii, moja kwa moja inaonesha kuwa hakuwa amewasiliana na Mwenyekiti wake.
Na kama ni hivyo, napata shaka kuelewa kama hata Mwenyekiti na ofisi kuu ya chama (katibu mkuu na mtendaji mkuu wa chama) kama walikuwa wanajua kuwa Makamu Mwenyekiti wao atakuwa ziarani Same - Kilimanjaro siku hizo.
USHAURI:
CHADEMA kaeni chini, malizeni tofauti zenu amicably. Na kama kuna mambo yanayokwanza wengine, basi yashughulikiwe haraka ndani ya chama kwa taratibu za wazi za kichama....
Kuonesha tofauti zenu waziwazi huku nje ni hatari sana na wapinzani wenu wakuu CCM watatumia mwanya na udhaifu huu kuwamaliza kabisa na kusambaratika Moja kwa moja...
Hiki (Anguko la CHADEMA) ndicho CCM wanachokisubiri kukiona kikitokea Ili waweze kupumua....
Na hili la kuisambaratisha CHADEMA likitokea mikononi mwenu wewe Freeman Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika na Kamati kuu kwa ujumla fahamuni leo kuwa, mtalipa gharama kubwa sana Ili Watanganyika wawasamehe...!!!
CC: Erythrocyte